Al-Azhar Al-Sharif yalaani mashambulizi ya kigaidi ya Vienna

  • | Wednesday, 4 November, 2020
Al-Azhar Al-Sharif yalaani mashambulizi ya kigaidi ya Vienna

     Al-Azhar Al-Sharif na Mheshimiwa Imamu mkuu wake Profesa/ Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar, analaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea  katika masaa yaliyopita katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Austrian Vienna.
Na Al-Azhar inasisitiza kuwa kumwua mtu mmoja ni kama kuwauwa ubinadamu wote, na kwamba haki ya mwanadamu katika uhai ni lengo lililo juu kabisa katika sheria na kanuni zote, akitakia taasisi zote za kimataifa kusimama safu moja mbele ya ugaidi, na watu wote waonyeshe mshikamano kwa ajili ya kueneza amani ulimwenguni na kukataa ukali na uchuki.
Na Imamu Mkuu anatoa salamu za rambirambi yake kwa raisi na wananchi wa Austrian, akimwomba Mwenyezi Mungu kuwapona haraka majeruhi, na kuokoa ulimwengu kutoka hatari ya ugaidi na shari yake, na kwamba watu wote wapate neema ya usalama, amani na utulivu.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.