Chuo kikuu cha Al-Azhar chazindua mkutano wa kimataifa wa viongozi wa Elimu ya Juu Barani Afrika

  • | Tuesday, 9 July, 2019
Chuo kikuu cha Al-Azhar chazindua mkutano wa kimataifa wa viongozi wa Elimu ya Juu Barani Afrika

     Mkutano wa kimataifa wa viongozi wa elimu ya juu Barani Afrika unaopangwa na Chuo Kikuu cha Al-Azhar kwa kushirikiana na umoja wa Vyuo Vikuu vya kiafrika ulianza sasa katika kituo cha Kimataifa cha Al-Azhar cha mikutano na unaendelea hadi Julai 11.

Mkutano -unaofanyika kila miaka miwili- chini ya anuani ya «jukumu la taasisi za elimu ya juu katika kuimarisha mkakati wa elimu ya juu Barani Afrika», unaofanyika kwa mara ya kwanza mjini Cairo sanjari na uraisi wa Misri kwa Umoja wa Afrika, na chini ya ulezi wa Rais Abdel Fattah Al-Sisi, Rais wa Jamhuri.

Mkutano huo unazingatiwa kuwa mkutano mkubwa zaidi kwa wahusika wakubwa kutoka taasisi za elimu ya juu, kwa lengo la kutafiti na majadiliano ya pamoja kwa masuala yanayowashughulika na masuala yenye umuhimu kwa ajili ya kuendeleza elimu ya juu katika Vyuo Vikuu na taasisi za kielimu kwa ujumla, na Afrika hasa.

Wanashiriki katika mkutano huo ni 300 kutoka kwa wakuu wa Vyuo Vikuu na wawakilishi taasisi za kimataifa, na wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 40 kutoka Mabara yote ya dunia, na vyuo vikuu vya 180 na taasisi za kimataifa za 43.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.