Al_Azhar yalaani shambulio la kigaidi kwenye moja ya vituo vya maji magharibi mwa Sinai, na kuwaomboleza mashahidi wa nchi

  • | Sunday, 8 May, 2022
Al_Azhar yalaani shambulio la kigaidi kwenye moja ya vituo vya maji magharibi mwa Sinai, na kuwaomboleza mashahidi wa nchi

     Al_Azhar Al-Sharif inalaani vikali shambulio la kigaidi lililolenga kituo cha kuinua maji magharibi mwa Sinai, ambalo lilisababisha kifo cha afisa mmoja na wanajeshi 10, na wengine 5 kujeruhiwa.
Al_Azhar inasisitiza kwamba Wamisri wanasimama safu moja na mashujaa wetu wa wanajeshi na maafisa wa vikosi vyetu vya kijeshi na polisi wetu wajasiri, katika vita dhidi ya ugaidi huu mbaya, ikiunga mkono tena na tena juhudi zinazofanywa na vikosi vya kijeshi na polisi katika kukabiliana na ugaidi, ikimwomba Mwenyezi Mungu Aziwekee juhudi hizo mafanikio na kuutokomeza kabisa ugaidi huu katika mizizi yake.
Mheshimiwa Imamu Mkuu Dk. Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al_Azhar Al-Sharif, anatoa salamu za rambirambi kwa Rais Abdul Fattah Al-Sisi, Rais wa Jamhuri, kiongozi mkuu wa vikosi vya kijeshi, na kwa familia za mashahidi wetu mashujaa, kwa vikosi vyetu vya kijeshi, na kwa watu wa Misri, akimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Awarehemu, Awaingize katika bustani zake kubwa, na Azifunge nyoyo za mama zao, Aiweke mioyoni mwa familia zao na jamaa zao subira na faraja, Awape waliojeruhiwa kupona haraka, na Ailinde Misri na watu wake kutokana na madhara na maovu yote, “Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea”.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.