Mchango wa Elimu na Utamaduni katika Kujenga mtu mwenye nafsi na akili timamu

  • | Sunday, 19 June, 2022
Mchango wa Elimu na Utamaduni katika Kujenga mtu mwenye nafsi na akili timamu

     Inatajwa kuwa imani ya kweli inahimiza tabia njema na mwenendo mzuri unaotokana na maadili mema na kudhibiti maumbile ya mtu kukubali lililo sawa na kukataa mabaya na maovu.
Kwa mujibu wa sheria ya kiislamu mwanadamu anatakiwa kujengwa hata kabla hajafika duniani, ambapo malezi yanaanza kabla ya kuzaliwa kwake kwa kumchagua mke na kuunda familia inayojenga jamii nzuri yenye maadili na mafanikio. 
Kwa mtazamo wa Uislamu mwislamu anatakiwa awe na mfano bora wa kuigwa ambaye huwa na sifa nzuri kidini, kitabia kistaarabu, kiutamaduni na kielimu. Kwa hiyo, elimu na utamaduni ni miongoni mwa misingi ya kujenga mwanadamu na kuunda nafsi yake kwa namna inamfanya mtu mwenye heshima na cheo katika jamii yake.
Mambo mengine yanayosaidia kujenga mwislamu ni pamoja na elimu, fikra, utamaduni na mwenendo bora, ambapo haya yote yanazingatiwa misingi na nguzo za kurekebisha nafsi na kuitakasa roho ya mwanadamu yeyote.
Elimu ni njia ya pekee ya kuleta amani na utulivu kwa umma wowote kwa kuwa elimu inawachochea wananchi kujenga umma wao, kuendeleza na kulinda jamii na nchi yao. Kwa hiyo si la kushangaza kukuta Uislamu uliipa elimu heshima kubwa mno na kuwatakasa wataalamu na kuwapa cheo cha juu kabisa mpaka wakawa warithi wa Manabii na Mitume, isitoshe Mwenyezi Mungu (S.W.) Akawafanya wataalamu kuwa mashahidi wa upweke wake kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima} [3/18].
Naye Mtume (S.A.W.) aliwafaradhishia waislamu kutafuta elimu akabainisha ubora wa mtaalamu kuliko anayefanya ibada ilhali hana kiasi chochote cha elimu. Uislamu unawaita wafuasi wake kujifunza na kufundisha na ukawapa wataalamu nafasi kubwa katika dini. Kwa kuwa vijana ndio nguzo iliyo muhimu zaidi kwa umma wowote wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha kwa ajili ya waweze kukabiliana na mawimbi ya kuwavutia wajiunge na fikra kali na misimamo ya kigaidi.


Kwa hakika majaribio ya kuwashawishi vijana yako mengi na yanaendelea kwa kutambua nafasi yao kujenga au kuangusha umma wowote, jambo linalotulazimisha kuwahimiza vijana wetu hawa wajikanga na majaribio ya ushawishi haya na kupambana na shughuli za kuwavutia kwa njia mbaya hii. Kinga hiyo haitapatikana isipokuwa kwa yule anaye elimu ya kutosha kumwelekeza kwenye njia iliyo sawa na kumjulisha namna ya kuepukana na njia isiyo sahihi. Kwa kuwa wafisadi wanaojitahidi sana kuzichafua akili za vijana na kuwatumia vibaya kuziharibu jamii na kusababisha maangamizi mabaya, kwa ajili ya hali hii tunatakiwa kufanya jitihada kubwa zaidi kuliko kwa ajili ya kuwakinga na kulinda vijana wetu kutoka shari na fitina hizo.
Inafahamika kuwa elimu ni msingi mojawapo misingi ya maendeleo ya umma na sababu ya mafanikio, kwa hiyo, jamii isiyo na elimu ya kutosha huwa jamii rahisi kushawishiwa na kuharibika, huku jamii inayohimiza wananchi wake kujifunza fani mbalimbali za elimu ya sheria, dini na sayansi za kiutendaji.
Kwa hakika makundi ya kigaidi yanakusudia kuwavuta vijana ambao akili zao ziko tupu hazina elimu wala mafunzo yoyote yanayoweza kuwasaidia kutambua yaliyo sahihi na yaliyo kosa. Japokuwa baadhi ya waliovutwa na makundi haya walikuwa wameshapata kiasi cha elimu lakini si kiwango wala aina ya elimu kinachowalinda kutoka kwa hatari ya kushawishiwa na kuathirika kwa fikra hizo.
Inafahamika kwamba wafisadi wanaotaka kueneza vurugu na ugaidi duniani wanakusudia kuwatumia vijana kwa kuwa vijana hawa wana nafasi kubwa zaidi kuliko katika umma wowote ambao wana uwezo wa kubadilisha hali halisi ya mambo, jambo linalosisitiza ukweli wa kwamba vijana hawa ndio silaha muhimu zaidi kwa umma wowote. Kwa hivyo, kuwaelimisha vijana hawa na kuwakinga kutokana kwa fikra mbaya na maoni yanayowaelekeza kwenye njia za ukatili, vurugu na ugaidi.
Inatajwa pia kwamba vijana ndio msingi wa maendeleo ya umma na tegemeo la mwamko wake, kwa sababu vijana ni ukwasi ulio ghali wa umma, maana umma wowote huwa na hazina mbalimbali .. hazina za kiuchumi, kijeshi, kijiografia, na za kibinadamu, lakini hazina iliyo muhimu zaidi kwa umma ni hazina ya kibinadamu, ile hazina ambayo inaundwa na kuimarika sana kwa vijana.
Kama ungetaka kujua mustakabali wa taifa lolote, basi usiulize juu ya dhahabu yake na hazina yake ya kifedha, lakini unaweza kuangalia vijana wake na mambo gani wanayoshughulikia nayo, basi ukiwakuta vijana hao wanashikilia Dini, basi utambue kuwa ni taifa kubwa lenye hadhi nzuri na ujenzi nguvu, ama ukiwakuta vijana hao ni wamepoteza maadili wakawa na tabia mbaya wakishughulikia mambo duni na maovu, basi ujue kuwa ni taifa dhaifu (nyonge), litakaoanguka kwa haraka mbele ya maadui wake, kwa hivyo basi vijana ni msingi wa umma na sababu ya kuimarika au kuanguka kwake.
Vile vile, shughuli ya kupambana na ugaidi wa kifikra ingalianza mapema, ingalikuwa na manufaa makubwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo na kushauriana kama ni suluhisho lenye athari kubwa kumaliza hali hiyo, ambapo mazungumzo ni mtindo na mbinu unaofaa kuunda dhana sahihi na kubainisha haki na kudhihirisha ufisadi wa baadhi ya itikadi, tuhuma na fikra, pamoja na kunufaika na wanavyuoni wa sheria, wataalamu wa kisaikolojia na kijamii, kwani wana elimu, maarifa na uzoefu.
Kwa hiyo, wanaweza kuwakinaisha wale walioathirika kwa fikra za kigaidi, na kurekebisha istilahi potofu na maoni mabaya waliyo nayo kuhusiana na familia, jamii na nchi nzima. Mashirika, Taasisi na mamlaka watakiwa kupambana na magaidi hawa, kwa lengo la kufanya hivyo ili wale ambao wameshawishiwa kuharibu nchi, kufanya vurugu na mauaji, kusababisha ghasia na uharibifu wa aina yoyote waelewe kuwa wanafanya hatia kubwa zilizokatazwa katika sheria ya kiislamu.
La kuzingatiwa ni kwamba Al_Azhar Al-Sharif kwa idara na taasisi zake inatekeleza ujumbe wa hali ya juu sana nao ni kueneza elimu na kuwaongoza wanadamu wote kwenye njia sahihi na kuchangia kwa namna ama nyingine katika kupitisha amani na utulivu katika jamii mbalimbali. Kwa mujibu wa ujumbe huo mtukufu, Al_Azhar Al-Sharif inatoa wito wa kuzingatia na kuipa shime elimu na kuhakikisha kuwa kinga ya elimu na utamaduni kinaweza kukabiliana na matatizo ya zama hizi yakiwemo janga la kifikra pamoja na majanga mengine kama vile Uviko-19 na mengineyo.
Kuhusu namna ya kukabiliana na janga la kifikra ambalo ni kupotosha fikra za vijana na kuwashawishi kutowajibika kwa maadili ya dini na maumbile ya kibinadamu, Al_Azhar inasisitiza katika mnasaba na mahafali mbalimbali kuwa elimu ni kinga cha msingi cha kuzuia vijana wasiathirike kwa mawazo potofu yanayosambazwa na makundi ya kigaidi na kuhimiza kueneza elimu na utamaduni wa kujiboresha kifikra na kimada.
Vile vile kituo cha uangalizi cha Al_Azhar kimetoa matoleo mengi yanayohusiana na jambo hilo, ambayo yanaashiria umuhimu wa elimu na roli ya familia katika kulinda watoto wao wasivutiwe na makundi ya kigaidi na mawazo yao potofu.
Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kuwapa dawa kwa kila janga au maradhi sawa sawa ni maradhi ya kimwili au ni ya kiroho au kiakili. Lakini mwanadamu anatakiwa kuchagua dawa inayofaa hali yake na kujikinga dhidi ya magonjwa ya zama anapoishi hasa magonjwa ya kifikra kwa kutumia neema ya akili aliyopewa na Mola wake kwa lengo la kumpa nafasi bora zaidi kuliko viumbe wengine.
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.