Elimu sahihi ni kinga kwa vijana na jamii dhidi ya fikra kali

  • | Monday, 29 June, 2020
Elimu sahihi ni kinga kwa vijana na jamii dhidi ya fikra kali

     Tukio la siasa kali na ugaidi ni moja ya matukio yanayoenea sana ulimwenguni, mpaka yakawa kama kilele cha mgogoro wa kwanza wa ustaarabu ambayo tunaishi leo. Hakuna nchi fulani ambayo haina kundi linalobeba silaha au angalau kundi la watu ambalo hubeba fikra kali ambayo inaleta vurugu inayopelekea kupambana na nchi na jamii. 
Ili kukabiliana na tukio hili hatari au hata kulipunguza, ni lazima kuamsha roli ya elimu sahihi kama njia bora ya kushinda mgogoro huu wa kiustaarabu; wa kuzidisha siasa kali na ugaidi, kwa sababu kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya elimu na tukio la siasa kali na ugaidi, wakati inapoenea zaidi athati ya elimu nafuu katika jamii, umepungua mwelekeo wa watu wa jamii hii kwa kukumbatia siasa kali au kuifanya, pia wakati inapopungua athari ya elimu nafuu katika jamii, umezidi mwelekeo wa watu wa jamii hii kwa kufuata mawazo yenye siasa kali au kuifanya Katika mfumo wa ugaidi.
Aya ya kwanza kuteremshiwa Mtume (S.A.W) ilikuwa wito wa kutafuta elimu. Wito huo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ulitokana na kutambua mchango na nafasi ya elimu katika kuendeleza jamii na kuilinda nchi na dunia nzima kutokana na maovu na mabaya ya aina zote. Katika aya hii, Mwenyezi Mungu Alitoa amri kwa Mtume wake asome. Kusoma ndiyo msingi na hatua ya kwanza kabisa ya kutafuta elimu. Aya hii inaonesha kwa wazi athari ya elimu na nafasi yake katika Uislamu. Mwenyezi Mungu Anasema: “Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.” [AL - A'LAQ: 1-5].
Elimu ni njia ya pekee ya kuleta amani na utulivu kwa umma. Elimu inawahimiza wananchi kuendeleza na kulinda jamii na nchi yao, na ndiyo maana siyo jambo la kushangaza kukuta Uislamu ukiipa elimu heshima kubwa na kuwapa wanazuoni cheo cha juu kabisa mpaka wakawa warithi wa Manabii na Mitume.
Kama hiyo haitoshi, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amewafanya wanazuoni kuwa mashahidi wa Upweke wake kama Alivyosema katika Qur’an: “Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” [AL I'MRAN:18].
Naye Mtume (S.A.W) aliwafaradhishia Waislamu kutafuta elimu na akabainisha ubora wa wenye elimu mbele ya wasio na elimu. Uislamu unawataka Waumini kujifunza. Kwa kuwa vijana ndiyo nguzo muhimu zaidi katika umma wowote, basi wao wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha ili waweze kukabiliana na mawimbi yanayowavutia katika fikra kali na misimamo ya kigaidi.
Kuna majaribio mengi ya kushawishi vijana kuingia kwenye misimamo mikali. Wale wanaowashawishi vijana wanaelewa uwezo wa kundi hili wa kujenga au kuangusha umma wowote. Ni kwa sababu hii, tunawahimiza vijana wajikinge na majaribio ya ushawishi huu wa kuingizwa katika mambo mabaya.
Kinga kwa kijana dhidi ya majaribio hayo haitapatikana isipokuwa kupitia elimu. Ni elimu ndiyo itakayowakinga vijana dhidi ya mafisadi wanaojitahidi kuchafua akili zao na kuwatumia vibaya. Pia ni kazi yetu kuwakinga na kulinda vijana wetu dhidi ya shari na fitina hizo. Kazi hiyo ni jukumu kubwa ambalo Al-Azhar Al-Sharif kupitia taasisi zake husika inajitahidi katika kutekeleza jukumu hilo kwa uwezo wake wote kwa kuelimisha vijana na kuwafahamisha ili wasiwe mateka rahisi chini ya mikono ya makundi ya kigaidi.
Inafahamika kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya umma na ni moja ya sababu zinazopelekea katika mafanikio. Kwa hiyo basi, jamii isiyo na elimu ni rahisi kushawishiwa na kuharibika na ndiyo maana makundi ya kigaidi yanajaribu kuwavutia vijana wasio na elimu ya kuwasaidia kupembua haki na batili.
Kama ilivyotangulia kusema, mafisadi wanatambua nafasi na uwezo wa vijana katika kubadilisha mambo katika umma; na hakika hiyo ndiyo sababu watu hao wanaotaka kueneza vurugu na ugaidi duniani wanapenda kuwatumia vijana. Watu hao wabaya wanajua kuwa, vijana ndiyo silaha muhimu ya umma wowote, ndiyo msingi wa maendeleo ya umma na ndiyo tegemeo la jamii. 
Vijana ni hazina ya kiuchumi, kijeshi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Lakini hazina muhimu iliyo ndani ya vijana kwa umma wowote ni hazina ya utu. Kama ukitaka kujua mustakabali wa taifa lolote, basi usiuliza juu ya dhahabu yake na hazina yake ya kifedha, bali angalia vijana wake na mambo gani wanayoshughulikia. Ukiwakuta vijana hao wanashikilia dini, tambua kuwa hilo ni taifa kubwa lenye hadhi nzuri. Ama ukiwakuta vijana wamepoteza maadili na wana tabia mbaya, basi ujue kuwa ni hilo ni taifa dhaifu (nyonge) litakaoanguka kwa haraka mbele ya madui zake. Kwa hivyo basi, vijana ni msingi wa umma na sababu ya kuimarika au kuanguka kwake.
Watu, taasisi na mamlaka mbalimbali, ni lazima zipambane na ugaidi, ili walioshawishiwa kuharibu nchi, kufanya vurugu na mauaji, kusababisha ghasia na uharibifu wa aina yoyote, waelewe kuwa wanafanya hatia kubwa zilizokatazwa katika sheria ya Kiislamu.
Na kwa upande wake, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra kali kinajitahidi sana kupitia lugha ya kiarabu na lugha 12 za kigeni kukabiliana – kimawazo – siasa kali na ugaidi kwa kueneza elimu sahihi duniani hapa na huko, na kuchunguza na kujibu yote yanayotolewa na makundi ya kigaidi kwa kutumia hoja na dalili wazi zinazobatilisha fikra na itikadi za makundi hayo, mbali na kutolea machabisho mengi kuhusu masuala makuu yanayotumiwa vibaya na wenye siasa kali na wagaidi kama masuala: JIHAD, KHILAFA, UKAFIRISHAJI, n.k.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.