Kiashirio cha operesheni za kigaidi nchini za kifrika kwa mwezi wa Aprili 2023

  • | Tuesday, 9 May, 2023
Kiashirio cha operesheni za kigaidi nchini za kifrika kwa mwezi wa Aprili 2023


     Mwezi wa Aprili 2023 ulirekodi ongezeko kubwa la asilimia ya operesheni za kigaidi zilizofanywa na makundi yenye fikra kali barani Afrika, ikilinganishwa na Machi uliopita, kwa karibu 19%, ambapo mashambulizi 37 ya kigaidi yalirekodiwa mwezi huu, na ongezeko hili kwa kawaida lilisababisha ongezeko la idadi ya wahanga, na waliojeruhiwa, na watu waliotekwa nyara mwezi huu. Kwa sababu hiyo, wahanga (432) waliuawa, (118) walijeruhiwa, na (32) wengine walitekwa nyara. Wakati idadi ya operesheni katika mwezi wa Machi ilifikia operesheni (30) za kigaidi, ambazo zilisabibisha vifo vya watu (243), na (31) walijeruhiwa, na ( 8 ) wengine walitekwa nyara. Hii ni kutokana na hali ya kijamii na kiuchumi inayohusishwa na kuenea kwa ugaidi, ambapo makundi ya kigaidi yanatumia fursa ya umaskini na kutengwa ili kukusanya wanachama wao wapya, au hata kujiunga vijana wenyewe kwa makundi haya kwa hiari yao kutokana na hali mbaya inayowasukuma vijana wasio na ajira kujiunga na makundi kama haya kwa hamu ya kupata pesa.
Katika mwezi huo, eneo la Sahel ya Afrika, ambalo ni chanzo cha wasiwasi, lilishika nafasi ya kwanza kwa upande wa idadi ya operesheni za kigaidi na idadi ya wahanga, ambapo ilishuhudia mashambulizi (17) ya kigaidi, sawa na (45.9% ya jumla ya idadi ya operesheni za kigaidi zilizofanywa na makundi ya kigaidi katika bara katika mwezi huo), ambayo yalisababisha vifo vya watu (241) na (82) walijeruhiwa, pamoja na utekaji nyara wa wawili, Burkina Faso ikijumuisha operesheni (10) za kigaidi, zilisababisha vifo vya watu (209), na (12) wengine walijeruhiwa, Mali ilifanyiwa operesheni (6), ambazo zilisababisha vifo vya watu (27) na kujeruhiwa (67), Ama kuhusu Niger, ilishuhudia operesheni moja iliyosababisha vifo vya watu (5), na (3) walijeruhiwa, na (2) walitekwa nyara.
Kwa hivyo, eneo la Afrika la Sahel ndilo lililokuwa na umwagaji damu zaidi katika mwezi huu, Sababu ya hayo ni kutokana na kupanuka kwa makundi yanayofungamana na makundi ya “ISIS” na “Al-Qaeda”, kwa sababu ya changamoto nyingi na migogoro ya kiuchumi inayozikabili nchi za Sahel, na kuongezeka kwa matatizao dhidi ya rasilimali za nchi, ambayo yalisababisha kuteseka kwa watoto 970,000 kwa sababu ya utapiamlo kutokana na migogoro ya silaha katika nchi za kanda hiyo, kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), jambo linalohitaji hatua za haraka za kimataifa ili kukabiliana na janga na maafa ya kibinadamu yanayotokea nchi za eneo la Sahel barani Afrika, Pamoja na umuhimu wa kufanya kazi katika wakati mmoja ili kuboresha hali ya usalama katika eneo hilo ambalo limekuwa likishuhudia kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi kwa miaka mingi, na wahanga wengi wa vitendo hivyo ni kutoka raia.
Kulingana na takwimu, Afrika ya Magharibi ilishika nafasi ya pili kwa idadi ya mashambulizi ya kigaidi, na ya tatu kwa idadi ya wahanga, ambapo ISIS ya Afrika ya Magharibi na adui yake ya kigaidi Boko Haram waliishambulia kwa (9) operesheni za kigaidi, sawa na (24.3% ya jumla ya operesheni za kigaidi), ambazo zote zilitokea nchini Nigeria, na zilisababisha vifo vya watu (75) na (30) walitekwa nyara.
Kwa upande wa ukanda wa Afrika ya Mashariki, ilishika nafasi ya tatu kwa idadi ya mashambulizi ya kigaidi, na ya nne kwa idadi ya vifo, Somalia pekee ilikabiliwa na operesheni (6), sawa na (16.2% ya idadi jumla ya operesheni za kigaidi), ambazo zilisababisha kuuwawa na kujeruhiwa (3).
Imebainika kuwa kuna kupungua kwa operesheni za kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika mwezi huu, na hii kwa sababu ya juhudi zinazoendelea za serikali ya Somalia katika kupambana na kundi hilo la kigaidi na kuwasaka mabaki yake, pamoja na kurejesha maeneo mapya ambao yalikuwa chini ya udhibiti wa kundi, ambapo jeshi la Somalia kwa kusaidiwa na wakazi wa eneo hilo, liliweza kukomboa vijiji kadhaa vya mji wa "Galad" katika mkoa wa "Galgudud" katika jimbo la "Galmadug" katikati mwa nchi, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kinathibitisha kwamba msongamano wa kijeshi dhidi ya "al-Shabab" unakuja katika mwanga wa azma mpya ya kisiasa ya serikali ya nchi hiyo ili kukomboa maeneo yaliyosalia na kuondoa ugaidi, Kituo cha Uangalizi kinatumai kuwa kipindi cha pili cha kijeshi ndicho kitakuwa hatua madhubuti ya ukombozi wa Somalia na nchi jirani kutokana na tishio la makundi ya kigaidi.
Ama kanda ya Afrika ya Kati, ilishika nafasi ya nne kwa upande wa idadi ya operesheni, lakini ilishika nafasi ya pili kwa upande wa idadi ya vifo, ambapo eneo hilo lilikumbwa na mashambulizi (5) ya kigaidi, sawa na (13.5% ya jumla ya operesheni za kigaidi), ambayo yote yalisababisha vifo vya watu (113) na majeruhi (33), "Congo ya Kidemokrasia" pekee ilikabiliwa na mashambulizi (3) ya kigaidi yaliyofanywa na waasi wa " Vikosi vya Muungano wa Kidemokrasia" wa kundi la "ISIS", ambayo yalisababisha vifo vya watu (90) na (33) walijeruhiwa, wakati "Chad" na "Cameroon" zilikabiliwa na shambulio moja la kigaidi kwa kila nchi, ambalo lilisababisha vifo vya watu (17) katika la kwanza na (6) katika la pili.
Kuhusu juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi barani Afrika, idadi ya vifo vya magaidi ilifikia (321) waliokufa na (5) waliokamatwa, pamoja na kujisalimisha kwa magaidi (2), Katika eneo la Sahel, juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi zilisababisha kutengwa kwa wanachama wa kigaidi (205), ambapo takriban magaidi 150 waliuawa nchini Burkina Faso, huku serikali inayalenga makundi ya waasi kaskazini na kusini mwa nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi kwa mashambulizi ya anga, jeshi la Mali pia lilifanikiwa kuwaangamiza magaidi wengine (55).
Magharibi mwa bara hilo, jeshi la Nigeria lilifanikiwa kuwaua magaidi (65) kutoka kwa makundi ya "ISIS Magharibi mwa Africa" na "Boko Haram".
Kwa upande wa mashariki mwa bara, haswa nchini Somalia, serikali iliwaua wapiganaji (51) wa kundi la kigaidi la "Al-Shabaab", na iliwakamata (5), huku magaidi wawili wakijisalimisha kwa hiari yao kwa vikosi vya jeshi.
Kwa upande wake, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kinaamini kwamba kuna juhudi zinazofanywa na serikali za Afrika ili kukabiliana na vitisho vya ugaidi, lakini ni juhudi za mtu mmoja mmoja ambazo hazina ushirikiano wa nchi za mpakani pamoja na zile za kieneo, Kituo cha Uangalizi kinathibitisha kwamba hakuna nchi inayoweza kwa hali yoyote kusimamia usalama na amani yake kwa kutengwa na nchi jirani, kwani amani ya kudumu itapatikana tu chini ya kivuli cha usalama kwa wote, Kituo cha Uangalizi kinaonya kwamba iwapo jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kimataifa yanayohusika hayatakabiliana na upanuzi wa ugaidi barani Afrika kwa haraka na kwa kiasi kikubwa, basi jambo hilo litatishia amani na usalama wa kimataifa katika siku zijazo.
 

Print
Categories: Infographic
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.