Hija ni wito wa Kuimarisha Mshikamano na Umoja wa Waislamu

  • | Thursday, 30 July, 2020
Hija ni wito wa Kuimarisha Mshikamano na Umoja wa Waislamu

     Hapana shaka kwamba lengo la kwanza la Hija ni kuzidisha kumuelekeza mja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumfanya kuwa mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, na kuimarisha uhusiano kwake na kuiingiza kwa ndani zaidi imani katika moyo wake, na kuithibitisha itikadi ndani ya dhamiri yake juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu.

Zaidi ya hayo, Hija inalenga kukutana na kujuana na Waislamu wengineo kutoka pande mbali mbali za dunia, kutambua hali zao, kuunganisha mawasiliano na kushirikiana nao kwa kheri.

Ibada ya Hija ni nafasi nzuri sana kwa Waislamu kuleta maelewano baina yao, kuimarisha udugu wa kidini na kieneo, kuweka pembeni hitilafu zao ndogodongo na kuungana mkono katika kurejeshea heshima na utukufu wa umma mzima wa Kiislamu.

Kwa hivyo, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kinaona kwamba ni lazima kutumia vyema ibada ya hija kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu na kudhihirisha nguvu ya umma wa Kiislamu. Umoja na mshikamano wa nchi za kiislamu ni miongoni mwa njia bora za kukabiliana na mashambulizi yanayofanywa na nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu, au wale wagaidi wanaojinasibisha Uislamu kwa uongo, kwani maslahi ya umma wa Kiislamu imo katika kuimarisha umoja na mshikamano baina yao na kuwa kitu kimoja katika kupambana na adui na ugaidi.

Vile vile, Kituo cha Al-Azhar kinasisitiza kwamba siku kumi za kwanza za mwezi wa mfunguo tatu (Dhul Hija) ni siku bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko zingine, na vitendo vya mauaji vinaharamishwa katika siku hizo takatifu, kwani mwezi wa Dhul Hija ni miongoni mwa miezi minne mitakatifu ambayo inaharamishwa mauaji humo. Kwa hivyo, makundi ya kigaidi yanayodai kusimamisha shari'a ya Allah ardhini, tunasema kwayo: je! hayakujua kwamba shari'a ya Allah inaharamisha kuwaua watu wasio hatia katika miezi minne mitakatifu? Naam yanajua! Lakini yanasema yasiyoyatenda, nayo ni chukizo kubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mtu anasema asiyeyatenda.   

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.