kituo_cha_uangalizi_cha_Al_Azhar katika siku_ya_kimataifa_ya_amani: amani ni asili katika kuamiliana na mwavuli kwa watu wote

  • | Monday, 21 September, 2020
kituo_cha_uangalizi_cha_Al_Azhar katika siku_ya_kimataifa_ya_amani: amani ni asili katika kuamiliana na mwavuli kwa watu wote

    Kila mwaka mnamo tarehe 21 mwezi wa Septemba, ulimwengu unaadhimisha "siku ya kimataifa ya amani," iliyopitishwa na jumuiya kuu ya umoja wa mataifa mnamo 1981; ili kusherehekea na kuimarisha maadili ya amani kati ya mataifa na watu wote.
Na kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinasisitiza kuwa aya za Qur'ani Tukufu zinasisitiza kwamba amani na mazungumzo ni misingi ya kuamiliana na wengine, na sio vita na ugomvi, kikionyesha kwamba neno la "amani" limetajwa katika Qurani kwa umbo lake tofauti mara 140, wakati neno la "vita" limetajwa kwa umbo lake tofauti mara 6 tu.
Pia kituo kinasisitiza kuwa kufanya kazi kwa ajili ya kuhakikisha amani ni dharura ya kibinadamu, Kwa sababu ni lengo linalotakiwa na wanadamu wote - hakuna tofauti kati ya Waislamu na wafuasi wengine wa dini zingine – basi wote ni sawa kuelekea amani, na washirika katika kuweka misingi yake na kuilinda, na kuondoa vizuizi vinavyoizuia, kikielezea kuwa amani ni mwavuli unaolinda wanadamu wote kutokana na mizozo na vita, na huwaepuka migogoro.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.