Maadili ya Kusameheana na Kukubali Maoni Tofauti katika Uislamu

  • | Wednesday, 7 June, 2023
Maadili ya Kusameheana na Kukubali Maoni Tofauti katika Uislamu

       Kutokana na maumbile ya kibinadamu inatokea mara kwa mara kuwa watu kuhitilafiana mitazamo na maoni yao, lakini katika hali hii lazima kitu cha pamoja kipatikane nalo ni suala lenyewe, kwa hiyo kutofautiana ni hali thabiti inayoendelea milele kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana * Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja} [11/118 - 119].

Khitilafu iko katika aina nyingi kama vile; khitilafu baina ya watu wanao imani tofauti nayo ni khitilafu inayosababishwa na kutofautiana katika dini na itikadi na khitilafu baina ya wafuasi wa dini moja, ambapo khitilafu ya aina hii huwa kwa sura mbili:

Sura ya kwanza: Khitilafu inayokubalika ambayo iankuwa katika masuala madogo madogo kwa kuzingatia heshima ya kila mtu na huwa kwa njia ya kushauriana kama Alivyoeleza Mwenyezi Mungu: {Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashikaSala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa} [42/38]

Sura ya pili: Khitilafu isiyokubalika kisheria ambayo humpatia washiriki wake madhambi na makosa nayo ni ile khitilafu inayohusiana na mambo yaliyo thabiti na misingi ya dini isiyokubali maoni mbalimbli katika masuala yanayo hukumu wazi katika Qurani na Sunna, kwa hiyo kutofuatiana kuhusu masuala kama haya hakuwa na faida bali madhara na wasi wasi nyingi, jambo linalosababisha ghasia isiyokubalia katika dini. Aina hii ya khitilafu imekatazwa na Mwenyezi Mungu Aliposema: {Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa} [3/105] Hivyo tunaona namna Mwenyezi Mungu Alivyoahidi kuwaadhibu watu hawa kwani wanausha fitina na faraka katika dini na baina ya waumini ingawa wamepata hoja zilizo wazi. Hali hiyo hiyo Mwenyezi Mungu Ameieleza katika kauli yake: {Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada yakuwajia hiyo bayana} [98/4].

Japokuwa kuhkitilafiana ni jambo la kimaumbile lakini wakati huwa sababu ya fitina isiyokubalika hasa katika masuala thabiti ya dini, kwa hiyo Mwenyezi Mungu Amewatahadharisha waja wake wasikhitilafiane na kufarakana wakakosa umoja na mshikamano wao kama Alivyosema: {Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, walamsizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Nasubirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri} [8/46] Na kauli yake: {Wala msiwe kama wale walio farikiana nakukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Nahao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa} [3/105].

Inakumbukwa kuwa asli ya watu ni umma mmoja bila ya khitilafu yoyote, kwani mwanzo wa kuumbwa kwa wanadamu walikuwa umma mmoja kama Akivyosema Mwenyezi Mungu: {Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka} [2/213]

Khitilafu iliyoharamishwa ni ile inayohusiana na nguzo na misingi thabiti inayo hoja na dalili wazi, vile vile khitilafu inayopelekea mizozo na migongano baina ya watu, ambapo khitilafu kama hii inawagawanya watu katika makundi mbalimbali na kila kundi linakosea jingine, bali wakati mwingine hugombana au kupigana na kuwafanyana dhuluma na uadui kama Alivyoeleza Mwenyezi Mungu Aliposema: {Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka} [2/213].

Kutokana na hayo ya juu tunaelewa kuwa kukhitilafiana siyo kosa bali ni maumbile ya kibinadamu, lakini kosa ni kupandisha khitilafu mpaka ifike kiwango cha kugombana na kukufuriana na hata kupigana, ilhali khitilafu ilikuwepo kwa ajili ya kukamilishana na kushirikiana na kutafuta mambo ya pamoja na kuyakuza kwa faida ya wote pamoja.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.