Uislamu hauharamishi kujenga makanisa

  • | Friday, 7 August, 2015
Uislamu hauharamishi kujenga makanisa

Kwa hakika Uislamu unaheshimu dini ya wengine kupitia kwa yaliyokuja katika Qurani tukufu, Mwenyezi Mungu Anasema (Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini). {yunus:99}
Kuanzia kwa msamaha huu na mtazamo wa Qurani kuhusu utofauti wa kidini, basi mtume (S.A.W) Amewadhamini wasio waislamu uhuru wa kutekeleza ibada za dini yao, kwani Uislamu hauwalazimishi watu kuacha dini yao kwa sababu Hapana kulazimisha katika Dini, kwa hivyo Uislamu umewaruhusisha kutekeleza ibada ya dini yao katika mahala pa ibada yao, na umelinda mahala pa ibada yao, na umeharamisha mashambulizi ya aina zote yanayolenga makanisa na mahala pa ibada kwa wasio waislamu.
Bali Qurani tukufu imejaalia Jihadi ya waislamu kwa ajili ya kuzuia uvamizi ni sababu ya kulinda mahala pa ibada ili kutoporomoka, Mwenyezi Mungu Anasema (Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. ){al hajj:40}.
Ibn Abbass Anasema nymba za wat'awa ni: ambapo wata'wa wanakuwepo ndani, na na makanisa ni: hekalu za mayahudi, na, na masinagogi ni : makanisa ya wakristo.
Na Mtume (S.A.W) Ameandika kwa askofu wa Banil Hareth ibn Kaab na askofu wa Nagraan na makuhani, wata'wa, na wafuasi wao (kwamba hawatachukui wanayoyamiliki ikiwa nyingi au chache kutoka mali yao, mahala pa ibada zao na hatawafukuza kutoka Madina , na hatabadilisha viongozi wa dini yao , wala hatafuta haki zao wala kiongozi wao, kama wakitoa nasaha bora na wametekeleza wajibu bila ya kudhulumu au kudhulumiwa) . {Tabakat Ibn Saad 1/266}.
 
Na bwana Omar Ibn EL Khattab ametoa mfano bora alipoandika katika ahadi yake kwa wakazi wa Al Quds kwamba amedhamini uhuru wa dini yao na kuwapa usalama kwa nafsi zao, na amani kwa makanisa, na imekuja pia katika ahadi yake kwa watu wa Iylyaa ( amewapa usalama kwa nafsi zao, mali zao, makanisa yao, misalaba yao, wagonjwa wao, wazima wao na mila zote zao na kwamba waislamu hawataishi katika makanisa yao, wala kuyaporomoka, wala kuchukua kipande kutoka kwa makanisa yao, wala misalaba yao, mali zao wala kulazimishwa kuacha dini yao……)
Na Omar Ibn El Khattab amekataa kusali katika kanisa moja alipoingia mji wa Al Quds, na ameswali kwenye mlango wa kanisa ili waislamu wasije baadaye na kuchukua kanisa hilo kwa sababu bwana Omar Ibn El Khattab amesali hapa , na Uislamu umekiri haki ya wakristo katika kujinga  makanisa ambao wanaweza kutekeleza ibada yao kutokana na kuheshima utofauti wa dini iliyokiriwa na Uislamu, na umewaharamisha kuporomoka makanisa au kuyalipua, au kuwaua watu waliyomo ndani yake, au kuwatishia na umezingatia hayo miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa, Mtume (S.A.W) Amesema (aneyemdhulumu Myahudi au mkristu (walioishi katika nchi za kiislamu) au kupunguza haki yake, au kumlazimisha kulipa Jizyah zaidi, au kuchukua kitu bila ya kuridhia kwake, basi mimi ni mlinzi wake siku ya kiyama)(Abu Dawood:3052).

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.