Khusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W kwa mtazamo ulio wastani na ulio mpotofu

meandaliwa na Dkt. Mohammed Abd El-Rahman Attia

  • | Thursday, 28 September, 2023
Khusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W kwa mtazamo ulio wastani na ulio mpotofu

Kila mwaka waislamu wote husherehekea kumbukumbuya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. Lakini kuna baadhi ya watu wenye fikra potofu wanaona kuwa jambo hili ni bidaa mbaya (uvumbuzi), wakitoa huja mbalimali, miongoni mwa huja hizo kuwa Mtume S.A.W, Makhalifa waongofu wake, Masahaba wake hawakusherehekea kuzaliwa kwake S.A.W. Hakika watu wa mawazo walikuwa na 'Shubha' (tuhuma) kubwa, wakiwa wanadhani kuwa wataalamu wa 'Ahlu Suna' wanafanya bidaa mbaya! Kwa kusikitisha, watu haowalitilia shaka mwenendo wa 'Ahlu Suna', jambo lililofanya watu wengi wa kawaidakuwatuhumu wataalamu wa Ahul Suna kwa upotevu na kufanya bidaa mbaya.
Ukweli ni kwamba 'Ahlu Suna' sivyo ilivyo, bali ni watu wanaofuata Suna za Mtume S.A.W. kwa dalili nyingi za kuruhusu kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume (S.A.W.), dalili hizo ni kama zifuatazo:
Kwanza, Mtume S.A.W alikuwa hufunga siku ya jumatatu kila wiki, na alipoulizwa juu ya sababu ya kufunga, akajibu kwamba siku hii ya jumatatu ni siku ya kuzaliwa kwake [Sahih Muslim: 2/819].
Pili, Mwenyezi Mungu alisema katika Qurani {Sema: "Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake (ndiyo mumepata haya)." Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hivyo wanavyokusanya} [Yunus: 58] hivyo, tunaona kuwa Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuwe wenye furaha kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, na katika Qurani imeteremka aya inayotoa dalili ya kuwa Mtume S.A.W ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wote. Ibn Abas alisema katika tafsiri ya aya hiyo kuwa fadhila ya Mwenyezi Mungu ni elimu na rehema yake ni Mtume Muhammad. 
Mwenyezi Mungu alisema katika Qurani: {Nasi hatukukutuma, (hatukukuletea) ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote} [Al-Anbiyaa: 107]. (kwa kurejelea kitabu cha Al-durr Al-Manthour Fe Altafsir Bil-Maathour – kwa Emam Al-Suyuti).
Neno 'Suna' lina maana ya 'mwenendo', na Mtume S.A.W. aliwagawanya watu kulingana na 'mienendo' yao katika aina mbili; aina ya kwanza: ni watu wanaofanya Suna mbaya na aina ya pili ni watu wanaofanya Suna nzuri. Bila shaka kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. ni miongoni mwa mienendo mazuri; wakiwa watu katika siku hii wanamkumbuka Suna za Mtume S.A.W ili waislamu wote ulimwenguni wazifuate. 
Basi, jambo hilo la kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. lina historia katika sheria ya kiislamu na kuzigatiwa kama nafila. Wataalamu wengi wa Ahlu Suna wameandika kuhusu uhalali wa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W, na miongoni mwao ni Imam Al-Suyuti aliyesema katika kitabu chake kiitwacho: (Al-hawy Lil-fatawy): "Ibn Hajar Al-Asqalany ameulizwa kuhusu kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. akajibu: hukumu ya msingi ya kufanya sherehe ni bidaa, wakiwa waja wema waliotutangulia -katika karne tatu zilizofuata kifo cha Mtume S.A.W- hawakufanya sherehe kama hiyo, hata hivyo sherehe za maulidi zimekusanya mambo mazuri na mambo mabaya, na mtu anayefanya mambo mazuri katika sherehe hiyo na kuepukana na kufanya mambo mabaya, basi kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W ni bidaa nzuri.. Na ilikuwa wazi kuwa sherehe hiyo ina asili thabiti katika Sahihi ya Bukhari na Muslim, kuwa Mtume S.A.W alipohamia kwenda Madina akajua kuwa mayahudi wanafunga 'siku ya Ashuraa', akawauliza kuhusu sababu ya kufunga siku hiyo, wakamjibu kuwa katika siku hiyo Mwenyezi Mungu Alimzamisha Firauni na kumwokoa Musa, kwa hiyo, wanafunga ili kumshukuru Mwenyezi Mungu. Basi Hadithi hiyo inaeleza kwamba mtu anapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema yake katika siku maalumu na anarudia shukrani kila mwaka katika siku maalumu hiyo hiyo.. kwa hiyo: hakuna neema kubwa zaidi kulikoneema ya kuzaliwa Mtume wa rehema S.A.W katika siku hii, basi inapaswa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W 
Vitendo vyema vinavyopaswa kufanywa katika siku hii ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W ni kusoma Qurani, kuwalisha watu, kutoa sadaka, kuimba nyimbo za kumsifu Mtume S.A.W, ama vile vitendo yanavyofanywa na baadhi ya watu kwa kudai kuwa wanahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Mtume S.A.W. kama vile; kusikia nyimbo za kumsifu Mtume, kuwafuruhisha waislamu, pamoja na mambo mengine yanayofanywa na waislamu katika siku ile,  na shughuli nyingine zinazoletea furaha myoyoni mwa waislamu ni bidaa inayokubalika 'Mubah' ".
[kwa ufupisho: Al-hawy Lil-fatawy: sehemu ya kwanza, Uk 229].
Pia, wataalamu wengi wa 'Ahul Suna' wa kale na wa kisasa wametoa fatwa kuhusu uhalali wa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W, miongoni mwao ni Al-Hafedh bin Hajar Al-asqalany, Abdallah bin Al-Haj, Al-Hafedh Al-Sakhawy, Al-Hafedh Al-Qastalany, Ibn Hajar Al-Hayatamy, Ibn Dehia, Shams Al-Din bin Al-Jazary, Ibn Nasir Al-Demeshky, Mula Ali Al-Qary, Abu Al-Faraj bin Al-Jawzy, Zin Al-Din Al-Iraqi, Abad Al-Raouf Al-Menawy.. na wenginyeo wengi. 
Kutokana na Maelezo hayo ya juu tunasema kwamba kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W ni bidaa nzuri na jambo liliokuwa kama nafila, kwa hiyo Ibn Tayimya anasema: "kutukuza kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W, labda baadhi ya watu wanaona kuwa ni msimu mtukufu unaotukia kila mwaka, na wanakuwa na ujira mkubwa katika msimu huu kutokana na nia yao nzuri ya kumtakasa Mtume S.A.W [Iqtidaa Al-Sirat Al-Mustaqim: 2/126]
Kwa hiyo, kituo cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra potofu kinaona kwamba waislamu wote ulimwenguni wapaswa kuwafuata wataalamu wa 'Ahl Suna' ambao wanaruhusu kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W.     

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.