Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar chapokea ujumbe kutoka taasisi ya Shabab Al-Mutawaset kuzitambua juhudi za kupambana na fikra kali na ugaidi

  • | Monday, 30 August, 2021
Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar chapokea ujumbe kutoka taasisi ya Shabab Al-Mutawaset kuzitambua juhudi za kupambana na fikra kali na ugaidi

     Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar cha Kupambana na fikra kali kilipokea ujumbe kutoka taasisi ya Shabab Al-Mutawaset, leo, Jumapili, katika uwanja wa mradi unaosimamiwa na Wizara ya Vijana na Michezo; Kwa lengo la kutambua namna ya kazi ya Kituo cha uangalizi, vituo vyake, machapisho yake mashuhuri katika uwanja wa kupambana na fikra kali na ugaidi, na njia za kuwalinda vijana kutoka fikra kali.
Dr. Muhammad Al-Dhuwini, Makamu wa Imamu Mkuu wa Al Azhar Al-Sharif, alitoa hotuba ya kuwakaribisha kwa ujumbe huo, wakati ambapo alisisitiza jukumu lililofanywa na Al_Azhar Al_Sharif katika kupambana na fikra kali na ugaidi, kupitia timu maalum ya watafiti wanaofanya kazi katika kituo cha uangalizi cha la Al_Azhar, ambao hufuata matukio na kufuatilia shughuli za makundi ya kigaidi ulimwenguni kote, ili kuchambua na kuchanganua matukio mapya kila wakati.
Chini ya anuani "Cairo na Roma .. Miji ya mediterranean", Mshauri Mohamed Abdel Salam, Katibu Mkuu wa Kamati ya Juu ya Udugu wa Binadamu, alijadiliana na ujumbe wa taasisi hiyo kupitia mkutano wa video mada kadhaa zinazohusiana. Kwa lengo la kufungua upeo mpya ili kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya vijana katika nchi zote mbili, jambo litakalokuwa na faida kubwa katika juhudi za kupambana na fikra kali na kuwalinda vijana ili wasivutwe na fikra kali, ambayo jamii hazivuni chochote kutoka fikra kali hicho isipokuwa uharibifu.
Ni muhimu kukumbuka kuwa kuna ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali, ili kutekeleza mpango wa "Kuelekea Maono ya Vijana Kukabiliana na fikra kali na Ugaidi", ambapo wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu vya Misri walipokelewa ili kujua namna ya kazi ya kituo cha uangalizi, na juhudi za Al-Azhar katika uwanja wa kupambana na fikra kali, Kwa lengo la kuwaelimisha wanafunzi na kuwalinda kutoka fikra kali, kusahihisha mawazo yasiyosahihi, na kukanusha tuhuma zinazoenezwa na vikundi vya kigaidi, kupitia machapisho yao kwenye mtandao na tovuti za mitandao ya kijamii. Ziara hii ilitanguliwa na kuandaa shughuli kadhaa na Taasisi ya "Shabab Al-Mutawaset" chini ya anwani: "Mazungumzo kuhusu waraka wa Udugu wa Binadamu".
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.