Siku ya Arafa ni mojawapo ya maonyesho ya umoja wa Kiislamu

  • | Tuesday, 27 June, 2023
Siku ya Arafa ni mojawapo ya maonyesho ya umoja wa Kiislamu

Inatupasa tumshukuru Allah (S.W) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, siku tukufu, na nyakati tukufu ambazo matendo mema huwa na thawabu kubwa kabisa. Na miongoni mwa nyakati tukufu hizo ni siku ya Arafa.

Siku ya Arafa ni mojawapo ya siku kumi bora za mwezi wa Dhul-Hijjah, nayo ni siku tukufu, siku iliyokamilika nayo dini yetu, siku ya kukubali Du’aa siku ya msamaha wa dhambi; ambapo thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili. Imetoka kwa Abu Qataadah (R.A) ambaye amesema Mtume(S.A.W) akasema kuhusu Saumu ya Arafah kuwa “Inafuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake”. {Muslim}. Na imetoka kwa Mama wa Waumini, Aaishaah (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Hakuna siku Allah (S.W) Anayowaacha huru waja na moto kama siku ya Arafah”. {Muslim}.

Hapana shaka kuwa Uislamu unatilia mkazo umoja wa Waislamu katika Nyanja zote za maisha, kimaadili, kitabia, kwenye kazi, hata katika Ibada; Hakuna ibada, au tabia ya Kiislamu, au jambo la kidunia isipokuwa unakuta ndani yake wito wa umoja, tauhidi, na kielelezo cha roho ya kufungamana na usawa kati ya ummah. Kwa hivyo Umoja wa Waislamu unatakikana, kwani ni matamanio na lengo, bali ni wajibu kwetu tunapoishi chini ya utawala wa madola makubwa ya kigeni juu ya uwezo na utajiri wa watu.

Siku ya Arafa inazingatiwa kuwa ni picha halisi ya umoja wa Waislamu na nguvu zao, ambapo maana hii inafumbatwa kwa uwazi katika siku ya Arafa. Mamilioni ya Waislamu wanasimama katika safu za karibu wakiwa wameungana katika nia, dua, na mavazi ili kuhuisha mansaki Hijja Kubwa zaidi, wakimwitikia Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutangaza utumwa na utiifu Kwake Yeye pekee, kumkana kila mshirikina, na kukataa dhulma yoyote au kiburi cha kimataifa dhidi ya taifa la Kiislamu na Waislamu wote. Hakika ni siku ya umoja na nguvu za Waislamu.

Kwa mnasaba huu Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kinawausia taifa la Kiislamu kuzingatia mafunzo ya siku ya Arafa na kufungamana wawe wanguvu dhidi mdhalimu yeyote. Na kusisitiza umoja wa safu na mshikamano wa Waislamu.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.