Jukumu la vijana katika mageuzi na marekebesho ya jamii

  • | Thursday, 5 September, 2019
Jukumu la vijana katika mageuzi na marekebesho ya jamii

     Vijana ni msingi wa taifa, umuhimu wa vijana uko katika kuwa wanaume wa taifa na mzizi wake na siri ya kuwepo kwake, kwani wao ni watakaostahmili mzigo wa ujumbe, na kupitia kwao Uislamu umeimarika. vile vile umuhimu wa vijana unarejea kuwauliza juu ya ujumbe huo mara mbili katika siku ya mwisho, ambapo imesimuliwa katika Hadithi kuwa Mtume (S.A.W) amesema: (Itakapokuwa siku ya Kiama, miguu miwili ya mja haitatele­za (haitavuta hatua) hadi kwanza aulizwe juu ya mambo manne: umri wake aliupoteza katika nini; elimu yake alifanya nini kwayo; mapato yake aliyapata kutoka wapi na aliyatumia katika nini, na mwili wake aliuangamiza katika nini).

Kwa hivyo vijana wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, kwani mwamko wa taifa unasimamika juu ya mwamko wao, rika la vijana ni kipindi bora zaidi cha marika ya umri, vijana katika rika hilo la umri wanaburudika kwa nguvu na shughuli, ambapo vijana wanaweza kutumia vizuri hisia zao zote, na kunufaika nazo. Rika la vijana linasifika kuwa ni kipindi ambacho mwili unakuwa wenye muundo nguvu, kwani kijana anapita kipindi cha utotoni, lakini bado hajaingia rika la uzee. Vijana wanazingatiwa kuwa ni watu wa kesho, wajenzi wa siku zijazo, na wao ni msingi wa kulea vizazi, hivyo uongozi wa taifa unategemea vijana katika nyanja zake mbalimbali na masuala yake. Maslahi ya taifa inategemea maslahi ya vijana

Vijana ndio msingi wa maendeleo ya taifa na tegemeo la mwamko wake, kwa sababu vijana ni kilicho ghali kinachomilikiwa na taifa. Kama unataka kujua mustakabali wa taifa lolote, basi usiuliza juu ya dhahabu yake na hazina yake ya kifedha, lakini unaweza kuona vijana wake na yanayowashughulia, ukiwaona vijana hao wanashikilia kwa Dini, basi ujue kuwa ni taifa kubwa lenye hadhi nzuri na ujenzi nguvu, na ukiwaona vijana hao ni wenye maadili mbaya wanashughulika mambo duni, na kutendea maovu, basi ujue kuwa ni taifa dhaifu, litakaoanguka kwa haraka mbele ya adui yake, kwa hivyo basi vijana ni msingi wa taifa.

Vijana katika wakati wa kale na hivi sasa walikuwa katika taifa lolote ni msingi wa mwamko wake, nao katika kila mwamko ni siri ya nguvu zake, nao katika kila wazo ni wenye kubeba bendera yake: (Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu.) (Al-Kahf: 13).

Vijana wana jukumu kubwa katika maendeleo na ujenzi wa jamii, na jukumu yao hiyo haihusiani na uwanja maalum, bali inaingiliana na nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi, na sekta mbalimbali za ustawi, kwani wao wana lengo kuu zaidi katika jamii, na kuwa harakati (mchakato) ya mageuzi na maendeleo haisimamika mipaka maalumu kwao, kwani wao ni msingi wa mageuzi na nguvu unaoweza kuyafanya, kwa hivyo basi ni lazima kuwa kuvutia nguvu zao ni kipaumbele cha taasisi zote.

Vijana waislamu walikuwa na jukumu kubwa katika ujenzi wa uma, na juu ya mabega yao staarabu zimezuka, na walikuwa na athari kubwa katika mwamko wa uma wa Kiislamu katika zama zote na nyanja tofauti tofauti, basi ni haki yao kuwa ni mifano mema na ruaza njema kwa vijana wa taifa katika zama zote.

Vijana ni wenye haraka kwa kukubali wito za kimarekebesho, ambapo wamekabiliana na batili, na walikuwa na haraka katika kukubali haki, kwa sababu ni wenye mioyo nyepesi yenye huruma, na wenye roho nyamavu, na hawana matarajio katika maisha kama hali ya wazee.

Miongoni mwa mifano mikuu iliyopigwa na vijana katika enzi ya Maswahaba ni Zaid Ibn Thabit ambaye ni mfano mzuri sana aliyeusiwa na Mtume (S.A.W) ajifunza lugha ya kisiriani. Zaid Ibn Thabit alisema: aliniambia Mtume (S.A.W), je unajua kisiriani? Nikasema: hapana. Mtume‎ (S.A.W) akasema: uijifunze, kwa kuwa vitabu vyake vinatujia. Zaid alisema: niliijifunza katika siku kumi na saba. Al-‘Amash alisema: ilikuwa ikamjia mtume ‎(S.A.W) ‎vitabu ambaye hapendi kuviangalia ila anayemwaminika. Kutoka hapa Zaid aliitwa mfasiri wa Mtume‎(S.A.W). Mfasiri huyu wa Mtume‎(S.A.W)‎ alikuwa na umri gani? Miaka 13!! Baada ya hayo amelazimishwa kwa kukusanya Qur’ani katika utawala wa Bwana wetu Abu Bakr (R.A).

Na Zaid alisimama na kumaliza vizuri kazi hiyo, ambapo alikuwa analingana na kupinga na kuchunguza mpaka alikusanya Qur'ani kwa uratibu. Zaid alisema kuhusu ukubwa na uzito wa jukumu hilo: (Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau wangalinikalifisha kwa kuhamisha mlima kutoka mahala pake, basi ingalikuwa jepesi kwangu kuliko waliyoniamrisha na ukusanyaji wa Qur'ani). Na Zaid alimaliza kazi hiyo kwa ukamilifu na kukusanya Qur'ani katika msahafu moja.

 

 

 

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.