Kwa lugha 12... kituo cha uangalizi cha Al-Azhar chazungumzia jambo la kuzishambulia nyumba za ibada katika video mpya

  • | Monday, 7 June, 2021
Kwa lugha 12... kituo cha uangalizi cha Al-Azhar chazungumzia jambo la kuzishambulia nyumba za ibada katika video mpya

     Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kilitoa video 12 kwa lugha zake tofauti, ambazo zilikuwa kuhusu jambo la kuzishambulia nyumba za ibada na kulichambua kupitia kubainisha hatari yake kwa uhuru wa binadamu, na haki yake ya kumwabudu Mwenyezi Mungu.
Kituo cha uangalizi hapo awali kimetoa tafiti nyingi na ripoti kuhusu mashambulio hayo yasiyo ya kibinadamu ambayo yanatishia amani na usalama wa jamii na kuzua ugomvi ndani yao. Kituo cha uangalizi kitatoa karibuni kitabu cha"kuzishambulia nyumba za ibada" katika Maonyesho ya Vitabu ya Kimataifa ya Cairo, ambacho kinazungumzia jambo hili kwa kufuatilia na kuchambua kupitia kubainisha hatari yake juu ya jamii.
Kituo cha uangalizi kinasisitiza kwamba matoleo yake yanabainisha msimamo wazi wa Al-Azhar ambao unakataa uhalifu huo unaopingana na kile kilichokuja katika waraka wa "udugu wa kibinadamu", ambao ulihimiza umuhimu wa kulinda nyumba zote za ibada, na umezingatia kwamba kuzilenga ni kuacha wazi kwa ujumbe wa dini zote na maadili ya kibinadamu, na ukiukaji wazi kwa makubaliano na kanuni za kimataifa.