Makundi Yanayofichwa ya ISIS na Hatari za Kurudi

  • | Tuesday, 18 July, 2023
Makundi Yanayofichwa ya ISIS na Hatari za Kurudi

     Mnamo Aprili 2023, serikali nchini Morocco iliweza kulisambaratisha kundi la kigaidi ambalo wanachama wake walikuwa wakitaka kutekeleza operesheni za kuharibisha nchini, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Sky News, siku ya Alhamisi, Aprili 27, 2023, Kundi hili lilikuwa linawajumuisha watu (13), wana umri kati ya miaka (19) na (49). Uchunguzi umethibitisha kwamba washukiwa hao walihusika katika kuandaa mipango yao ya kuharibisha, pia walikuwa na uhusiano wa kutiliwa shaka na magaidi nje ya Morocco kwa lengo la kuratibu ili kujiunga na moja ya matawi ya kundi la kigaidi la "ISIS" katika eneo la Sahel na Sahara.

Hakuna shaka kwamba makundi yanayofichwa huleta hatari kubwa, haswa makundi yanayofichwa ya kundi la kigaidi la ISIS. Ingawa ya upotevu wa udhibiti wa kundi hili katika maeneo ambayo lilikuwa linapanua nguvu yake humo, lakini bado lina uwezo wa kuafanya mashambulizi ambayo yanaathiri juu ya raia na wanajeshi kuputia kutumia makundi yake yanayofichwa, katika jaribio la kuthibitisha nguvu na mshikamano wake baada ya kupoteza viongozi wake wa kihistoria, na kugeuza macho na migogoro yake.

Makundi haya yanayofichwa yanawakilisha sehemu muhimu ya mipango yake, haswa baada ya kufuata mkakati wa kuchukua miji na uwepo wa wafuasi wake kwenye milima, majangwa, na vijiji vilivyotelekezwa. Ambapo kundi hilo baada ya kupoteza maeneo yake ya zamani lilisambaratisha mfumo wake wa kijeshi uliokuwa unajumuisha majeshi matatu (Dabiq, Ukhalifa, na Al-Asra), na lilitosheleza na baadhi ya mitandao ya kijeshi, na baada ya lilikuwa linamiliki katika Iraq peke yake vikosi vinavyozidi na wapiganaji (elfu 20) lilitosha kwa Maelfu (3) na likageuza iliyobaki kwa makundi yaliyofichwa ambayo huwatumia wakati wowote linapotaka.

Jambo ambalo linazua mbele yetu maswali kadhaa, miongoni mwa maswali haya ni: Je, kundi linawezea kurudi tena kwa uhai katika hali ilivyokuwa katika kipindi cha kuanzia 2014 AD hadi 2017 AD? Je, makundi haya yaliyofichwa yana hatari kweli? Ni mbinu gani za kupambana zinazofaa ili kuzuia kuenea kwake?.

Ili kujibu maswali haya kuhusu makundi yaliyofichwa ya ISIS, tutatafuta kuchunguza maswali haya kwa kufuatilia vipimo vifuatavyo:

Kwanza: kwa kuzingatia asili yake; Ambapo Kituo cha Ulaya cha Masomo ya Kupambana na Ugaidi na Ujasusi kilifafanua kama ni makundi yaliyofichwa yanayojumuisha magaidi ambao hawafanyi kazi kwa wakati huu, lakini wanajificha ili yawe katika mahali pasipoweza kufikiriwa ili kutekeleza operesheni za kigaidi katika siku zijazo.

Kutokana na ufafanuzi huu uliotangulia tunatoa muhtasari kwamba makundi haya yaliyofichwa yana kazi, lakini yamefichwa, na wakati huo huo daima yawe tayari na yanaongoja mwanga wa kijani ili kutekeleza uhalifu wao wa kigaidi.

Kukiri kwa baadhi ya wenye fikra kali kuliwasilisha namna ya kazi ya makundi yaliyofichwa na jinsi ya kuzifadhili, na kwa mujibu wa ripoti ya video ya kituo cha televisheni cha Al-Hadath, mmoja wa wafungwa ambaye alikuwa akisimamia moja ya makundi yaliyofichwa ya ISIS alisema kwamba idadi ya makundi haya yaliyofichwa ni kubwa sana, sawa ni ndani ya maeneo yanayodhibitiwa na kundi au nje yake, na kwamba wafuasi wa makundi yaliyofichwa huwasiliana kwa misimbo kupitia simu, na kwamba mtu anayesimamia makundi yaliyofichwa na anayetoa maagizo kwake ni gavana "anayedaiwa" katika eneo ambalo makundi yaliyofichwa yako, na kwamba wao wapo katika maeneo tofauti ya "Syria" kama vile: "Idlib", "Raqqa", "Manbij", na "Jarabulus".

Pili: kiwango cha hatari yake; Ambapo hatari ya makundi yaliyofichwa iko kwa kiasi kikubwa katika kueneza uvumi na kuwasha ugomvi kati ya wakazi wa eneo hilo, na kwa kufanya hivyo kundi halipunguzwe hatari kuliko shughuli za kijeshi za makundi yenye fikra kali. Kwa sababu ni vikosi vya siri vilivyosambazwa katika mikoa mbalimbali ili kurahisishwa kwake kufanya vitendo vya kigaidi bila ya mtu yeyote kuliona, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba moja ya kazi za makundi yaliyofichwa ni kufanya operesheni za kigaidi, lakini kwa njia ya amani, na si kwa kutumia silaha.

Makundi yaliyofichwa ya kundi la kigaidi la ISIS yameenea kaskazini, mashariki na kaskazini magharibi mwa Iraq, kaskazini mashariki mwa Syria, na Badia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, jambo linalosababisha tishio kubwa kwa uwezo wao wa kujificha na kujipenyeza kupitia njia za usalama, hii inajaalia jambo la kulifuatilia kundi ni vigumu sana kwa vikosi vya usalama, na hii inahitaji "juhudi laini" ili kuchunguza makundi yaliyofichwa na kusafisha maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa makucha ya makundi yenye fikra kali.

Tatu: Mbinu za kupambana nao, katika suala hili tunafichua kwamba operesheni za kijeshi ni muhimu katika kuondoa na kubomoa makundi haya yaliyofichwa na kusimamisha kuenea kwa ugaidi unaoelekea kwa maeneo dhaifu kutoka upande wa masuala ya usalama, pia juhudi za kijasusi zinazotegemea ufuatiliaji na uangalizi wa wafuasi na operesheni za makundi haya yaliyofichwa ili kujaribu kuyasambaratisha na kuyakausha vyanzo vyao vya ufadhili. Lakini wakati huo huo, yote haya lazima yaendana sawa sawa na juhudi za kupambana na fikra kali na kuongeza ufahamu wa maarifa, haswa kwenye vijana katika maeneo ya udhibiti wa zamani wa ISIS.

Na hatimaye, makundi ya kigaidi yakiwemo ISIS daima hutumia njia zote zinazowezekana, na pia huenda yanabadilisha mikakati yao, mipango, na hata itikadi ikiwa ni lazima, ili kurudi na kuongoza eneo tena, na kati ya hatua hizo ni uumbaji wa makundi yaliyofichwa yanayotumiwa wakati wa lazima, jambo ambalo lazima lifuatiliwe kwa uangalifu na kutayarishwa kwake.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.