Ibada huimarisha umoja na undugu na kukataa mfarakano na hitilafu

  • | Wednesday, 30 August, 2023
Ibada huimarisha umoja na undugu na kukataa mfarakano na hitilafu

 

 

      Kwa kweli ibada katika Uislamu ni zile hukumu za kisheria zilizofaradhishwa kwa mujibu wa matini thabiti katika Qurani na Sunna, pia ni wajibu ambazo Mwenyezi Mungu Alizozipitishia waja wake kwa malengo mahususi kama vile kuwajumuisha waumini kwa neno moja na hali moja na msimamo mmoja na kuwasaidia waepukane na mfarakano na mizozo.

Yeyote anayeangalia nguzo tano za Uislamu hapati taabu kutambua kuwa chanzo na msingi mkuu wa nguzo hizo zote ni umoja. Nguzo ya kwanza ambayo ni kukiri kuwa hakina anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee na kwamba Mtume Mohammed ndiye mtume wake ni Shahada ambayo hutolewa na Waislamu wote popote duniani na wakati wowote walipo. Katika nguzo ya pili ambayo ni Swala Waislamu wanatakiwa kuelekea upande mmoja wakati mmoja kwa namna moja wakimwabudu Mola Mmoja. Na katika ibada ya Saumu Waislamu wa ulimwengu mzima wanafunga mwezi mmoja kwa namna moja wakijizuia mambo haya haya. Zaka Waislamu wanatakiwa kuchangia vigezo na masharti haya haya na kutoa kiasi hicho hicho na kuwapa wastahiki ambao wana sifa hizo hizo wakati maalumu. Na mfano mkubwa zaidi kwa umoja katika Uislamu ni ibada ya Hijja ambapo Waislamu kutoka kila kona duniani wanaelekea nchi moja wakivaa mavazi haya haya kutekeleza ibada hiyo hiyo na kumwomba Mola Mmoja kwa namna hiyo hiyo.

Kwa hakika Uislamu umeweka sheria ibada kwa lengo la kuitakasa nafsi na kuisafisha kutoka maovu na shari, na kumfanya mwanadamu awe na cheo cha juu kabisa, hivyo huwa ruwaza na mwangaza kwa wengine, na kuishi katika jamii yake akiwa chanzo cha amani, usalama na umoja, akilingania kushirikiana na kukataa kupingana na kugongana na kuwatahadharisha wenzake kutokana na hatari ya kusambaratika. Ibada katika Uislamu zinasisitiza na kuelekeza kwenye maana hiyo, ambapo Swala katika Uislamu ina athari kubwa kuwaita Waislamu wawe na muungano na usawa kimwili na kimoyo, ambapo wanasimama katika mistari sawa bila ya ubaguzi wala upendeleo, wala hairuhusiwi kwa mmoja wa Waislamu ajivunia kuliko wengine japokuwa rangi, jinsia au nafasi aliyo nayo, na kuhakikisha umoja baina ya Waislamu, Swala ya Jamaa ikawa bora kuliko swala ya mmoja peke yake, kwa ajili ya kuwazoea Waislamu ushikamano, ushirikiano, usawa na umoja.

 

Jambo hilo linalowafanya waislamu japokuwa kutofautiana kwa kikabila, kilugha, kiutamaduni wasikie umoja na kushikamana, hivyo umma ushikamana na kuwa na muungano unaoupa nguvu na ustawi, kupitia kutambua na kutekeleza swala umma huwa umma wenye msimamo mmoja katika misingi na malengo yake, hatima yake, mwenendo na desturi zake, hisia na matamanio yake, matarajio na mateso yake, hivyo umma unaweza kujikomboa kutokana na unyonge, udhaifu na kutofautiana, mwenye nguvu amsaidie mnyonge, mtajiri amfadhili maskini, mdogo amheshimu mkubwa, mkubw amhurumia mdogo, hayo yote yanatokana na kuwa waislamu wote ni ndugu wanao uhusiano imara wa kuhurumiana, kusaidiana, kupendana na kukamilishana, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (S.W.): "Hakika Waumini ni ndugu" [Al-Hujuraat: 10].

Kwa Kweli, kusali pamoja msikitini kuna thawabu adhimu iliyobainishwa na Mtume (S.W.) aliposema: "Hakika Swala ya jamaa ina thawabu bora kuliko swala ya mmoja peke yake kwa alama ishirini na tano za thawabu". Hali hiyo hiyo, Zaka inawaelekeza waislamu kwenye umoja, ushirikiano na kuondoa hitilafu, ambapo ibada hiyo ambayo kimsingi ni mfumo wa kifedha na kijamii, ni mojawapo nguzo za dini hiyo na faradhi kuu zake, kwani inamlelea mwislamu na kumwandaa awe mja mwenye kumtakasa Mwenyezi Mungu peke yake, na mwanadamu mwenye manufaa kwa jamii yake. Aidha, kutoa zaka ni sifa hasa ya waumini kama ilivyo Swala, ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amezingatia kutoa zaka ni mojawapo sifa hasa za waumini Aliposema Akiwasifu waumini: "Na ambao wanatoa Zaka" [Al-Muminuun: 4]. Pia, Zaka ni ibada inayosaidia kuleta umoja baina ya waislamu sharti waihifadhi na kuitekeleza barabara, kwani inawaunganisha matajiri na mafukara, ambapo inachocheza hisia za huruma na rehma katika nyoyo za matajiri kwa maskini kwa kuwafanyia hisani na heri, isitoshe, zaka inasababisha nyoyo za mafukara ziheshimu na kupendana na matajiri kwa ufadhili wao.

Saumu iko hali hiyo hiyo ya Swala na Zaka, ambapo inaathiria vizuri mwenendo wa wafungaji saumu, bali ni mojawapo sababu za muungano wa umma na mshikamano wake. Vile vile, Saumu inachangia sana kuwaelekeza waislamu washikamane, washirikiane na wahurumiane wenyewe kwa wenyewe.

Kwa hakika tabia njema ni lile daraja la kuwaunganisha waislamu waliotoka sehemu mbalimbali na kuwahimiza waungane na kushirikiane, hivyo jamii za kiislamu zifungamane, zisaidiane na ziwe pamoja mstari mmoja kukabiliana na maadui na waovu, pia, Saumu inamsaidia mwislamu asikie huruma na rehma kwa ndugu yake. Yaliyotajwa kuhusu Swala, Zaka na Saumu ni yale yale yasemwayo kuhusu Hajj, ambapo ibada ya Hajj ni ibada inayowakutanisha waislamu walio zaidi  katika idadi yao kuliko ibada yoyote nyingine, kwa hiyo ibada ya Hajj inadhihirisha umuhimu wa umoja na muungano wa waislamu kwa ajili ya kumtakasa Mola Mmoja kwenye wakati na mahali moja, na kwa namna moja, bila ya kujali tofauti yoyote baina ya mwislamu na mwingine, wote wanakutana ardhi takatifu na mji mtukufu wa Makkah wakitoka pande zote duniani.

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.