Papa Francis: Sheikh wa Al-Azhar alikuwa chanzo cha msukumo katika kuandika ujumbe mpya wa kipapa

  • | Tuesday, 13 October, 2020
Papa Francis: Sheikh wa Al-Azhar alikuwa chanzo cha msukumo katika kuandika ujumbe mpya wa kipapa

     Papa Francis, Papa wa Kanisa la Kikatoliki, alisema kuwa Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa/ Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, alikuwa msukumo katika kuandika ujumbe mpya wa kipapa "Sisi sote ni wadugu".

Baba Francis alibainisha kuwa Imamu mkuu ndiye aliyemhimiza kuandika barua hiyo, alipokutana naye huko "Abu Dhabi" kwa ajili ya kusaini "hati ya Udugu wa kibinadamu", ili wasisitiziane kwamba dini hazikuwa kamwe kituo cha vita au chanzo cha hisia za chuki.
Imamu mkuu alikuwa ameandika chapisho katika ukurasa wake wa Facebook ambapo alisisitiza kwamba ujumbe huu wa kipapa "unakuja kama ukamilisho wa hati ya udugu wa kibinadamu, ikifunua ukweli wa ulimwengu unao na kasoro katika misimamo na maamuzi yake. Ujumbe huo unawazungumza walio na matakwa mema na dhamiri hai, na unaurejesha ufahamu kwa wanadamu”.

Kwa upande wake, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinazingatia matamshi ya Baba Francis ni yenye athari kubwa katika historia ya mazungumzo kati ya mashariki na magharibi kwa ujumla, na kati ya Uislamu na Ukristo hasa, kikielezea kwamba hiyo ilitokana na juhudi za Imamu na Papa kuhusu kuimarisha misingi ya udugu wa kibinadamu, ambayo hati yake ilisainiwa mnamo Februari mwaka jana 
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.