Bunge la kimataifa lasifu juhudi za Al-Azhar katika kusaidia kupatikana amani ulimwenguni

  • | Friday, 8 November, 2019
Bunge la kimataifa lasifu juhudi za Al-Azhar katika kusaidia kupatikana  amani ulimwenguni

      Mheshimiwa Imamu mkuu, Prof/ Ahmad El-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, amempokea Balozi / Mukhtar Omar, Mshauri mkuu wa katibu mkuu wa umoja wa bunge la kimataifa. Mwanzoni mwa mkutano, Mheshimiwa Imamu mkuu alimkaribisha Balozi Mukhtar na akieleza tathmini yake kwa jukumu kubwa linalofanywa na umoja kwa ajili ya kufanikisha maadili ya amani, na haki za kibinadamu, na kuwapa vijana nafasi ya maendeleo ya kudumu kupitia mazungumzo, ushirikiano na kazi za kibunge. Kwa upande wake, Balozi Mukhtar Omar alitoa shime yake kutokana na jukumu la wazi la Al-Azhar katika kuimarisha maadili ya kuishi kwa pamoja, na muono wa Mheshimiwa Imamu mkuu wenye hekima kwa ajili ya kueneza usamehevu katika nchi mbali mbali na wananchi wake, akielezea kuwa umoja wa bunge la kimataifa liko tayari kwa kushirikiana kwa pamoja katika kueneza na kuimarisha misingi ya juu iliyoidhinishwa na hati ya udugu wa kibinadamu.

Print
Tags:
Rate this article:
1.0

Please login or register to post comments.