Akimpokea mkuu wa Chama cha Kikristo cha Kidomkrasia cha kifaransa

  • | Friday, 27 May, 2016
Akimpokea mkuu wa Chama cha Kikristo cha Kidomkrasia cha kifaransa

Imamu Mkuu:

* Al-Azhar ina hamu kubwa ya kupambana na mawazo makali..na tuko tayari kuwapa maimamu mafundisho na mazoezi.

Mkuu wa Chama cha Kikristo cha Kidomkrasia cha kifaransa Frédéric Poisson:

* Nchi za kimagharibi zinahitaji kufaidika kutoka kwa juhudi za Al-Azhar…na ziara zako Ewe Mheshimiwa kwenda Alpataklan inaelezea hisia za kiutu za hali ya juu.

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa Baraza la wakuu wa waislamu, alipokea kwenye mahali pa kukaa kwake mjini Paris Jean Frédéric Poisson mkuu wa kikundi cha kupambana na kundi la Daesh, makamu wa rais wa tume ya sheria katika baraza la kitaifa la kifaransa, mkuu wa Chama cha Kikristo cha Kidimokrasia.

Ambapo katika mkutano huu Mheshimiwa Iamamu mkuu alisisitiza kwamba Al-Azhar Al-Shareif ina hamu kubwa ya kupambana na mawazo makali kwa kutumia mbinu mbali mbali, akibainisha kuwa Al-Azhar ilianzisha kituo cha Uangalizi kwa lugha nane za kigeni kwa ajili ya kujibu madai ya Daesh na kusahihisha dhana kosa hasa kwa vijana, akiashiria kwamba kuna mkakati wa kuendeleza kituo hicho katika kipindi kijacho na kuongeza lugha nyingine.

Mheshimiwa Imamu Mkuu alisema: kuna mbinu kadhaa tunazozitumia ili kupambana na mawazo haya sawa kupitia mikutano, kongamano, vitabu au tafiti, pamoja na kuituma misafara ya ulinginiaji na misafara ya amani ambayo inazunguka mabara yote duniani kwa lengo la kusisitizia msamaha wa Uislamu na kutoa wito ya kuishi pamoja kwa amani na usalama.

  Mheshimiwa yule alisisitiza kuwa Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuwapa maimamu wa kifaransa mazoezi ya lazima na kuwaandaa kwa mujibu wa mbinu ya uwastani na usawazisho, akiombea udharura wa kupitisha misingi maalum ya kuzingatiwa katika misikiti yote nchini Ufaransa kwa kuangalia Daawa inayoafikiana na uhuru wa misikiti na jamii husika na kupitisha adhabu kali kwa ye yote huenda kinyume cha kanuni na misingi hizo kwani atakaevuka kanuni hizo huzingatiwa anasaidia kueneza mawazo makali na hustahiki kupatwa na adhabu.

Mheshimiwa alieleza pia kwamba wito wa Uislamu huwa kwa kutumia hekima na mawaidha mazuri, wala haiwi kwa kuwaua watu wala kuwalazimisha waache makazi yao au kwa kuzimwaga damu na kufanya jinai kama vile wanavyofanya wafuasi wa makundi ya kigaidi ambayo hayahusiani kamwe na Uislamu ambayo ndiyo dini ya kusameheana.

Kwa upande wake, Poisson alitoa shukurani zake kwa Mheshimiwa Imamu mkuu akisisitiza kuwa ziara yake hiyo imekuja katika wakati muhimu mno, akizisifu juhudi zinazofanywa na Al-Azhar Al-Shareif kueneza uwastani na amani na kupambana na mawazo makali, akibainisha kuwa nchi za kimagharibi zinahitaji sana kufaidika kutoka kwa juhudi hizo na kuzitumia na kuzieneza baina ya vijana ili kuwakinga kutoka kwa hatari za mawazo ya kigaidi.

  Vile vile, Poisson alisifu ziara aliyoifanya Imamu mkuu kwenda Theater ya Alpataklan, akisisitiza kwamba ziara kama hii inabainisha hisia za huruma na rehema kubwa, akiashiria

kuwa ziara hiyo itakuwa na athari kubwa katika jamii ya kifaransa ambayo inaizingatia Al-Azhar Al-Shareif ndiyo taasisi ya uwastani na usawazisho.

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.