"Maulama Wakuu wa Al-Azhar": kwa mujibu wa Sheria ni wajibu kulazimika na kufuata hatua za kujikinga zilizowekwa na mamlaka yanayohusika na wanaharimisha kutozifuata...

  • | Tuesday, 29 December, 2020
"Maulama Wakuu wa Al-Azhar": kwa mujibu wa Sheria ni wajibu kulazimika na kufuata hatua za kujikinga zilizowekwa na mamlaka yanayohusika na wanaharimisha kutozifuata...

     "Maulama Wakuu wa Al-Azhar": kwa mujibu wa Sheria ni wajibu kulazimika na kufuata hatua za kujikinga zilizowekwa na mamlaka yanayohusika na wanaharimisha kutozifuata. "Maulama Wakuu wa Al-Azhar": Nafasi kati ya Wanaosali katika makusanyiko na wakati wa kusikiliza hotuba ya Ijumaa haiathiri usahihi wa Sala "Maulama Wakuu wa Al-Azhar": Dutu za kileo zilizoandaliwa kwa ajili ya usafishaji na kuondoa uchafu ni zenye twahara na matumizi yake ni halali, bali ni wajibu katika hali kama hizo. "Maulama Wakuu wa Al-Azhar": Kuepuka mkusanyiko wa harusi au kutoa rambirambi... na kupongeza au kutoa rambirambi kupitia simu au mitandao ya kijamii kunakubalika kisheria. Taarifa ya baraza kuu la #Maulama_wa_Al_Azhar kwa taifa la Kiislamu kuhusu hatua za kujikinga dhidi ya virusi vya Corona Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, sala na amani ziwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.. na baadaye,, - Kwa kuzingatia mfululizo wa ripoti zinazoonyesha ukuaji wa haraka na kuenea kwa virusi vya Corona (Covid 19), na kwa kuongezeka kwa kile kinachoitwa wimbi la pili, ambayo ripoti zinaonyesha kuwa hatari halisi ya virusi ni katika kuenea kwake kwa haraka, athari yake kali, na pengine, mtu aliyeambukizwa hahisi ugonjwa na hajui kumwambukizwa lakini anaeneza maambukizo katika kila mahali anapohamia, na kwa sababu kuwa mojawapo wa malengo makuu ya Sharia ya Kiislamu ni kuhifadhi roho na nafsi, Baraza kuu la Maulama wa Al-Azhar Al-Sharif -kulingana na jukumu lake- linasisitiza kwamba ni lazima kwa mujibu wa Sheria kufuata taratibu na hatua za kujikinga zilizowekwa na mamlaka yanayohusika, miongoni mwa hatua hizo ni: (1) Kuvaa vinyago ambavyo hupunguza uwezekano wa kuambukizwa na virusi hivi hatari, na kulazimikia hayo ni wajibu wa kisheria katika harakati zote za wanadamu au katika kuwasiliana na wengine, na hii ni lazima kabisa katika Sala ya Jamaa ili anayesali asifanye dhambi ya kuhalifu, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: "wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo." (Al-Baqarah, Aya 195).. (2) Kuepuka salamu ya mkono -pia kukumbatiana na kumbusu kama jambo la kipaumbele- kulingana na kile kilichopendekezwa na mamlaka yanayohusika; Kama tahadhari dhidi ya kuambukizwa au Kueneza maambukizo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Hakuna madhara wala kudhuriana", kuepusha madhara ni wajibu, na kuchukua tahadhari katika kesi hii pia ni wajibu. (3) Kujiandaa nyumba au mahali pa kazi kwa ajili ya kusali sala za Jamaa au Ijumaa kabla ya kwenda misikitini ili kusali, kwa kutawadha au ghusl (kuosha); inazingatiwa kama mojawapo wa hatua muhimu za kujikinga ambazo hupunguza uwezekano wa kuenea kwa maambukizo, na kabla ya hayo, ni utii mkubwa, na kitendo ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amewauliza watu kukifanya ambapo anasema: "Mtu aliyejitakasa ndani ya nyumba yake, halafu ametembea kwenda nyumba ya Mwenyezi Mungu ili kutekeleza faradhi ya Mwenyezi Mungu, mojawapo wa hatua yake itashuka dhambi, na nyingine huinua daraja". Imesimuliwa na Muslim. (4) Kuweka umbali baina ya wanaosali katika sala ya jamaa na wakati wa kusikilizia hotuba ya Ijumaa, na hiyo haiathiri katika usahihi wa sala au thawabu ya jamaa; kwani hiyo ni hatua lazima ya kukinga kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa janga hilo, pamoja na ulazima wa kusawazisha safu wanaoswali pamoja na kuwepo umbali baina yao. (5) Kumtengana au kujitenga kwa anayepata virusi hivyo, au athari za virusi zilidhihiri katika afya yake, au wanaoshukiwa kuambukizwa na virusi Hivyo, na hiyo inakuwa katika hospitali za kutengwa au nyumbani; kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa na kutowadhuru wengine. (6) Epuka wale wanao na ugonjwa sugu au ugonjwa ya kinga, na wazee au wale wenye ugonjwa wa joto kali, au kikohozi, kupumua kwa pumzi, na kutowepo katika maeneo yenye watu wengi na mikutano iliyofungwa kwa sababu yoyote kufuatia kilichopendekezwa na taasisi husika, pamoja na kuwapa idhini ya kusali sala za Ijumaa na wa kawaida nyumbani. (7) Kuua vijidudu katika sehemu zote za mikusanyiko ambayo wagonjwa wanaoshukiwa kupita kutoka kwake, aidha lazima kuua vijidudu kwa kileo misikitini kabla na baada ya sala, na ni lazima kutumia Alkoholi kwa lengo kusafisha ni yenye ni halali na inaruhusiwa kutumiwa, bali ni wajibu katika hali hiyo. (8) Kusisitiza kwamba kusali sala za Sunna nyumbani ni bora kuliko kuzisali msikitini- na hiyo ni wajibu wakati wa janga- katika Sahih Al-Bukhari, Mtume (S.A.W) alisema: "enyi watu salini nyumbani mwenu, kwani sala iliyo bora zaidi ni sala ya mtu nyumbani mwake, isipokuwa sala za faradhi." Imetolewa na Al-Bukhari. (9) Epuka kukutana katika sherehe za harusi, au salamu za rambirambi, na kupongeza au kutoa salamu za rambirambi kwenye simu au kupitia mitandao ya kijamii; kwa sheria imesema kamba maslahi ya umma inawekwa mbali na maslahi ya mtu au familia, na anayefanya hivyo kupitia simu atapata thawabu kamili. - kwa ujumla watu wanapaswa kufahamu hali ambayo ulimwengu unapita sasa hivi, kwa kuzingatia maagizo yaliyotolewa na taasisi zinazohusika; kufuatia kauli ya Mwenyezi Mungu: (enyi mnaoamini, mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi) [An-Nisa: 59]. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailinde nchi na watu wake, na aifanye nchi yetu iwe salama na ya kutuliza na nchi zote, na kumaliza balaa na janga kwa nchi na watu. - Na sala za Mungu na salamu zimfikie bwana wetu Mtume Muhammad na familia yake, na sifa njema ni kwa Mungu, Mola wa walimwengu wote. #Kituo_cha_uangalizi_cha_Alazhar

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.