Sheikh wa Al-Azhar ampokea waziri wa ulinzi wa Guinea Conakry, na kujadili njia za kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kisayansi na kiulingano

  • | Wednesday, 19 July, 2023
Sheikh wa Al-Azhar ampokea waziri wa ulinzi wa Guinea Conakry, na kujadili njia za kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kisayansi na kiulingano

     Mheshimiwa Imamu Mkuu, profesa/ Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al Azhar Al Sharif, alimpokea leo, Jumanne, katika makao makuu ya Al-Azhar, Meja Jenerali Abu Bakr Siddiqi Kamara, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Guinea Conakry; kujadili njia za kuongeza faida ya fursa za kupata masomo kwa wana wa Guinea-Conakry.
Mheshimiwa Imamu Mkuu alimkaribisha Waziri Abu Bakr Siddiqui katika Al-Azhar AlSharif, akisisitiza nguvu wa uhusiano kati ya Al-Azhar Al-Sharif na Jamhuri ya Guinea Conakry, ulioimarishwa kupitia wanafunzi wa Guinea wanaokuja kusoma katika vyuo na vitivo vya chuo kikuu cha Al-Azhar, akiashiria kuwa Al-Azhar ina wanafunzi wa kiume na wa kike 653 kutoka Jamhuri ya Guinea Conakry, wanaosoma katika viwango mbalimbali vya elimu, aidha Al-Azhar inatenga nafasi 33 za masomo kwa wana wa Guinea-Conakry; ambapo  Idadi ya wanafunzi wa Guinea waliojiunga na Al-Azhar kwa nafasi ya kusoma ni 268, na Al-Azhar ina wajumbe 21 wa Azhar nchini Guinea wanaoeneza mtaala wa Al-Azhar nchini kote, akisisitiza utayari wa Al-Azhar kuongeza nafasi za masomo unaotolewa kwa wana wa Guinea Conakry katika taaluma mbalimbali zinazokidhi mahitaji yao ya mustakabali.
Mheshimiwa Imamu mkuu alisisitiza kuwa moja ya nguvu za elimu ya Al-Azhar ni mchanganyiko wake wa elimu ya kiraia, ambayo inawakilishwa katika sayansi inayotumika, pamoja na sayansi ya kiislamu, na kwamba uhufadhi wa Al- Azhar kwa mtindo huu wa kielimu uliifanya kuwa ya kipekee katika vizazi vinavyohitimu vilivyobeba ujumbe wa Uislamu na mbinu zake pamoja na taalamu zao za kisayansi, nayo ni moja ya nguvu za Al-Azhar Al-Sharif katika historia.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Guinea Conakry ameeleza furaha yake kwa ziara ya Sheikh wa Al-Azhar, akiwasilisha salamu za Rais wa Guinea Conakry kwa Mheshimiwa Imamu Mkuu, na ufuatiliaji wake kwa juhudi za Sheikh wa Al-Azhar ya kuhudumu Uislamu na kuunga mkono masuala ya Waislamu duniani kote, na shukrani zake kwa msaada uliotolewa na Al-Azhar kwa wana wa Guinea-Conakry hasa, na wana wa Afrika kwa ujumla, na jitihadi ya Al-Azhar ya kuwalea watoto wetu kufuatia Uislamu, akisisitiza kwamba wahitimu wa Al-Azhar nchini Guinea Conakry wanapata heshima ya kijamii na kushikilia nafasi za kazi juu zaidi katika taasisi mbalimbali.

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.