Katika siku ya kimataifa ya mtoto Kituo cha Al Azhar: ulindaji wa watoto ni lazima uwe lengo kuu kwa jamii zote

  • | Wednesday, 25 November, 2020
Katika siku ya kimataifa ya mtoto Kituo cha Al Azhar: ulindaji wa watoto ni lazima uwe lengo kuu kwa jamii zote

Ulimwengu wote hushereheka katika siku ya 20 mwezi wa Novemba kila mwaka kwa siku ya kimataifa ya mtoto, nayo inaafikiana na tarehe ya kutia saini juu ya makubaliano ya kimataifa ya haki za mtoto mwaka wa 1989, na kusherehekea kwa siku hiyo kumeanza katika mwaka wa 1990 kwa ajili ya kuimarisha ufungamano wa kimataifa na kuongeza uelewa kati ya watoto wa ulimwengu, na kuleta ustawi kwao.
Kituo cha Al-Azhar kinasisitiza kuwa kuwavuta watoto, kuwalazimisha kujiunga, kupotosha mawazo yao na kubadilisha fika zao ni moja wapo ya mambo muhimu zaidi kwa makundi ya kigaidi yenye fikra kali, kwani inazingatia ndio dhamana ya kuendelea fikra kali, kizazi baada ya kizazi, kwa hivyo makundi ya kigaidi yanategemea watoto kama moja ya mikakati yao.
Mnamo mwaka wa 2018, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusiwa kwa dawa za kulevya na uhalifu ilichapisha ripoti muhimu ikisisitiza kuwa kundi la "Boko Haram" lililazimisha kujiunga watoto 8,000 nchini mwa Nigeria tangu 2009, na kuwalazimisha watoto wengine kushambulia familia zao kwa ajili ya kuthibitisha utii wao kwa kundi hilo, na kwamba kundi hilo lilitumia wavulana na wasichana kama ngao za kibinadamu katika mashambulizi yake ya kigaidi. Ripoti hiyo pia ilisisitiza kuwa watoto wanalazimishwa kujiunga na kundi la Al-Shabab la Somalia, na kundi la Al-Tawhiid wa Al-Jihad katika Afrika ya Magharibi, na kundi la Ansar Al-Din, na kundi la Al-Qaeda nchini mwa Mali na nchi za jirani, na kundi la Abu Sayyaf nchini mwa Ufilipino na makundi mengine. Ama kundi la kigaidi la ISIS, basi linazingatiwa kama kundi la kigaidi linalowatumia watoto zaidi, na linatoa juhudi kubwa ya kuwatumia na kuwazoea kutekeleza operesheni za kigaidi, na kuwatumia kwa ajili ya kuwasaidia wanamgambo wake kwa sababu ya kupoteza wanamgambo wengi, na kwa hivyo linashughulika kwa kulima fikra kali katika tangu utoto.
Kwa sababu hiyo, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinasisitiza kuwa kuwalinda watoto kutoka kwa makundi ya kigaidi inapaswa kuwa lengo kwa jamii zote kupitia kukuza uelewa kupitia familia, mitaala ya kielimu, programu za televisheni, na filamu ya katuni na sanaa zote zinazowafaa watoto.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.