Siku ya kimataifa ya kumaliza vurugu dhidi ya mwanamke.

  • | Saturday, 28 November, 2020
Siku ya kimataifa ya kumaliza vurugu dhidi ya mwanamke.

     Uislamu ulimheshimu mwanamke hata akiwa, mtoto, mke na mama, na ukahimiza Kumtendea kwa wema, na kuishi naye kwa uzuri, kumtunza Mtume (S.A.W) Alisema: "Wausieni wanawake mambo ya kheri" (ilisimuliwa na Masheikh wawili).
Hakika Uislamu umetaka kuwatendea wanawake kwa ulaini, upole na uzuri, na kutomtendea kwa nguvu kwa maneno au matendo. Iliripotiwa kuwa, hakika imesimulia kwamba Mtume (S.A.W) alikuwa safarini, na alikuwa na mvulana mweusi anaitwa Angasha anaendesha ngamia ambao wanapanda wanawake, na ngamia walikuwa wanatembea kwa haraka, na anatetemeka sana, basi Mtume (S.A.W) amesema: "ewe Angasha, endesha ngamia kwa upole na angalia glasi (wanawake). (ilisimuliwa Al-Bukhari).
Na Uislamu umeonya kwamba watu wazuri ni ambao kheri yao inakuwa kwa wanawake wao; na imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurayrah, kwamba Mtume (S.A.W) Alisema: "Waumini wanao na imani kamili, ni wale wanao na tabia njema, na wazuri wao ni wanaowatendea pamoja na wanawake wao kwa uzuri" (Imesimuliwa na Ahmad). Na imesimuliwa na Bibi Aisha kwamba Amesema, Mtume (S.A.W) amesema Walio bora miongoni mwenu ni wale walio bora kwa wake zao, na Mimi ni mbora kwenu kwa wake zangu.”
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.