Katika mkutano wake na Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa

  • | Thursday, 26 May, 2016
Katika mkutano wake na Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa

Imamu Mkuu:

* Tunabidi kupanga kazi za maimamu na walinginiaji barani Ulaya kwa ajili ya kuchangia kueneza mawazo sahihi ya dini.

* Usalama wa nchi na utukufu wa damu ni jambo la kuzingatiwa sana…tunaiunga mkono Ufaransa kupambana na ugaidi.

* Tunathamini utashi wa Ufaransa wa kufikia suluhisho lafaalo kwa suala la kipalastina..na tunahimiza juhudi zile.

Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa: 

* Ziara yako Ewe Mheshimiwa imekuja katika wakati muhimu sana..na tunapambanua kabisa baina ya Uislamu na ugaidi.

* Tunahitaji kuwazingatia vijana na maimamu wetu..na ushirikiano wa Al-Azhar nasi katika kuhakikisha lengo hilo ni jambo la maana sana.

* Al-Azhar Al-Shareif ni taasisi yenye historia bora zaidi..na ziara yako kwa Alpataklan imetuathiria vizuri sana.

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa Baraza la wakuu wa waislamu, alisisitiza kwamba inabidi kuwepo kwa mfumo maalum unaodhibiti kazi ya maimamu na walinginiaji barani Ulaya kwa lengo la kuhakikisha maslahi za nchi na

kueneza fikira na utamaduni wa kiislamu zilizo sahihi pasipo na makosa au upotofu wo wote.

Katika mkutano wake na Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa Claude Bartolone Mheshimiwa Imamu Mkuu alisema kuwa usalama wa nchi na utukufu wa damu za watu wote ni jambo la kuzingatiwa sana na ni lazima tushirikiane pamoja kwa ajili ya kulifikia, akibainisha kuwa Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kufanya juhudi za ziada ili kuhakikisha lengo hilo na kueneza amani baina ya watu wote.

Mheshimiwa Imamu Mkuu akaongeza kwamba Al-Azhar Al-Shareif itasaidia Ufaransa na kuiunga mkono kupambana na ugaidi, akisisitiza kuendelea juhudi za Al-Azhar Al-Shareif kueneza mawazo ya kiwastani, amani na dhana sahihi badala ya dhana potofu katika viwango vyote vya kinyeji na kimataifa.

Imamu Mkuu alibainisha kuwa jinai zinazofanywa na baadhi ya makundi ya kikatili yanayojinasabisha kwa Uislamu kiuwongo hazihusiani na Uislamu hata kidogo, akiashiria kwamba mahusiano baina ya Misri na Ufaransa ni mahusiano ya kushirikiana kabisa kupambana na ugaidi, na kuwa Al-Azhar na Chuo kikuu chake na taasisi zake ziko tayari kupagania vita mawazo potofu hayo wakati wote, na kwamba msimamo wa Ufaransa kusaidia Misri inazingatiwa ni jambo linalostahiki kuthaminiwa mno hasa tukitambua kwamba Misri inateseka kutoka ugaidi katika baadhi ya maeneo yake.

Mheshimiwa Imamu mkuu akaelezea heshima yake mkubwa kwa utashi wa Ufaransa kutafuta suluhisho adili la suala la kipalastina, akisisitiza kwamba Al-Azhar Al-Shareif inahimiza juhudi hizo ikitumai zipate matokeo yake yanayotarajiwa karibuni sana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa Claude Bartolone alimkaribisha sana Imamu Mkuu akisisitiza kwamba ziara yake Mheshimiwa nchini Ufaransa ilikuja katika wakati ulio muhimu mno, akibainisha kuwa nchi

yake inapambanua kabisa baina ya Uislamu na jinai zinazofanywa na baadhi ya wahalifu.

Bartolone alisema pia: tunahitaji kuwazingatia vijana na kuwarahisishia nyanja zote, vile vile inapaswa kuwazingatia maimamu wa kifaransa ambao tunaamini kuwa tuna wajibu muhimu sana kuwafanyia, akisisitiza kwamba kujitayarisha kwa Al-Azhar Al-Shareif kushirikiana nao katika kuhakikisha lengo hilo ni jambo la maana sana.

Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa alisifu sana hotuba ya kimataifa aliyoitoa Imamu Mkuu kwa waislamu wa Ulaya na wa ulimwengu wote, akibainisha kwamba maneno ya Imamu Mkuu kuhusu kujiingiliana kwa waislamu na jamii zao nchini Ufaransa na barani Ulaya kwa ujumla kwa namna yanayotakiwa ni jambo ambalo linatarajiwa kuathiria vizuri sana waislamu wa kifaransa wanaoheshimu sana Al-Azhar Al-Shareif na Imamu Mkuu wake.

      Bartolone aliendelea akisema: tumejaribu sana kukupokea kwa mapokezi mema zaidi kama ipasavyo kwani wewe ni Imamu mkuu wa waislamu na unawakilisha shirika la kiislamu lililo kubwa zaidi kuliko dunaini, ambapo wafaransa wanatambua vyema cheo cha shirika hilo, pia wanatambua cheo cha ustaarabu wa kihistoria wa kimisri, akisisitiza kuwa nchi yake inatambua sana cheo kinachofaa kwa Misri katika eneo.

Mkuu wa Jumuiya ya kinyeji nchini Ufaransa alisisitiza kwamba nchi yake ina hamu kubwa ya kuimarisja mahusiano baina yake na Misri na Al-Azhar Al-Shareif, ambapo hatima zetu katika mashariki na magharibi zinafungamana yenyewe kwa yenyewe, na tunawaombeni kudumisha mapambano na kuzidisha juhudi zenu thabiti nchini Ufaransa na Misri na katika ulimwengu kote.       

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.