Mwishoni mwa ziara yake kwa Nigeria…

  • | Wednesday, 18 May, 2016
Mwishoni mwa ziara yake kwa Nigeria…

Mwishoni mwa ziara yake kwa Nigeria…
Imamu Mkuu akutana na Rais wa Nigeria kwenye ikulu ya urais jijini Abuja..na asisitiza kwamba:

•    Tuna hamu ya kupambana na mawazo makali katika ulimwengu wote..na hatutachelewa kufanya hivyo hata kidogo.

Rais wa Nigeria:

•    Ziara yako ewe Mheshimiwa imewafurahisha wanigeria..tunatambua juhudi za Al-Azhar kueneza uwastani na amani.
•    Ziara yako kwa kambi ya wakimbizi ni kazi ya kiutu…tunakushukuru kwa kuwazingatia na kuchunga wanafunzi wanigeria wanaosoma katika Al-Azhar.


Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu, alikutana na Rais wa Nigeria; Mohammad Bukhari kwenye ikulu ya urais katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Mheshimiwa imamu mkuu alisisitiza katika mkutano huu kwamba Al-Azhar Al-Shareif ina hamu na utashi kubwa ya kupambana na mawazo makali katika ulimwengu kote, akibainisha kuwa kipindi kijacho kitashuhudia kufanya juhudi zaidi hasa barani Afrika kwa ajili ya kuwafahamisha watu na kuwaonya kutoka hatari za ugaidi na vurugu.
Akaongeza kuwa Al-Azhar Al-Shareif kwa kushirikiana na baraza la wakuu wa waislamu ina lengo wazi ili kuimarisha misingi ya amani, upendo na kuishi pamoja baina ya mataifa na jamii tofauti kwa ajili ya kueneza amani baina ya wanadamu wote duniani.
  Kwa upande wake, Rais wa Nigeria alimkaribisha sana Mheshimiwa Imamu mkuu na wajumbe wanaoambatana naye, akibainisha kwamba ziara hiyo ya imamu mkuu imefurahisha sana wananchi wote wa Nigeria na imewapa hisia ya fahari, ambapo taifa la nchi hiyo wanaheshimu sana Al-Azhar Al-Shareif na Imamu wake.
 Mwanzoni mwa mkutano Rais wa Nigeria amemwombea Imamu mkuu atoe nasaha ambazo zinaweza kuchangia kutekeleza matamanio ya wananchi wa Nigeria kwa kuzingatia wananchi hawa wote ni waislamu, akisisitiza kwamba ziara ya Imamu mkuu inazingatiwa msaada kwake binafsi katika kutekeleza majukumu yake ya kupitisha uadilifu wa kijamii baina ya wananchi wote wa Nigeria.
Rais wa Nigeria alitoa shukurani zake zote kwa Imamu mkuu kwa ziara hiyo ya kihistoria, akieleza heshima yake na ya wanigeria mkubwa kwa ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu kwa kambi moja ya wakimbizi jijini Abuja, akisisitiza kuwa ziara hiyo inaelezea msimamo wa kiutu wa Imamu mkuu ambayo utakuwa na athari kubwa mno sio kwa wakimbizi hawa tu bali kwa wananchi wa Nigeria wote.
Vile vile, rais wa Nigeria alieleza heshima yake kubwa kwa Al-Azhar Al-Shareif na Imamu wake mkuu juu ya juhudi anazozifanya kuchunga wanafunzi wa kinigeria wanaosoma katika Al-Azhar Al-Shareif.
Mkutano huu ulihudhuriwa na wahusika kadhaa kutoka upande wa Nigeria alihudhuria Mheshimiwa Sheikhi Ibrahim Swaleh Al-Husainy Mufti wa Nigeria, na baadhi ya mawaziri na wahusika wa serikali ya Nigeria, wakati ambapo upande wa wajumbe walioambatana na Imamu mkuu walikuwa ni: profesa; Ibrahim Al-Hudhud mkuu wa Chuo kikuu cha Al-Azhar, profesa; Abu Zeid Al-Amir mkuu wa idara kuu ya taasisi za Al-Azhar, profesa; Abdul-Fattah Al-Awariy mkuu wa kitivo cha Usuul-Diin, profesa; Ali Al-Noeemiy katibu mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu, kadhi Mohammad Abdul-Salam mshauri wa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar na mwanachama wa ofisi tekelezi ya baraza la wakuu wa waislamu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.