Mtume (S.A.W.) ndiye ruwaza njema wetu na Rehema wa Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wote

Imeandaliwa na; Dkt. Ahmed Khalaf Abulfadl

  • | Sunday, 24 September, 2023
Mtume (S.A.W.) ndiye ruwaza njema wetu na Rehema wa Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wote

 

       Rehema ni mojawapo sifa ambazo Mwenyezi Mungu amewahimiza waja wake, na ameiweka kuwa mojawapo kanuni muhimu za dini ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu amemtaja Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kwa sifa ya rehema, akisema:

 . [الأنبياء: 107] (وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ)

)Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote ([Al-Anbiya:107]

Naye Mtume (s.a.w.) alikuwa rehema kwa walimwengu, katika wito wake kwa Mwenyezi Mungu, na katika uhusiano wake na watu. Alikuwa mwenye huruma kwao, mwenye upole kwao, mwenye upendo kwao, anayejitahidi kuwanufaisha na kutimiza mahitaji yao, na kuondoa yale yanayowasababishia huzuni, taabu na mateso.

Na kumfuata Mtume (s.a.w.) katika sifa ya rehema, ulikuwa ni mojawapo sababu muhimu za ustawi wa mtu binafsi na jamii, ambapo rehema huchochea upendo, msamaha, na husaidia kuondoa chuki na uadui, na kusambaza amani na maelewano kati ya watu.

Athari za kumfuata Mtume wa Rehema katika maisha ya mtu binafsi:

Kumfuata Mtume wa Rehema katika maisha ya mtu binafsi kuna athari chanya nyingi, zikiwemo:

  • Kuhisi furaha na utulivu: Rehema huchochea hisia za furaha na utulivu, kwa sababu mtu anahisi kuwa anafanya kile kinachomhakikisha radhi za Mwenyezi Mungu, na anasaidia wengine na kuwanufaisha.
  • Kuondoa hisia mbaya: Rehema husaidia kuondoa hisia mbaya, kama vile; chuki, ubinafsi, choyo na husuda, na humfanya mtu awe na mtazamo chanya na matumaini zaidi.
  • Kuboresha mahusiano ya kijamii: Rehema husaidia kuboresha mahusiano ya kijamii, na kusambaza upendo na msamaha kati ya watu wote.
  • Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu: Rehema ni mojawapo sifa za Mwenyezi Mungu, na mja anayewajibika nayo huwa anamtii na Mola wake, na Mwenyezi Mungu humtakasa duniani na Akhera.

Athari za kumfuata Mtume wa Rehema katika jamii:

Kumfuata Mtume wa Rehema katika jamii kuna athari chanya nyingi, zikiwemo:

  • Kusambaza amani na maelewano: Rehema inasaidia kusambaza amani na maelewano kati ya watu, na hufanya jamii iwe imara na yenye ustawi.
  • Kutatua tofauti na migogoro: Rehema huchangia kutatua tofauti na migogoro kati ya watu, na kuwafanya wakubaliane.
  • Kuimarisha mahusiano ya kijamii: Rehema husaidia kuimarisha mahusiano ya kijamii, na kufanya jamii iwe na mshikamano na ushirikiano.
  • Kufanikisha haki ya kijamii: Rehema inawahimiza watu kusaidia wanyonge na maskini, na kutunza haki ya kijamii.

Umuhimu wa kumfuata Mtume wa Rehema:

Kwa hakika, kumfuata Mtume wa Rehema (s.a.w.) ni miongoni mwa majukumu muhimu ya Waislamu, kwa sababu ni mojawapo dalili za kumpenda na kumtii Mtume, jambo ambalo Mwenyezi Mungu Amewataka waumini walifanya na kuwajibika nalo.

Namna za kumfuata Mtume wa Rehema katika sifa ya rehema:

Kumfuata Mtume wa Rehema (s.a.w.) katika sifa ya rehema, kunaweza kufanywa kupitia:

  • Kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika mambo yote ya maisha: Rehema ni mojawapo kanuni za Kiislamu, na kwa hivyo ni lazima sheria za Mwenyezi Mungu ziwe msingi wa mambo yote ya maisha, ili rehema iweze kuenea kati ya watu.
  • Kuwasiliana na watu: ambapo kuwa na mahusiano mazuri na watu ni sifa mojawapo sifa muhimu za waumini, kwa mujibu wa mafunzo ya dini na uongofu wa Mtume (S.A.W.)
  • Kuchangia kueneza amani na maelewano kati ya watu: Mtume Muhammad (s.a.w.) alikuwa akifanya kazi ili kuleta amani na maelewano kati ya watu, na alikuwa na mchango mkubwa kutatua migogoro.
  • Kusaidia maskini, wasiojiweza na wanyonge: Mtume Muhammad (s.a.w.) alikuwa mwenye kutoa msaada mkubwa kwa maskini na wasiojiweza, na huruma yake ilikuwa kubwa mno.
  • Kuwatendea watu kwa upole na huruma: Mtume Muhammad (s.a.w.) alikuwa mpole na mwenye huruma kwa watu wote, hata wale waliomchukia na waliopinga, bali alikuwa (S.A.W.) mwenye huruma na upole kwa wanyama na vitu visivyo hai pia.

Kutokana na hayo ya juu, sisi katika kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali tunatoa wito kwa waislamu wote duniani waongoke kwa mafunzo na tabia za Mtume Muhammed (S.A.W.) hasa katika zama ambayo Uislamu umechafushwa sana kwa bahati mbaya kwa sababu ya vitendo vya baadhi ya wanaojinasabisha kwao, ilhali wanakwenda kinyume na mafundisho ya sheria yake.

Ulimwengu wa kisasa unahitaji sana kuenea kwa upendo, upole, rehem ana tabia nyinginezo njema ambazo huchangia kuhakikisha amani na kuondoa mizozo na mateso, kwa hiyo sote tunatakiwa kuwajibika kwa tabia zake Mtume na uongofu wa Qurani kujibu yake madai yanayosambaa kuhusu dini yetu adhimu na kuthibitisha kuwa dini hiyo ndiyo dini ya msamaha, rehema na amani.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.