Uislamu na (Dini) zingine

  • | Tuesday, 30 May, 2023
Uislamu na (Dini) zingine

      Mwanaadamu ni kiumbe mwenye utukufu Zaidi na anastahiki kuwa kiumbe kipenzi mbele ya Allah Mtukufu. Kwa mujibu wa Qur’an kila mwanaadamu hupewa heshima kwa fadhila ya kuwa tu ni mwanaadamu kabla hata watu hawajagawanywa kwa misingi ya imani au uzawa.

Quran inasema:

“Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vyakupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.." (Al-Israa:70)

Uislamu unasisitiza juu ya umoja wa wanaadamu kama familia na Qurani inasema:

Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni...." (An-Nisaa:1)

Watu wote wako sawa katika haki za msingi za mwanaadamu, zikijumuisha haki ya uhuru wa mtu kuchagua dini bila ya kutezwa nguvu, kwani katika Uislamu fursa ya "fikra nyingine" imehifadhiwa vyema na kulindwa. Uislamu si dini iliyojitenga, na hakuna mwanaadamu, kiongozi wa dini au mfuasi, anayeruhusiwa, kuweka mipaka ya huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na msamaha, au kuzungumza kwa niaba Yake katika kutoa malipo au adhabu. Hakimu wa mwisho ni Mwenyezi Mungu Mtukufu tu Peke Yake.

“… Kisha marejeo yenu nikwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwamkikhitalifiana."(Al-Anaam: 164)

Uislamu na Ahlul-Kitab: Wayahudi na Wakristo

Miongoni mwa watu Wayahudi na Wakristo ndiyo waliyo karibu zaidi na Waislamu na wao wamepewa cheo cha kuitwa watu wa Kitabu. Wao ni wenzao katika imani ya Mungu Mmoja Allah-Mtukufu na waliopokea maandiko kutoka Kwake, Taurati kwa Nabii Musa na Injili kwa Yesu (Nabii Isa bin Mariamu). Nao pia wana imani katika mlolongo wa unabii, na wengi katika marafiki zetu Mayahudi na Wakristo hushangazwa wanaposikia kuwa manabii wanaotajwa katika Biblia pia ni manabii katika Uislamu. Dini hizo tatu zina kanuni za kimaadili zinazofanana. Qur’an inasema;

"Semeni nyinyi: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyopewa Musa na Isa, na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake." (Al-Baqarah: 136)

Waislamu wanaruhusiwa na Uislamu kula chakula cha watu wa Kitabu (isipokuwa kile kilichoharamishwa kama vile pombe au nyama ya nguruwe) na Waislamu wanaweza kufanya vivyo hivyo kwa kuwapa chakula chao, Mwislamu mwanamume anaruhusiwa kumchukua Myahudi au Mkristo anayefuata mafundisho sahihi ya Nabii Isa bin Mariamu kama mke kwa kumwoa (uhusiano uliyo wa karibu mno uliyo barikiwa)n na Katika hali hiyo itakuwa haramu kwa mume Mwislamu kumlazimisha mkewe kuingia katika Uislamu, kwani itakuwa ni kinyume na agizo la Qur’an;

" Hapana kulazimisha katika Dini." (Al-Baqarah: 256).

Kwa hakika utakuwa ni wajibu wake wa kidini kuhakikisha haki za mkewe kuabudu kwa mujibu wa imani yake.

Waislamu wameonywa dhidi ya vitendo vya ubaguzi au kisasi au chuki kwa Watu wa kitabu, na Mtume Muhammad (S.A.W) amesema:

"Yeyote atayemdhuru mtu miongoni mwa Watu wa kitabu ni kama vile kanidhuru mimi mwenyewe."

Kwa mtazamo wa Uislamu watu wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na hakuna mtu au kundi kinachoweza kudai kuhodhi rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu au kuwanyima wengine, Qurani inasema:

" Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. ." (Al-Baqarah: 62)

Kituo cha Al-azhar cha kupambana na fikra kali ilitilia mkazo dhana hii ya kuamiliana  baina ya Waislamu na dini zote za Mwenyezi Mungu na baina ya Waislamu na viumbe vyote kwenye ulimwengu huu kupitia makala nyingi na  kampeni na jumbe zilizolenga kuishi pamoja, kuvumiliana, uhusiano wetu na nyengine, kuheshimu haki, kuhifadhi wajibu, na kuzingatia maslahi ya umma kwa ajili ya ujenzi wa nchi zetu na miongoni mwa kampeni hizi: (Mapenzi ya nchi), (Imamu na Papa), (maadili ya kibinadamu), (wanadai. na tunasahihisha)

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.