kimetangulizwa na Mheshimiwa Imamu Al Tayyib na Baba Mtakatifu Francis...

  • | Sunday, 4 July, 2021
kimetangulizwa na Mheshimiwa Imamu Al Tayyib na Baba Mtakatifu Francis...

     kimetangulizwa na Mheshimiwa Imamu Al Tayyib na Baba Mtakatifu Francis, na viongozi kadhaa na wahusika wakuu wa kimataifa wa kisiasa na kitamaduni walitoa maoni yao.
kimetangulizwa na Mheshimiwa #Imamu_Al_Tayyib na Baba Mtakatifu Francis, na viongozi kadhaa na wahusika wakuu wa kimataifa wa kisiasa na kitamaduni walitoa maoni yao.
"Imamu na Papa na Njia ngumu" ... kitabu kinachosimulia historia ya #Hati_ya_Udugu_wa_kibinadamu ... katika mabawa mawili ya Al-Azhar na wahenga wa waislamu kwenye maonyesho ya kitabu.
Mabawa mawili ya Al-Azhar Al-Sharif na Baraza la Wahenga wa waislamu katika Maonyesho ya Cairo ya Kimataifa ya kitabu yanatanguliza kwa wageni wao kitabu "Imam na Papa na Njia Ngumu. hishtoria ya Kuzaliwa kwa Hati ya Udugu wa kibinadamu,” kilichoandikwa na Jaji Mohamed Abdel Salam, Katibu Mkuu wa Kamati ya Juu ya Udugu wa kibinadamu, na mshauri wa zamani wa Imam Mkuu, Profesa/ Ahmad Al-Tayyib Sheikh wa Al-Azhar.
Kitabu hicho kinazungumzia vipindi vilivyopitiwa na #Hati_ya_Udugu wa kibinadamu, hadi kutiwa saini mnamo Februari mwaka wa 2019 huko Abu Dhabi. Mwandishi anasimulia hatua zilizochukuliwa haraka na Imamu Mkuu, profesa/ Ahmad Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar Al -Sharif, na Papa Francis, Papa wa Kanisa la kikatoliki, kuelekea kueneza amani ulimwenguni, zilizoanza kwa ziara ya Imam Al-Tayyib kwa Vatican, kisha ziara ya Baba Mtakatifu Francis kwa Al-Azhar Al-Sharif, baada ya hapo uhusiano wa kiudugu kati ya Imamu na papa  ulipata maendeleo, na mikutano iliendelea.
Katika utangulizi wa kitabu chake, mwandishi anataja sababu za kuandika kitabu hicho, akisema: "Nilifikiri sana kuhusu uwezekano wa kuchapisha ushuhuda wangu kuhusu hati ya udugu, baada ya kuonekana hadharani, na kukubaliwa na ulimwengu vizuri. Na nilisikia kwamba ulimwengu umekuwa kama kijiji changu. Kisha ilikuwa wajibu juu yangu kunukuu kwa watu kilichotokea. Kwa hivyo nilikuwa na bidii katika kurekodi kile kilichomo kumbukumbu, na licha ya kuwa mimi sio mmoja wa waandishi wenye ujuzi, na sina ujuzi katika sanaa ya uandishi. Lakini nilielezea maana kwa njia ambayo sio kama niliyotarajia hakika, lakini sio kila kitu ambacho mtu anataka kutambua, basi niliandika ushuhuda wangu, nasema: "Ushuhuda" na najua vizuri niliyeyasema kwani mimi ni jaji, kwani mshuhuda lazima kuwa asisemi ila haki, na havutiwi na matakwa, wala haelekei kwa utashi au woga”.
Kitabu hicho ni kama mtiririko wenye mantiki unaomsaidia msomaji kuelewa vipengele vya kisa, na uwezo wa kuishi maelezo ya safari hii. Ambapo mwandishi anazungumzia kuhusu mhusika wa Imamu Mkuu kama alivyomjua kwa ukaribu na kuzisifu pande mbalimbali za mtu huyo mtakatifu, na namna ya athari ya uundaji huo katika kujinga kiongozi anayependa amani, ambaye anaamini kuishi pamoja na mwingine.
Kitabu hicho kimebainisha neno la Imam Mkuu Ahmed Al-Tayyib Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif kuhusu kitabu hicho, kwa kusema: "Jaji aliandika vizuri kitabu chake, na alijitahidi katika kuandika kwake, na alitutolea kitabu hicho kinachokusanya vipendi vya kuandika "hati", ikifunua makusudio na siri kadhaa.
Mwandishi pia alinukuu ushuhuda wa Baba Mtakatifu Francis katika utangulizi wa kitabu chake, "Sikutarajia kwamba Jaji Muhammad Abd al-Salam atamaliza kitabu hicho haraka sana, na kitabu hiki kinakusanya wakati muhimu wa safari hii ambayo ilituchochea kutia saini "Hati juu ya Udugu wa kibinadamu" mnamo Februari mwaka wa 2019 huko "Abu Dhabi". Basi Mwana mpendwa, Muhammad Abd al-Salam, alikuwa mshuhuda wa macho kwa hatua zilizochukuliwa na changamoto na shida zilizokabiliwa ili Kufikia lengo hili. Hakuwa tu mshahuda, lakini alishiriki kwa hamu katika kazi hiyo. Jaji Muhammad Abd al-Salam alinionyesha mimi na kaka yangu Imam Ahmad Al-Tayyeb kwmba yeye anastahiki uaminifu aliompa”.
Kitabu hiki kinaelezea jinsi kuwasili kwa Baba Mtakatifu Francis akiwa mkuu wa Kanisa Katoliki ambapo ilirejesha matumaini kwa Imamu Mkuu kwa kurudishwa kwa uhusiano na taasisi kubwa zaidi ya dini ya Kikristo, ambapo watu walijua kwamba Baba Francis, anapenda amani, kwa hivyo uamuzi wa Imamu mkuu ulikuwa wa ujasiri kwa kutembelea Vatican, kama anavyoelezea vikwazo vilivyopitiwa kwa ajili ya kukamilisha ziara hiyo, haswa kwa kuzingatia hali ya kutojali ambayo ilikumba uhusiano wa Al-Azhar na Vatican kabla ya kipindi hicho cha Al-Tayyib na Francis..
Na Al-Azhar Al-Sharif inashiriki - kwa mwaka wa tano – katika Maonyesho ya Cairo ya kimataifa ya kitabu katika kufanyika kwake kwa mara ya 52, na hiyo kutokana na jukumu la Al-Azhar la kielimu na katika kueneza fikra za Kiislamu zilizo sawa ambazo imekubaliwa zaidi ya miaka elfu moja. Na upande wa Al-Azhar liko katika maonyesho katika Jumba la Urithi Namba ya 4, na linaenea kwa eneo la karibu mita elfu moja, na linajumuisha mahali kadhaa, kama eneo kwa semina, mahali kwa fatwa, na mahali kwa maandishi ya Kiarabu, na pia kona kwa watoto na maandishi.
 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.