Katika mkutano wake na Rais wa kifaransa kwenye Ikulu ya Elysee ...

  • | Wednesday, 25 May, 2016
Katika mkutano wake na Rais wa kifaransa kwenye Ikulu ya Elysee ...
 
Katika mkutano wake na Rais wa kifaransa kwenye Ikulu ya Elysee
Imamu Mkuu:
• Tunathamini roli ya Ufaransa katika kutetea suala la kipalastina…na kupambanua baina ya Uislamu kwa kuizingatia dini ya amani na kuiweka mbali na ugaidi.
• Damu za wanadamu katika Uislamu ni haramu kuvukwa sawa wao ni waislamu au wasio waislamu.
• Kupambana na ugaidi ni wajibu ya watu wote…sisi tuko tayari kuisaidia Ufaransa katika juhudi zake za kupambana na ugaidi na vurugu.
 
Rais wa Ufaransa:
• Tunaheshimu sana juhudi zako ewe mheshimiwa kupambana na ugaidi na misimamo mikali…na hotuba uliyoitoa leo ni msukumo mkubwa kueneza fikira za kuishi pamoja na amani.
• Al-Azhar ni taasisi yenye historia ndefu …tunashukuru utashi wako nguvu ili kueneza Uislamu ulio sahihi.
• Tunaheshimu sana msimamo wako wa kiutu ambayo mmeuelezea kwa ziara ya Alpataklan
 

Akikaribishwa sana kwa makaribisho makubwa kwa kiwango cha kirasimu na kitaifa …. Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib Sheikhi mkuu wa Al-Azhar, mkuu wa Baraza la wakuu wa waislamu alikutana siku ya Jumanne, na Rais wa Ufaransa; Francois Hollande kwenye Ikulu ya Elysee katika mji mkuu wa kifaransa, Paris.
Mheshimiwa Imamu mkuu alisisitiza katika mkutano huu kwamba uhusiano baina ya Misri na Ufaransa ni kale na imara katika nyanja mbali mbali, akibainisha kuwa Al-Azhar Al-Shareif inaheshimu misimamo ya Ufaransa katika kusaidia suala la kipalastina, vile vile inaheshimu misimamo ya rais wa kifaransa katika kupambanua baina ya Uislamu kwa kuizingatia dini ya amani na kuiweka mbali na ugaidi.
Pia, yule mheshimiwa alisisitiza kwamba damu za wanadamu na roho zao katika Uislamu ni haramu kuvukwa sawa kwa mnasaba wa waislamu au wasio waislamu, akisisitiza kuwa kupambana na ugaidi ni jukumu na wajibu ya watu wote, na kwamba Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuisaidia Ufaransa kama iwezakanavyo kwa ajili ya kupambana na ugaidi, akielezea shime yake kwa roli ya kifaransa na juhudi zake za kupambana na ugaidi.
  Imamu mkuu alielezea kuwa juhudi za kupigania vita mawazo makali zinahitaji kukwepo mtazamo wa kijumla kwa kushirikiana kwa wote, pamoja na kutambua umuhimu wa kuwazingatia vijana na kufanya juhudi zaidi kwa lengo la kuwatahadharisha wale vijana kutoka hatari za ugaidi na misimamo miklali.
Yule Mheshimiwa aliongeza kuwa Al-Azhar Al-Shareif ina hamu kubwa ya kuwasiliana kwa kudumu na tamaduni na staarabu zote kwa lengo kueneza uwastani, amani, kuishi pamoja na kukataa vurugu na ugaidi, akielezea kwamba Al-Azhar Al-Shareif ina kituo cha kiutamaduni cha kifaransa kwenye Chuo kikuu cha Al-Azhar kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi lugha ya Kifaransa kwa sababu ya kutekeleza utashi wa Al-Azhar kuwasiliana na utamaduni wa kifaransa na tamaduni nynginezo.
Kwa upande wake, Rais wa kifaransa Francois Hollande alimkaribisha sana Mheshimiwa imamu mkuu, akielezea heshima yake mkubwa na wanachama wa serikali yake na kushangaa kwao kwa juhudi alizozifanya Imamu mkuu kupigania vita ugaidi na kueneza uwastani, kusameheana na amani, akiongeza: tunatambua vyema utukufu wa Al-Azhar Al-Shareif, vile vile tunaheshimu sana matakwa nguvu ya shirika hilo kwa ajili ya kueneza dini sahihi.
     Vile vile, Hollande alitoa shukurani zake zote na wananchi wa kifaransa kwa ziara aliyoifanya imamu mkuu kwa ukumbi wa michezo ya kuigiza wa Alpataklan katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambapo mahali pa mashambulizi ya kigaidi yaliyotukia hapo mwezi Novemba uliopita yalisababisha maafa ya wahanga wengi, akisisitiza kwamba msimamo huo wa kiutu unathibitisha ushujaa na usisitizo wa Mheshimiwa imamu mkuu juu ya kupambana na mawazo makali na ugaidi.
Pia, Rais wa kifaransa alitoa shukurani kwa Imamu mkuu juu ya hotuba yake ya kimataifa aliyoitoa kwa mataifa wa bara la Ulaya na waislamu ulimwenguni wote, akisisitiza kuwa hotuba kama hii huchangia kikubwa kusahihisha ufahamu usio sahihi kuhusu Uislamu, akidokeza kwamba nchi yake inafanya bidii kuwafanya waislamu waishi nchini Ufaransa wakijipata uhuru na heshima ambapo nchi hiyo ilianzisha Baraza la kifaransa la waislamu wanaoishi nchini humo na kongamano la mazungumzo kwa lengo la kuimarisha husiano baina ya waislamu hao na mashirika yote yanayowawakilisha waislamu wa kifaransa.
 Rais wa kifaransa alielezea kwamba nchi yake inataka kushirikianana Al-Azhar Al-Shareif katika kuwapa maimamu na walinginiaji mazoezi na matayarisho ya lazima, jambo linaloweza kurahisisha kubadilishana zoefu na ujuzi ambazo maulamaa wa Al-Azhar Al-Shareif wanazo na hasa hasa katika uwanja wa kupambana na mawazo makali na ugaidi, akibainisha kuwa ushirikiano huo unaweza kuwa katika kuandaa tafiti na masomo ya pamoja na pia kuainisha baadhi ya tuzo za kimafundisho kwa wanafunzi wa Al-Azhar ili kufanya mawasiliano na kubadilishana zoefu na ujuzi, hasa tukitambua kuwa Ewe Mheshimiwa una uhusiano mzuri na utamaduni wa kifaransa, Hollande alisisitiza pia udharura wa kutafuta suluhisho la kisiasa kwa suala la kipalastina, akibainisha kwamba nchi yake ilitoa wito kwa kulitatua tatizo hilo, na kwamba Ufaransa ina uhusiano usio na mfano na Misri ambayo inazingatiwa ni mojawapo nchi muhimu zaidi katika eneo la mashariki ya kati.
Mwishoni mwa mkutano, Rais wa kifaransa alisema kwamba inapaswa kufanya juhudi zote na kuimarisha njia zote za kueneza fikira za mazungumzo baina ya dini tofauti nchini Ufaransa, akisisitiza kuwa anatambua vyema umuhimu wa jambo hilo hasa katika kipindi hicho ambapo ulimwengu unashuhudia changamoto nyingi.
Hollande alielezea umuhimu wa mkutano wa kilele uliofanyika baina yake na Mheshimiwa Imamu mkuu na Pop Francis Baba wa Vatican katika mji mkuu wa Italy, Rome, akisisitiza kwamba mkutano huo ulikuja katika wakati muhimu sana ili kuthibitisha umuhimu wa mazungumzo baina ya dini tofauti na kuishi pamoja, akielezea mshangao wake binafsi kwa Mheshimiwa Imamu mkuu kwa kuchukua hatua muhimu hii kwa ajili maisha iliyo bora zaidi kwa wanadamu wote.
Mkutano wa Imamu mkuu na Rais wa kifaransa ulishuhudiwa na waziri wa mambo ya nje wa kifaransa Jan Mark Ero, na waziri wa mambo ya ndani na mshauri wa Rais kwa masuala ya kidini Bernar Kaznouv kutoka upande wa kifaransa, ilhali kutoka Al-Azhar Al-Shareif wajumbe waliohudhuria ni pamoja na; profesa; Mahmoud Hamdy Zaqzouk mkuu wa kituo cha mazungumzo katika Al-Azhar, Kadhi; Mohammad Abdul-Salam mshauri wa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar na mbalozi wa Misri nchini Ufaransa Ehab Badawy. 
 
 
Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.