Al-Azhar yalaani vikali jinai za kukata Msahafu nchini Uholanzi na yaziita nchi za kimagharibi zibainishe msimamo wake wa kweli kuhusu suala la uadui dhidi ya Uislamu

  • | Tuesday, 26 September, 2023
Al-Azhar yalaani vikali jinai za kukata Msahafu nchini Uholanzi na yaziita nchi za kimagharibi zibainishe msimamo wake wa kweli kuhusu suala la uadui dhidi ya Uislamu

     Al-Azhar inaeleza kulaani kwake jinai za kukata nakala ya Msahafu tukufu mbele ya balozi kadhaa mjini Lahai nchini Uholanzi, katika mfululizo wa jinai zinazotekelezwa dhidi ya Uislamu na vitakatifu vyake, ikisisitiza kwamba kutekeleza jinai hizo hutukia sambamba na mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu, amani na ubinadamu, hiyo ndio dalili ya kukusudia kuzidisha kiwango cha uadui dhidi ya Uislamu na waislamu.

Pia, Al-Azhar inasisitiza kwamba kufanya tena jinai hizo ni dalili kwamba baadhi ya serekali za nchi za magharibi hazichukui hatua za kikweli kuhusu kuimarisha maadili ya amani na kuishi pamoja kwa amani ambazo Al-Azhar ilifanya juhudi kubwa kwa nia nzuri kuhusu kuzisambaza na kuziimarisha, na imebainishwa kwamba serekali hizo zinaandika kwa mkono mmoja wito wa mazungumzo na ushirikiano, na zinawasha kwa mkono mwingine moto wa chuki na uadui baina ya wananchi, na zinaruhusu kufanya jinai zinazoharibu majaribio yote ya mazungumzo na kuishi pamoja baina ya wananchi, na kufungua njia mbele ya jinai na uadui dhidi ya Uislamu na waislamu.

Kwa hiyo, Al-Azhar inatoa wito kwa serekali zote za kimagharibi, wananchi na ulimwengu mzima kwa kusoma kuhusu Uislamu na waislamu kwa kina, na kuufahamu vizuri kwa namna inayolingana na maendeleo na ustaarabu zinazodaiwa na nchi hizo, na kusoma vizuri sera ya Mtume wa rehema na ubinadamu (S.A.W), ikisisitiza kwamba wenye fikra potofu wanaofanya jinai kama hizo wangejua mafundisho na maadili yaliyomo katika Msahafu tukufu -Kitabu cha Mwenyezi Mungu- ambayo yanahifadhi uhuru wa wasio waislamu na kulinda haki zao, wangeaibika sana kabla ya kutenda jinai ya kukata Msahafu Mtukufu.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.