Taarifa ya Al Azhar kuhusu Libya

  • | Tuesday, 23 June, 2020
Taarifa ya Al Azhar kuhusu Libya

     Al-Azhar inaunga mkono msimamo wa Misri kuhusu kila inayohusiana na hatua za kuhifadhi usalama wa kitaifa wa Misri na kulinda mipaka yake.

Al-Azhar inaunga mkono suluhisho la amani nchini Libya na inatoa wito tena kwa ajili ya kusimamisha kufyatua risasi na kuyaendelea mazungumzo.
Al-Azhar inafuata kwa wasiwasi vita vinavyoendelea baina ya Walibya, na uingizaji wa nchi za nje zenye malengo zinazosababisha ugawaji zaidi baina ya wananchi wa Libya.
Al-Azhar inakariri kukataa kwake kwa msingi wa ulinzi ambayo baadhi ya nchi zinajaribu kuufaradhisha kwa ulimwengu wa kiarabu, na kuuchukua kama kisingizio kwa ajili ya kukiuka utawala wake, ikitoa wito kwa kuchukua msimamo wa pamoja wa kiarabu kuhusu kutatua mgogoro huo, na ikielekeza wito wake kwa wananchi wa Libya kwa dharura ya kuwa pamoja na kuweka mbali hitilafu na ugawaji unaofanya Libya kuwa nafasi kwa ukoloni na uingizaji wa nchi nyingine.
Aidha Al-Azhar inaunga mkono msimamo wa uongozi wa kimisri kuhusu hatua zote zitakazochukuliwa kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa kitaifa wa Misri na kulinda mipaka yake, ikiunga mkono wito wa Misri kwa kutatua suala la Libya kupitia suluhisho la amani, na wito wa kweli wa raisi Abdelfattah El Sisi kwa kusimamisha kufyatuwa risasi katika Libya yote, na kuendelea mazungumzo chini ya ulinzi wa Umoja wa matiafa kwa ajili ya kuhakikisha utulivu wa Libya, amani na umoja wa wananchi wake.
Al-Azhar inaelekeza ujumbe wa uungaji mkono kwa bingwa wa Misri,  maofisa na askari wa jeshi wanaolinda mipaka, ikimwomba Mwenyezi Mungu awahifadhi na kuwalinda kwa macho yake yasiyopati usingizi, na kuwafanyikia kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Pia Al Azhar inamwomba Mwenyezi Mungu kuwajumuisha Walibya, na kuunganisha maamuzi yao, na kuwaepusha Libya na Walibya chungu ya vita na ole wa migogoro, na kuhifadhi Libya na wananchi wake na nchi za kiarabu kwa kila uovu na ubaya.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.