Kiashirio cha operesheni za kigaidi kwenye nchi za Kiafrika kwa Mwezi wa May 2023

  • | Wednesday, 7 June, 2023
Kiashirio cha operesheni za kigaidi kwenye nchi za Kiafrika kwa Mwezi wa May 2023

Mwezi wa Mei 2023 ulishuhudia upungufu mkubwa kwa asilimia ya operesheni za kigaidi zilizoanzishwa na makundi yenye fikra kali barani Afrika, ikilinganishwa na Aprili iliyopita, kwa takriban 18.9%. Ambapo mashambulizi ya kigaidi (30) yalirekodiwa mwezi huu, na kupungua huku kwa kawaida kulisababisha kupungua kwa idadi ya wahanga na waliojeruhiwa katika mwezi huu; Ambapo operesheni hizo zilisababisha wahanga (268), (33) waliojeruhiwa, na (33) wengine walitekwa nyara, na idadi ya operesheni katika mwezi wa Aprili ilifikia (37) operesheni za kigaidi, ambazo ziliacha (432) wahanga, (118) waliojeruhiwa, na (32) wengine walitekwa nyara.

Katika mwezi huo, eneo la Sahel barani Afrika, ambalo ni chanzo cha wasiwasi, lilishika nafasi ya kwanza kuhusu idadi ya wahanga, ambapo lilishuhudia mashambulizi (10) ya kigaidi, sawa na (33.3%) ya jumla ya idadi ya operesheni za kigaidi zilizofanywa na makundi ya kigaidi katika bara wakati wa mwezi huo), ambazo zilisababisha vifo vya watu (135) na (16) waliojeruhiwa, ambapo Burkina Faso ilipatwa na Operesheni (7) za kigaidi, ambazo zilisababisha vifo vya watu (120). Mali ilikabiliwa na matukio mawili ya kigaidi, ambayo yalisababisha vifo vya watu (6) na (16) waliojeruhiwa. Kwa upande wa Niger, ilishuhudia operesheni moja iliyowaua (9), bila kusababisha waliojeruhiwa wowote.

Kwa hivyo, eneo la Sahel ndilo lililokuwa na umwagaji damu zaidi katika mwezi huu. Sababu ya hayo ni kutokana na ukubwa wa changamoto za kiusalama zinazozikabili nchi za Sahel. Ambapo Makundi yenye fikra kali yanaendelea kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya malengo ya kiraia na kijeshi. Hasa eneo la mpakani la Burkina Faso, Mali na Niger. Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kinatahadharisha kuhusu kuzidi kwa hali mbaya ya kibinadamu kwa sababu ya mzozo wa usalama.

Ama kuhusu eneo la Afrika Magharibi, lilishika nafasi ya pili kwa idadi ya vifo, ambapo limeshambuliwa na makundi ya kigaidi "ISIS katika Afrika Magharibi" na "Boko Haram" kwa operesheni (5) za kigaidi, sawa na (16.6%) ya jumla ya operesheni za kigaidi), ambazo zote zilijilimbikiza Nchini Nigeria, na zilisababisha vifo vya watu (56) na (12) waliojeruhiwa, pamoja na (33) waliotekwa nyara.

Kwa upande wake, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kinaamini kwamba vita vya umwagaji damu vinavyoendelea kati ya ISIS huko Afrika Magharibi na Boko Haram vimewalazimisha wapiganaji wengi wa Boko Haram kujisalimisha, na wakawa katika hali dhaifu tangu kifo cha kiongozi wao "AbuBakr Shekau", jambo lililosababisha kupunguzwa kwa operesheni zao za kigaidi.

Kuhusiana na eneo la Afrika ya Kati, lilishika nafasi ya tatu kwa idadi ya vifo. Ambapo eneo hilo lilikumbwa na mashambulizi (5) ya kigaidi, sawa na (16.6%) ya jumla ya idadi ya operesheni za kigaidi), ambayo yote yalisababisha vifo vya watu (44) bila ya kuwepo kwa waliojeruhiwa wowote. "Kongo ya Kidemokrasia" ilikabiliwa na mashambulizi mawili yaliyodaiwa na waasi wa "Vikosi vya Muungano wa Kidemokrasia" wanaohusishwa na "ISIS", jambo lililosababisha vifo vya watu (22). Cameroon ilikabiliwa na mashambulizi mawili pia, ambapo raia (5) waliuawa. Chad ilikabiliwa na shambulio moja la kigaidi, ambalo lilisababisha kifo cha watu (17).

Kwa mujibu wa takwimu, Afrika Mashariki imeshika nafasi ya nne kwa idadi ya wahanga. Ambapo ilishuhudia mashambulizi (10) ya kigaidi, sawa na (33.3% ya jumla ya idadi ya operesheni za kigaidi), ambazo zilisababisha vifo vya (23) na (5) wengine waliojeruhiwa. Somalia pekee ilikampwa na operesheni (6), ambazo zilisababisha vifo vya watu (23) na (3) waliojeruhiwa. Kwa upande wa "Kenya" ilishambuliwa mara mbili na zilisababisha  (2) waliojeruhiwa.

Ingawa ya kuongezeka kwa idadi ya operesheni za kigaidi, kuna kupungua kwa idadi ya wahanga mwezi huu, kwa sababu ya kuzuiwa kwa kundi la kigaidi la Al-Shabaab na vikosi vya usalama vya Somalia na washirika wa kimataifa, na Nchi ya Kenya ina jukumu kubwa katika kuwaondoa wanamgambo wa kigaidi wanaohusishwa na Al-Qaeda na juhudi zake zinazolenga kuzuia operesheni zake na kuzisitisha.

Ama kuhusu juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi barani Afrika, idadi ya vifo vya magaidi ilifikia (477) na (1466) waliokamatwa, pamoja na kujisalimisha kwa magaidi (520). Katika eneo la Sahel, juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi zilisababisha kutengwa kwa (165) na kukamatwa kwa (1400) kutoka magaidi. Ambapo magaidi wasiopungua (110) waliuawa nchini Burkina Faso, kwani serikali inalenga makundi ya waasi kaskazini na kusini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mashambulizi ya anga. Ambapo jeshi la Niger pia lilifanikiwa katika kuwaua magaidi (55) na kuwakamata (1400).

Na mashariki mwa bara hilo, hasa nchini Somalia, serikali iliwaua wapiganaji (235) kutoka kundi la kigaidi la "Ash-Shabaab", kuwakamata (13), na gaidi akijisalimisha kwa hiari kwa vikosi vya jeshi. Jeshi la Kenya lilifanikiwa katika kuwakamata magaidi (3).

Magharibi mwa bara, jeshi la Nigeria lilifanikiwa kuwamaliza magaidi (55) kutoka kwa makundi ya "ISIS Afrika Magharibi" ​​​​na "Boko Haram", na kuwakamata (50) wengine, pia (519) walijisalimisha na wakazisalimu silaha zao kwa vikosi vya jeshi.

Katika Afrika ya Kati, juhudi za vikosi vya usalama vya Kongo zilisababisha kuangamizwa kwa magaidi (20), na wengine wawili nchini Kameruni.

Kwa upande wake, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kinaamini kwamba Afrika bado inakabiliwa na changamoto kubwa zinazohitaji kuendeleza juhudi za kimataifa zenye lengo la kupambana na janga la ugaidi katika bara zima na kuzuia fikra kali inayosababisha ugaidi kwa njia kadhaa, miongoni mwa njia hizi ni kushughulika kwa sababu za msingi za ugaidi, kupambana na simulizi na mikakati ya kigaidi, na kuboresha kiwango cha kiuchumi cha watu binafsi. Hili halitafikiwa na juhudi za watu binafsi zilizotengwa na nchi jirani, Bali, ni muhimu kushirikiana na vipande vingine katika nyanja hiyo, vikiwemo serikali, jumuiya za ndani na jumuiya za kiraia, ili kila mtu aweze kufurahia usalama na utulivu.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.