Ramadhani ni mwezi wa kufunga, kusimama, na kusoma Qurani, nayo ni mwezi wa ukarimu, wema, huruma, msamaha, na kufanya kheri, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: ﴾Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi﴿ [AL – BAQARA: 185]. Na bila shaka kufunga Ramadhani ni njia ya ucha Mungu ambao ni kumtii Allah na Mtume wake kwa kufanya maamrisho na kuacha makatazo kwa moyo safi na ikhlasi kwa ajili ya Allah (S.W). Kufunga Ramadhani kunatupatia faida na hekima nyingi sana, ikiwa ni pamoja na kujisafisha nafsi na kuitakasa na maadili mabaya, na kuizoesha maadili mema.
Waislamu na wasio waislamu tangu kuasisiwa kwa dola ya Kiislamu ndani ya Mji wa Madina chini ya kiongozi wa kwanza Mtume (S.A.W) daima walifurahia usalama, amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kweli, ambapo wanadamu walihifadhiwa damu zao, mali zao, na heshima zao.
Lakini hali hiyo haikufurahisha makundi ya kigaidi na wapiganaji wake ambao walikuwa na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hao wanakwenda mbio usiku na mchana kuweka vikwazo dhidi ya waislamu hata katika mwezi huo mtukufu, ambapo damu zao zamwagwa ovyo, mali zao zaporwa ovyo, heshima na matukufu yao yakejeliwa kwa mikono ya magaidi ambao hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi. Makundi ya kigaidi yanauzingatia mwezi wa Ramadhani ni nafasi kubwa ya kumwaga damu kwa kisingizio cha kuwa ni mwezi wa Jihadi, ambapo yanazidisha mashambulizi yao ya kihalifu wakati wa mwezi huo, na kubadilisha mnasaba wake karimu na furaha yake kwa mabwawa ya damu na huzuni na kusumbua usafi wa ulimwengu wa kiislamu.
Makundi yale katika kufanya vitendo vyake vya kigaidi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani yanategemea kuhojiana kwa vita vya kihistoria vilivyopigwa katika mwezi huo, lakini ni kuhojiana kwenye makosa ambako kunapunguka kusoma muktadha za kihistoria na kijamii za zilizotokea wakati wa vita vile vya kihistoria.
Kwa visingizio hivyo tunaendelea kushuhudia hadi hivi sasa waislamu duniani wakishambuliwa na makundi hayo ya kigaidi kama Daesh, Shabab la Kisomalia, na Boko Haramu na mengineyo.
Kwa upande wa Afrika, bara hilo likawa likizungukwa kimashariki na kimagharibi baina ya migodi na makombora ya kundi la Shabab, mabomu na mikanda ya mabomu ya kundi la Boko Haram, na vurugu za makundi ya waasi na vikosi vyenye kubeba silaha hapa na pale, kama kwamba makundi hayo yanakataa kufurahia Waafrika kwa usalama na utulivu hata kwa siku moja.
Pamoja na kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, makundi hayo hayajasitasita kumwaga damu na kutekeleza mipango yake ya kiuhalifu, yakifumbua macho na utakatifu wa mwezi huo na uharamu wa kumwaga damu, tangu siku za mwanzo za mwezi wa Ramadhan, makundi hayo yamekuwa yakizidisha harakati zake na vitendo vyake vya damu. Na miongoni mwa mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa katika mwezi wa Ramadhani ni yale yaliyotokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi inayoathirika zaidi kwa harakati za kundi la waasi ambalo haliahiriki katika kueneza hofu na umwagaji wa damu za watu wasio na hatia, ambapo mashambulizi yake hadi kufika nusu ya mwezi mtukufu yamesababisha kuwaua watu 102 na kujeruhiwa makumi na kuchoma moto nyumba za wakazi.
Na kwa kuhamia magharibi ya bara, hasa Nigeria, tunaona kwamba hali inaweza kuonekana tofauti, lakini matokeo ni moja; damu inamwagwa bila hatia, usalama unakuwa kama ni ndoto tu, vyote hivyo si ila kwa sababu ya vitendo vya kiadui vya Boko Haram, Daesh Afrika magharibi, makundi ambayo yaliyojitokeza katika mfumo wa mafundisho ya Uislamu na kanuni zake, na kukiuka mipaka ya haki za binadamu, ambapo magaidi walishambulia vijiji kadhaa vya wilaya ya “Blato” katikati ya nchi na kuwaua watu 80 na kujeruhiwa mmoja.
Ama huko nchini Burkinafaso, watu wasiopungua 20 waliuawa na wapiganaji wanaopepa silaha ambao walishambulia kijiji cha “Barja” kaskazini mwa nchi. Vile vile shambulio lingine lilitokea nchini Benin mpakani mwa Burkinafaso lililosababisha kuwaangamia wanajeshi watano na kujeruhiwa mwingie.
Na kwa kusikitika sana, hali hiyo imepelekea Waislamu kuishi kwa hofu wasijue kesho wataamkia lipi jipya. Kwa mujibu wa hayo, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kina mtazamo kwamba makundi hayo yenye siasa kali hayanyimwi na utakatifu wa mwezi na wala mahali kama hayanyimwi na heshima ya damu ambayo kwa Mwenyezi Mungu ni zaidi kuliko heshima ya nyumba yake takatifu (Ka’bah), lakini makundi hayo yanapata siku hizi nafasi ya dhahabu kwa ajili ya kutekeleza mipango yake ambayo yanaizingatia ni Jihadi iliyoruhusiwa, lakini katika mizani ya Sheria na akili ni uhalifu na ukatili. Vile vile, Kituo cha Al-Azhar kinatoa wito kwa kuendelea mapambano katika ngazi zote kimawazo, kivita na kutumia silaha zote halali katika vita hii kali dhidi adui ambayo inafanya bidii ili kusambika ajenda yake iliyochafuka na damu ya watu wasio na hatia bila ya kujali. Pia Kituo cha Al-Azhar kinatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na ugaidi huu, ambao umekuwa balaa kwa wanadamu wote na ulimwengu kote, kikimwombea Mwenyezi Mungu Mtukufu kuneemesha usalama na amani duniani.
Mwishoni Kituo cha Uangalizi cha Al_Azhar kinawatakia waumini wote duniani mfungo mwema na funga zenye kukubaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu (S.W), kikitamania kueneza amani na usalama ulimwengu kote.