Usamehevu ni msingi wa kutatua shida nyingi za vurugu na msimamo mkali

  • | Wednesday, 27 January, 2021
Usamehevu ni msingi wa kutatua shida nyingi za vurugu na msimamo mkali

     Hakika, jamii hivi sasa zinakabiliwa na magonjwa mingi ya kijamii na ya kimaadili yanayowakilishwa katika kuenea kwa vurugu na ukatili. Jambo hili linarejea kwa kuacha misingi ya Uislamu ambayo inalazima kuwepo rehema, usamahehevu kama kanuni ya juu  inayotawala  baina ya wanadamu wote.
Kwa hiyo, kanuni ya usamehevu ni anwani ya nguvu katika Uislamu. Na maana hii ni moja ya maana ya imani, ambapo Uislamu umebadilisha uelewa (ufahamu) wa Waarabu kuhusu nguvu, kwani walikuwa wakidhani kuwa nguvu ni katika kulipiza kisasi na ushindi.
Basi, miongoni mwa sifa muhimu zaidi za tabia njema ni usamehevu, kwani ni sifa kubwa ya Mwenyezi Mungu, kwani yeye ni Msamehevu Mtukufu. Na Qurani Tukufu inasisitiza mara kwa mara juu ya usamehevu na kuepuka vurugu na sababu zake, na kukataa ugomvi unaosababisha machafuko na uharibifu.
Bali, jambo la nzuri zaidi ni kwamba Uislamu umeamrishia ihsani kwa wasio waislamu ambao hawakufanya adha dhidi ya waislamu wala hawapigani nao kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu), bali zaidi ya hapo, umeamrisha kuwasiliana na kuwalipa mali kwao.
Pia, Uislamu umewajibikia waislamu wafanye usamehevu na wasio waislamu. Na kaw hakika, Uislamu ulifikia kilele cha usamehevu, wakati iliamrisha kwa msamaha, hata katika eneo la imani, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema: (Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri) AN NAH'L:125,126.
Na bila shaka yoyote, kwamba matunda ya usamehevu ni kuenea kwa upendo kati ya watu wote, kwa sababu usamehevu unafungua mioyo na kuepuka ukatili na ukali baina ya wanadamu wote. Bali, lengo juu la ujumbe wa Mrtume Muhammad ni rehema na usamehevu, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema: (Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote) Al – Anbiyaa 107.
Kwa hivyo, Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali, kinabainisha daima kuwa tabia njema na usamehevu baina ya jamii zote, inapaswa kupatikana katika hali na nyakati zote.
Hakika, Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinaona kwamba uhusiano wa Waislamu na jamii zingine ni uhusiano wa kibinadamu unaotegemea hamu ya maisha bora na amani kamili kati ya watu wote, kuondoa wasiwasi, machafuko, na mzozo wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.