Nafasi ya Mwanamke na Vidhibiti vya kazi kwake kwa Mtazamo wa Kiislamu

  • | Sunday, 27 March, 2022
Nafasi ya Mwanamke na Vidhibiti vya kazi kwake  kwa Mtazamo wa Kiislamu
 

 

       Inafahamika kwamba mwanamke ana nafasi kubwa katika jamii, mpaka huitwa "Nusu ya Jamii", ambapo mwanamke amepewa nafasi, majukumu na cheo anachoshirikiana na mwanamme kutekeleza wajibu wake, kwani mwanamke anamsaidia mwanamme maishani. Kwa hiyo, Uislamu inamheshimu mwanamke na kumpa nafasi ya juu, kwa kuwa huwa sehemu ya maisha sambamba na mwanamme.

Kwa kuangalia hali ya mwanamke enzi za Jahiliya kabla ya ujio wa Uislamu na hata katika enzi za Warumi na Wayunani tunaona namna watu wa enzi hizi walikuwa wanamzingatia mwanamke kati ya vitu vya anasa na vifaa vinavyotumika nyumbani, kwa hiyo hakuwa na haki yoyote, ambapo mke anayefiwa na mumewe alikuwa halali kwa ukoo wake bila ya kuomba ridhaa yake. Imamu Al-Bukhariy alisimulia kuwa mwanamke wa enzi hizo hakuwa na haki ya kuchagua mumewe na hasa aliyefiwa na mumewe basi ukoo wake walikuwa wanashauriana akitaka mmoja wao kumwoa, au pengine kumwolewa kwa mwingine au kumzuia asioe, maana wao peke yao wanao haki ya kuainisha hatima yake kuliko yeye mwenyewe wala ukoo wake.

 

Pia, desturi za Waarabu kabla ya Uislamu zilikuwa zinawaruhusu kumshutumu mwanamke ambaye hawamtaki tena kwa zinaa ili aogope fedheha ambayo haipo kabisa na kulipa mahari aliyopewa kwa ajili ya kupata uhuru wake. Mwenyezi Mungu Amesema kukataza haya: {Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake * Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi? * Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?} [An-Nisaa: 19-21].

Dini ya Uislamu ilipokuja hali ya mwanamke imebadilika, ambapo mwanamke ametukuzwa akapewa haki zake akiwa sawa sawa na mwanamme kuhusu majukumu ya maisha ambapo kwa mtazamo wa Uislamu mwanamke ndiye msaidizi wa mwanamme na mwanamke bora zaidi ni yule anayemsaidia mumewe kuwajibika majukumu ya maisha, kama Mwenyezi Mungu (S.W.) Alivyoeleza sifa za mwanamke bora katika kauli yake: {Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} [An-Nisaa: 34].

Haya kwa mwanamke ambaye ni mke, ama kuhusu akina mama kweli Uislamu ilimtukuza sana mama ikawaamrisha wanawe wamtii na kuomba radhi yake wala wasimkasirishe na kubainisha kuwa ridhaa ya wazazi na hasa mama ni njia mojawapo njia za kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na baraka duniani na malipo mema Akhera; yaani Pepo. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu,na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu} [Al-Ahqaf: 15].

Inabainika kutokana na dua hii iliyotajwa katika aya tuliyoitaja kwa wazazi wawili kisha kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu kuitengeneza dhuriya na kuunganisha hii na kumtaja mama peke yake na kumtilia mkazo ni kwa sababu ya kuonyesha kuwa ana nafasi mkubwa mno na taabu anazozipata kuanzia ujauzito kisha kujifungua kisha unyonyaji kisha malezi na anaendelea kuwalea wanawe hata baada ya wafike utu wao mzima. Hayo yanaashiria kuwa Uislamu imemtukuza mama ikikiri fadhila zake na mchango wake ikijikita pia nafasi yake kuwalea wanawe kwa kujibu wa misingi ya malezi mema iliyopitishwa na Uislamu, jambo linalochangia kukiandaa kizazi cha waislamu wanaolazimika kufuata njia iliyonyooka wakishikilia tabia njema kama walivyolelewa na mama zao.

Kuhusiana na jambo hilo, Bin Al-Anbariy amesimulia kutoka kwa Abban bin Taghlib kwamba alisema: "Nilimsikia mama wa bedui mmoja akimwusia wanawe aliyetaka kufunga safaria kasema: Ewe mwanangu! Hebu kae nikupe wasia yangu kwani wasia hii ni bora kwako kuliko mawazo yako mwenyewe, ewe mwanangu epukana na masengenyo kwani yanasababisha mizozo na chuki na kutofautisha wapenzi, wala usifuatilie dosari za watu, wala usiuze dini yako kwa ajili ya kuwa na utajiri wa pesa, na ukitaka kuwa na rafiki basi ambatane na mwenye heshima na dini ambaye ukimhitaji atakusaidia, wala usiwe na rafiki mbaya ambaye hatakuwa na manufaa kwako wewe duniani wala dini, fahamu kuwa khiyana ni sifa mbaya zaidi kuliko na watu na anayesifika kwa upole na ukarimu huwa amepata heri zote" Hivyo tunaona vipi mama huyu alimpa mwanawe nyasia za kumfanikisha duniani na Akhera akimwelekeza kwenye heri zote na kumkataza shari zote, hivyo ndivyo malezi yanayotakiwa.

Sheria ya kiislamu ilipokuwa inatambua haki za mwanamke kuwa na kazi hasa katika shughuli ambazo zinabidi kufanywa na mwanamke, iliainisha vidhibiti na masharti maalum kwa kazi ya mwanamke kwa mtazamo wa kiislamu, vidhibiti hivyo na masharti haya ni pamoja na:

  1.   Kazi iwe inafaa kwa mwanamke kimwili, kimaumbile na kiroho kama vile kufanya kazi katika sekta ya elimu, kuwatunza watoto na kutoa huduma za matibabu kwa wanawake.
  2. Kazi isipingane na jukumu lake la msingi la kutunza nyumba  na familia yake (mume na watoto), maana nyumba yake isiathiriki vibaya kutokana na kazi yake hiyo.
  3. Kazi iwe baada ya kuomba ruhusa ya waliye yake ambaye ni wazazi au mume akiwa ameolewa.
  4. Kazi iwe haina maovu wala vitu vilivyo haramu kisheria kama vile uasherati n. k.
  5. Atoke akiwa mcha Mungu na kuwajibika mwenendo wa kiislamu na tabia zilizo bora kimaneno na kivitendo na aepukana na kuwa sababu ya kuwashawishi wengine wala hakubali kushawishika na wengine.
  6. Awajibike kwa mavazi ya kiislamu na adabu Alizozieleza Mwenyezi Mungu (S.W.) katika kauli yake: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao} [An-Nuur: 31].

    Hivyo ni baadhi ya vidhibiti na adabu za kisheria ambazo mwanamke anatakiwa kulazimika nazo wakati wa kutoka kwa kazi (akiwa amedharurika) ili apate ridhaa ya Mwenyezi Mungu na afanikiwe duniani na Akhera, na kwa lengo la aweza kutimiza kazi yake ipasavyo kama ilivyopitishwa kisheria.

Mwishoni, ukweli wa kwamba Uislamu ni dini ya kumtunza na kumheshimu mwanamke uko wazi kwa kila mwenye akili na uadilifu kwa kuwa hali ya mwanamke kabla ya ujio wa Uislamu iko tofauti kabisa na hali yake baada ya nuru ya dini hiyo kutawala dunia, hivyo madai ya kwamba mwanamke ana nafasi ya chini katika Uislamu hayana maana hata kidogo kwani dini ya kiislamu na sheria yake hudhamini haki za mwanamke na kuwasihi wanaume wazingatie na kutambua haki hizo.

Kwa upande wake, Al_Azhar Al-Sharif na taasisi zake zote ikiwemo Kituo cha Al_Azhar cha Kupambana na Fikra Kali inampa mwanamke haki za kujielezea na kuwa na mchango katika maendeleo ya umma wake, kupitia kazi na juhudi anazozifanya kwa kushirikiana na wanaume wenzi wake. Mifano iko mingi kwa wanawake walioongoza wanaume katika nyanja mbalimbali wakifaidika kwa uhuru wanaopewa na Uislamu na ufahamu sahihi wa sheria zake.            

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.