Sheikhi wa Al Azhar ampongeza Rais Al Sisi na umma wa kiislamu kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Hijra

  • | Saturday, 7 August, 2021
Sheikhi wa Al Azhar ampongeza Rais Al Sisi na umma wa kiislamu kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Hijra

     Mheshimiwa Imam Mkuu Profesa/ Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al_Azhar Al-Sharif, anatoa pongezi kwa Raisi wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi, na waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Hijra, akimwomba Mwenyezi Mungu aufanye kuwa mwaka wa baraka, mafanikio, usalama na amani.
Na Al_Azhar inasisitiza kwamba uhamiaji mtukufu wa Mtume (S.A.W) ulikuwa na bado ni tukio muhimu sana katika historia ya kiislamu, sira ya Mtume wetu (S.A.W), na historia nzima ya wito wa kiislamu; Na iliimarisha kwenye waislamu njia ya kumfuata Mtume wetu (S.A.W) kuhusu nguvu ya imani yake kwa Mwenyezi Mungu, kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kubeba kwake mambo magumu kwa ajili ya Uislamu, na kutoa kwake mifano bora kuhusu kuishiana na wasio waislamu.
Na Al_Azhar inaashiria kwamba uhamiaji wa Mtume ulionesha thamani ya nchi katika Uislamu, na sifa ya Masahaba wote wa Mtume (S.A.W) na kujitolea kwao.
Na Al_Azhar inatoa wito kwa waislamu wote ulimwenguni kwa kutoa kilicho ghali kwa ajili ya kuinua dini, na kuwa na hamu ya kutafsiri sira ya Nabii wetu (S.A.W) na mafundisho yake kwa vitendo na tabia.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.