Katika hotuba yake mbele ya mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani, uliofanyika mjini mkuu wa Italia, Roma...

  • | Sunday, 25 October, 2020
Katika hotuba yake mbele ya mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani, uliofanyika mjini mkuu wa Italia, Roma...

Katika hotuba yake mbele ya mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani, uliofanyika mjini mkuu wa Italia, Roma.

Imamu Mkuu Sheikh wa Al_Azhar:
Kuutusi dini na vitakatifu vyake kwa madai ya "uhuru wa kujieleza" ni kiwango kisicho sawa na wito wazi kwa chuki.

Mheshimiwa Imamu mkuu, Profesa Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar, amesisitiza kwamba ulimwengu unaishi ndoto mbaya kutokana na janga la virusi vya Corona, ambayo hakuna wananchi au nchi moja iliyookolewa kutoka kwake, akiongeza kwama kilichoongeza hali mbaya wa kisasa chungu ni kuona mamilioni ya wakimbizi hawa katika maeneo ya migogoro, na hali zao zimekuwa mbaya zaidi katika wakati wa kukosekana kwa huduma za kiafya zinazohitajika.

Mheshimiwa imamu mkuu, alisema katika hotuba yake mbele ya mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani mjini mkuu wa Italia Roma, ambayo aliisema badala yake mshauri Mohamed Abdel Salam, katibu mkuu wa kamati kuu ya udugu wa kibinadamu, kwamba licha ya hatari hizo zote zilizosababishwa na virusi vya Corona, kuna janga jingine la zamani na linaendelea, ambalo tulikuwa tunadhani kuwa itamalizwa mbele ya hatari ya janga linalotishia wanadamu wote, nalo ni janga la ubaguzi, na ugonjwa wa dhamiri ya kibinadamu, mpaka tuliposikia wito wa kuwacha baadhi ya watu wanangojea hatima yao kwa ajili ya kuwapa watu wengine nafasi ya kupata matibabu kwanza, nazo ni wito zisizomaanisha isipokuwa kutokuwepo ubinadamu kuhusu wanaozisema.

Mheshimiwa amebainisha kwamba kuyapona magonjwa ya chuki na ubaguzi wa kibinadamu yapo katika dawa iliyotolewa kutoka majaribio machungu yetu, nayo ni dawa ya udugu wa kibinadamu ambayo ni kinga thabiti mbele ya ugonjwa wa kifikra na kimaadili, akiashiria kwamba dhana ya udugu wa kibinadamu haimaanishi kutosha kwa kukubali mwingine tu, bali inamaanisha kutoa juhudi zaidi kwa ajili ya usalama wake, na kukataa ubaguzi kwa sababu ya tofauti ya aina yoyote, na tusiepushe kutoa juhudi yoyote kuhusu kueneza misingi hiyo juu kati ya watu.

Na sheikh wa Al-Azhar amesisitiza kwamba mfumo mpya wa ulimwengu umekuza kwa dhana ya utandawazi, na umetuhubiri kwamba utabeba kwa ulimwengu wote maadili mazuri ya kibinadamu kama uhuru, uadilifu na usawa, lakini kwa haraka imetubainika kwetu kwamba madai hayo yametumiwa kwa njia isiyo ya kibinadamu kuhusu kumweka mbali anayehitilafiana nao, na kufaradhisha mfano moja wa kiustaarabu na kumaliza vitambulisho, na kudai haki kuhusu kuwahukumu watu, na kudai kuwa kuna mfano mmoja wa kitamaduni unaofaa kwa ubinadamu, na kwamba mifano mingine imekuwa kumbukumbu ya kihistoria, na utandawazi hivi karibuni ulianguka katika unafiki na upingaji kati ya kile unachosema kwa watu na kile unachofanya nao. Hakika tuliona maadili yanaporomoka wakati ulimwengu ulipopuuza nchi kamili ambayo wananchi wake wameacha makazi yao, na wanakabiliwa na mauaji na kufa kwa sababu ya njaa, na ushahidi ulio karibu kabisa ni Rohingya, walioachiwa peke yao wakisubiri hatima yao kwa kufa kwa sababu ya kuzama au kufa kwa sababu ya njaa baharini, akiongeza kuwa Corona vilikuja kutangazia kwa ulimwengu kifo cha utandawazi ambacho uliogawanya ulimwengu na uliotenganisha baina ya watu, na kuweka mbali maadili, tabia na dini, na kwamba sasa hivi ni wakati wetu kwa ajili ya kukubali utandawazi mpya unaojengwa juu ya udugu wa kibinadamu, na kuimarisha kuishiana pamoja katika jamii, na kusimamisha mbio ya kununua silaha na kuelekeza mabilioni yanayotumiwa katika silaha na vita kwa elimu, huduma za kiafya na utafiti wa kisayansi, na wakati huo -tu- tutaweza kukabiliana na majanga na magonjwa, na tutakuwa na nguvu zaidi katika migogoro yoyote.

Sheikh wa Al-Azhar alitangaza akizungumzia kuhusu mauaji ya Paris, kwamba yeye anajiepusha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akaziepusha hukumu za dini ya kiislamu, na mafundisho ya Nabii wa Rehema, "Muhammad"(S.A.W), kutoka mtu yeyote anayefuata fikra kali, akisisitiza kwamba kuutusi kwa dini na vitakatifu vyao kwa madai ya "uhuru wa kujieleza" ni kiwango kisicho sawa na wito wazi kwa chuki, basi mtu huyo na walio kama yeye ni mbali sana na Uislamu, aidha mgaidi wa New Zealand aliyewaua waislamu msikitini ni mbali sana na dini ya Yesu (A.S).

Mkutano wa kimataifa wa kuombea kwa ajili ya amani kati ya dini kuu katika ulimwengu chini ya anuani: "Hakuna anayeisha kwa usalama peke yake - amani na udugu" ulifanyika kwa mwaliko wa Jumuiya ya Sant' Egidio katika mji mkuu wa Italia, Roma, na kwa kuhudhuria Baba Francis, Papa wa Kanisa la kikatholiki, na bwana Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Italia, na Ursula Von der Leyen, Rais wa kamishna ya kiulaya, na Andrea Ricardi, mwanzilishi wa Jumuiya ya Sant'Egidio, na idadi ya viongozi kadhaa wa kidini ulimwenguni.
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.