Imam Mkuu akutana na timu «Enactus Al-Azhar» akisifu uwakilishi wao wa heshima kwa Misri

  • | Wednesday, 16 September, 2020
Imam Mkuu akutana na timu «Enactus Al-Azhar» akisifu uwakilishi wao wa heshima kwa Misri

     Imam Mkuu amesema kwamba "Enactus wa Al-Azhar": ni mfano wa heshima kwa mwanafunzi wa Al-Azhar, ambaye ana faida kwa nchi na ubinadamu wake ----------
Imam Mkuu, Profesa Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, amepokea leo katika Mashyakhat Al-Azhar timu ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar iliyowakilisha Misri na iliyoshinda kwa nafasi ya kwanza ulimwenguni katika mashindano ya "Enactus" ya ujasirimali na miradi ya kijamii, Imamu Mkuu aliwapongeza vijana wa Al-Azhar akielezea fahari yake kwa mifano hii ya heshima ya wanafunzi wa Al-Azhar kuhusu kuwakilisha kwa heshima nchi yao katika mikusanyiko ya kimataifa, akisisitiza juu ya vijana kuendelea katika kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya nchi, na kwamba timu hii itakuwa kama kichocheo na motisha kwa wanafunzi wengine kustawi na kuingia katika ulimwengu wa ujasiriamali.
Fatima Sarri mkurugenzi mtendaji wa "Enactus wa Misri" alisema kuwa wanafunzi wa Al-Azhar wamethibitisha umahiri wa mwanafunzi huyo wa Al-Azhar ndani na nje ya Misri, na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa timu inayoshiriki kwa mara ya kwanza na kushinda tuzo hiyo, na kwamba hii ilikuwa matunda ya juhudi kubwa na ushirikiano kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu, viongozi wa vyuo vikuu na wafanyabiashara, na uteuzi wa timu ya Al-Azhar ulikuja kupitia kufuzu kadhaa kwa wenyeji kati ya vyuo vikuu 58, kisha kufuzu kwa kimataifa kutoka nchi 36.
Mkurugenzi Mtendaji wa Enactus wa Misri alisisitiza kuwa miradi iliyoundwa na iliyotekelezwa na vijana ni endelevu na yenye manufaa kwa watu na nchi.
Wanafunzi wa Al-Azhar ambao walishinda Kombe la Dunia katika ujasiriamali walionyesha furaha yao kubwa ya kukutana na Imamu Mkuu na msaada wake kwao katika vipindi vyote vya mashindano, na kwamba kupongeza Imamu Mkuu kwenye ukurasa wake rasmi wa media ya kijamii na mkutano wake wa haraka nao leo unazingatiwa heshima na kichocheo kubwa kilichowafanya wawe na hamu ya kuendelea Kwa bidii na uvumbuzi, na kwamba hii inathibitisha hamu ya Imamu Mkuu kusaidia wanafunzi wa Al-Azhar kwa njia zote, na kuwahamasisha kupata maarifa na kuitumia katika uvumbuzi, na huduma ya dini, nchi na ubinadamu, na kwamba mafanikio hayo yanathibitisha umahiri wa wanafunzi wa Al-Azhar ambao walishinda timu kutoka Canada, Amerika, Ujerumani, Uchina na nchi nyingi ambazo zina timu 32 zinazowakilisha vyuo vikuu maarufu vya kimataifa.
Wanafunzi walisisitiza kuwa wazo la mradi huo lilitoka kati ya mawazo 70 ambayo waliyatafiti na waliyachunguza kwa uangalifu, na wakagundua kuwa Ziwa Qarun inakabiliwa na uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya kutupa ganda la shrimp, na kijiji hakinufaiki na maganda hayo ambayo yalikuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira, na leo imekuwa chanzo cha mapato, na kwamba wavuvi wanatumia boti zaidi ya 1500 walilazimika kuacha kazi zao hapo na kutafuta kazi nyingine katika mikoa mengine kwa sababu ya ukosefu wa samaki ambao vimelea huua, kwa hivyo mradi huu ulikuja kuwahudumia watu wa eneo la ziwa wa Qarun, kuondoa hali ya kuacha shule, kuunda fursa mpya za kazi na kuinua kiwango cha maisha kwa watu. 
Mradi wa timu ya "Enactus Al-Azhar", ambao ulitekelezwa na zaidi ya wanafunzi 100 wa Al-Azhar unakusudia kutafuta njia mpya za kubadilisha maganda yasiyotumika katika kijiji cha Shakshouk katika mkoa wa Fayoum ili kutoa bidhaa tano za msingi (viungo, mbolea za kikaboni, losheni, mashamba ya shrimp, vichujio vya kikaboni) pamoja na kusafisha ziwa, timu iliweza kuwezesha zaidi ya wanawake 800 katika kijiji kupata kazi za kudumu kwa familia zao baada ya shughuli kadhaa za utafiti na maendeleo, na mradi pia uliweza kupunguza kiwango cha ukosefu wa kazi katika kijiji, kuongeza mapato kwa familia kwa 320%, na kupunguza kiwango cha walioacha shule ambao ni zaidi ya 1,300 mwanafunzi katika viwango tofauti vya elimu.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.