Ukingoni mwa ziara ya Imamu Mkuu nchini Ufaransa…

  • | Thursday, 26 May, 2016
Ukingoni mwa ziara ya Imamu Mkuu nchini Ufaransa…

Ukingoni mwa ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa Baraza la wakuu wa waislamu kwenda mji mkuu wa Ufaransa, Paris…yule mheshimiwa alimwakilisha profesa; Ibrahim Al-Hudhud mkuu wa Chuo kikuu cha Al-Azhar ili kutia saini mkataba wa ushirikiano baina ya Chuo kikuu cha Al-Azhar na Chuo kikuu cha Kikatholiki mjini Paris katikia nyanja za utamaduni, ufasiri, fasihi na mazungumzo baina ya dini mbali mbali.

Na katika hotuba yake, Profesa; Ibrahim Al-Hudhud alisisitiza kwamba Al-Azhar Al-Shareif tangu uanzishi wake ina mwono wazi kuhusu tamaduni zote, akibainisha kuwa Chuo kikuu cha Al-Azhar kinatia maanani sana ushirikiano baina yake na mashirika ya kielimu na ya kidini yote ulimwenguni kote; ambapo kinawatuma wana wake watafiti kila pande duniani ili kupata elimu mbali mbali, pia kinawapokea maelfu ya wanafunzi wageni ambao wanakuja kutoka zaidi ya nchi mia moja duniani kwa ajili ya kusoma katika Al-Azhar Al-Shareif.

Al-Hudhud aliongeza kuwa Uislamu unawafuza wafuasi wake kujuana na kuwasiliana na wanadamu wengine bila ya kujali kutofautiana nao kidini au kiutamaduni, akibainisha kwamba Al-Azhar Al-Shareif ililazimika kwa ujumbe huo ambao unasisitiza kuwa Uislamu ndiyo dini ya amani na rehema kwa malimwengu wote.

Kwa upande wake, profesa; Ussama Nabil, mkuu wa Kitengo cha Lugha ya Kifaransa, Kitivo cha Lugha na Ufasiri, Chuo kikuu cha Al-Azhar na mpangaji wa mkataba wa ushirikiano, alisisitiza umuhimu wa kushirikiana baina ya Chuo kikuu cha Al-Azhar na Vyuo vikuu vya kiualaya hasa hasa Chuo kikuu cha Kikatholiki ambacho kina umuhimu maalum kulingana na malengo ya pamoja baina ya vyuo vikuu hivyo viwili kuhudumia wanadamu wote, akibainisha kwamba kusoma fasihi za mataifa kama ni mwanzo wa mazungumzo ya kikweli baina ya tamaduni na dini inazingatiwa mbinu mpya ya kurekebisha dhana potofu kwa vijana hasa.

Kwa upande wake, mkuu wa Chuo kikuu cha Kikatholiki Philip Bordin alielezea furaha yake mkubwa na kusikia fahari kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Al-Azhar Al-Shareif ambacho kinasaidia kueneza fikira za mazungumzo na kuishi pamoja baina ya mataifa na jamii mbali mbali, akisisitiza kwamba ushirikiano huo ulikuwa ndoto kwake binafsi na kwa maprofesa na wanafunzi wote wa Chuo kikuu hicho ambao walikuwa wanatamani daima kuimarisha mawasiliano pamoja na Chuo kikuu cha Al-Azhar Al-Shareif.

 Pia, Bordin alieleza kwamba hotuba ya Imamu Mkuu kwa mataifa wa Ulaya aliyoitoa kwenye kongamano la pili la wenye hekima wa mashariki na magharibi, ilikuwa na athari kubwa mno katika nafsi za wananchi wa kifaransa ambao wanaiheshimu sana Al-Azhar Al-Shareif na mwenendo wake wa kiwastani, vile vile hotuba ile imetubainishia kiwazi wazi kwamba Imamu mkuu ana ufahamu, busara na msisitizo mkubwa wa kufanya juhudi za kupitisha amani na usalama kwa ajili ya maslahi ya mataifa.

  Akaongeza kuwa hotuba hiyo na mkutano wa kilele ulioitangulia uliofanyika baina ya Imamu mkuu na Baba wa Vatican ni hatua zinazoweza kuanzisha mazungumzo ya kweli baina ya mashariki na magharibi kwa kutegemea ushirikiano na kuishi pamoja, pia hatua hizo zinatusukuma mbele kwa ajili ya

kuendelea na kukamilisha hatua hizo za kuleta manufaa na kheri kwa mataifa wote duniani.

Mkuu wa Chuo kikuu cha Kikatholiki alisisitiza kwamba anaamini sana kuwa kazi ya pamoja na kushirikiana na Chuo kikuu cha Al-Azhar itarahisisha kufikia peo mpya za kufanya kazi ya pamoja baina ya wafuasi wa dini tofauti kwa lengo la mustakbali nzuri zaidi kwa wote kwa kutegemea mazungumzo, kufahamiana na kuishi pamoja kwa amani.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.