Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu mjini Abuja, Nigeria

  • | Wednesday, 18 May, 2016
Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu mjini Abuja, Nigeria

Akipokelewa na makaribisho rasmi na kiraia makubwa….Mheshimiwa Imamu mkuu afika kituo cha mikutano kwenye mji mkuu wa Nigeria, Abuja…ambapo atatoa hotuba kwa mataifa ya kiafrika na waislamu wote duniani, kumbi lenyewe limejaa kwa maelfu ya waliohudhuria kati ya wananchi wa Nigeria kwa makundi na madhehebu yao tofauti ili kusikiliza hotuba ya Imamu Mkuu…

•     Nimekuja hapa ili kusisitiza kuwa Uislamu haikuitia vurugu au ugaidi hata kidogo…bali ni dini ya ubinadamu, amani na usalama.
•    Waislamu hawakufikiria kabisa kusafiri hapa na pale ili kuitetea dini yao na kudhihirisha kiini chake na ukweli wake.
•    Makundi ya ugaidi yanataka kuuchafusha Uislamu katika ulimwengu wote na kuutuhumu kwamba ni dini ya vurugu, umwagaji damu na ukatili.
•    Tafuteni nani atakaefaidika kutoka ghasia hiyo wanaosababisha jinai hizo kwa mali, silaha, na mipango wakipata sababu za uwongo za kuhalalisha jinai hizo.
•      Uislamu ni jina la dini la pamoja ambayo manabii wote waliwaita watu waamini kwayo, na waumini walijinasibisha kwayo.
•    Ujumbe wa Uislamu unafanana na jumbe zilizopita katika madhumuni na ukweli.
•    Qur'ani inawaona watu wote kwa usawa na kwamba wametokana na baba mmoja na mama mmoja.
•    Qur'ani inathibitisha ukweli wa yaliyokuja katika vitabu vya mbinguni vilivyopita na inavisifu vitabu vya Taurati na Injili kwamba ni uongofu na nuru.
•     Kutofautiana ni jambo la kiungu lililopitishwa katika matini thabiti za Qur'ani.
•     Haikubaliki kiakili wala haitakuwa kwa hekima kwamba Mwenyezi Mungu Alitaka kuwaumba watu na kuwajaalia tofauti kisha Awaamuru watu walazimishwe juu ya yaliyo kinyume na maumbile yao waliyoumbwa nayo au Awaamuru wapiganiwe ili Awalazimishe kufanya kinyume cha matakwa yake kuhusu maisha yao.
•    Uislamu ndio dini ya amani na usawa na yanayosemwa kinyume cha hayo ni uwongo mtupu.
•    Hekima ya kupitisha kupigana na wengine katika Uislamu ni kujitetea na kuziba uadui sio kwa sababu ya kukufuru kwao au kutokuwa waislamu au kuhitalifiana katika dini.
•     Historia haikutuambia kuhusu vita moja kati ya vita vya kiislamu kwamba waislamu waliwapa wenyeji wa nchi yo yote hiari ya kuchagua ama kujiunga Uislamu au kuuawa kwa upanga.
•    Hatuna budi kupandisha sauti ya ufahamu wa kweli na kushuka kwa maulamaa na kudhibiti ghasia ya kutoa fatwa katika dini.
•    Maulamaa wa waislamu wanapaswa kulazimika majukumu yao kubainisha ukweli wa dini hiyo ambayo inaombea undugu, kujuana na amani baina ya watu wote mashariki na magharibi.
•      Hatuna budi kutoka kurejea fiqhi ya kutofautiana kwa maana yake iliyo sahihi ambayo inategemea kutofautiana kama ni chanzo na sababu ya kuupa umma nguvu na kustawisha ustaarabu wake katika enzi kadhaa.
•    Inapaswa kwamba yaliyokubaliwa na maulamaa wa umma ndiyo kipengele cha kutofautisha baina ya yaliyo sahihi na yaliyo kosa na wala tusiainishe madhehebu moja tu kwa watu katika itikadi na ibada kwa ulazimisho kisha tuwahimiza kuifuata mara kwa kuvutia na mara nyingine kwa kuogopesha.
•    Ghasia ya kutofautiana isiyo na mipaka wala vidhibiti ya kielimu ndiyo iliwasababishia waislamu kupatwa na misiba ya ukafirishaji na vurugu.
•    Al-Azhar inaongoza juhudi kubwa ili kueneza mfumo wa uwastani na amani na kutoa maelezo ya hatari za mawazo makali.
•    Ziara yetu nchini Nigeria ni ya kuhakikisha msaada wa Al-Azhar Al-Shareif na kuunga mkono wake kwa umoja wa wananchi wa Nigeria japokuwa madhehbu, makundi, tabaka za jamii zake zote tofauti.
•    Tumeamua kuzidisha tuzo za mafundisho kwa wana wa Nigeria kutoka tuzo 30 hadi 50 kila mwaka na kuhusisha vitivo vya kisayansi kama vile uganga, matibabu na uhandisi kwa ziada hiyo.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.