Viongozi wa dini dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

  • | Tuesday, 5 July, 2022
Viongozi wa dini dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

     Kwa kufuatilia majaribio ya kuingiza mawazo potofu ambayo yanayokwenda kinyume na dini zote za mbinguni na kuyalazimisha kwenye jamii, kituo cha uangalizi cha Al_Azhar cha kupambana na fikra kali kilifuatilia mikutano ya mheshimiwa Imamu Mkuu, Prof. Ahmad Al-Tayyib, Sheikh wa Al_Azhar Al-Sharif, katika siku mbili zilizopita na viongozi wa makanisa na madhehebu ya Kimisri, juu ya shambulio kali la wito kwa mapenzi ya jinsia moja, ambayo unatishia mfumo wa maadili ya kidini na kitabia na kiroho yaliyoimarishwa ulimwenguni tangu Mwenyezi Mungu Aliumba ardhi na wale walio juu yake, na ambayo ubinadamu umeyaumbiwa na kukua tangu nyakati za zamani.
Mikutano hiyo pia ilishughulikia vitendo vya vurugu vilivyoonekana barabarani, viwanja na shule, vilivyosababisha mauaji ya roho ambayo Mwenyezi Mungu Alikataza kuiua isipokuwa kwa njia ya haki, na pia uharibifu mazingira unaosababisha mabadiliko makubwa katika hali ya hewa ambayo yalipelekea Kuibuka kwa maafa mengi ya kiasili, ambayo inahitaji msimamo mkubwa mbele ya tabia hii na umuhimu wa kuikomesha, ili kuhifadhi mfumo wa maadili ya kidini na kimaadili, na pia kulinda ubinadamu kutokana na hatari hizi, hata pia ulimwengu wote kutokana na ile itakayosababishwa na majanga, misiba na uharibifu.
Waliohudhuria wamekubaliana kuongeza juhudi zao za kuchukua msimamo moja wa kukabiliana na hatari hizi zote na kuweka njia timamu za kukabiliana nazo. Vile vile wamekubaliana kufanya mikutano ya kitaifa, kijimbo na kimataifa kwa ajili ya hayo.
Al_Azhar inatoa wito kwa jamii ya kimataifa kwa umuhimu wa uasi ili kukabiliana na hatari hizi, na kufanya kazi kama mkono mmoja ili kuhifadhi mfumo wa kimaadili kidini na kuyahuisha tena ili kuhifadhi ubinadamu na utu.
Al_Azhar Al-Sharif pia inaombea nchi tofauti za ulimwenguni kueneza uelewa wa hatari hizi na njia tofauti zinazolenga kuzihimizia na kuzitetea, haswa kile kinachohusiana na ushoga kwa sababu ya kuumia kwa ubinadamu wote na misiba, na janga na maafa, na pia Al_Azhar inatoa wito kwa nchi za Kiisilamu - viongozi na raia - wasizembe kukabiliana na kupinga hatari hizi kwa nguvu zote, azimio na ujasiri.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.