Al-Azhar Al-Shareif yalaani kikali mashumbulizi ya kigaidi dhidi ya msikiti na sherehe ya Maulidi ya Mtume nchini Pakistan...

  • | Saturday, 30 September, 2023
Al-Azhar Al-Shareif yalaani kikali mashumbulizi ya kigaidi dhidi ya msikiti na sherehe ya Maulidi ya Mtume nchini Pakistan...

Al-Azhar Al-Shareif yalaani kikali mashumbulizi ya kigaidi dhidi ya msikiti na sherehe ya Maulidi ya Mtume nchini Pakistan, na kusisitiza kuwa: kuwalenga wanaosali misikitini na wanaosherehekea Maulidi ya Mtume hakukubaliwi na mafundisho ya Uislamu na maadili yake

 

Al-Azhar Al-Shareif imetoa taarifa ya kulaani na kukataa kilali mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga watu wasio na hatia nchini Pakistan siku ya ijumaa tarehe 29/9/2023, ambapo Shambulizi la kwanza lililenga kusanyiko la waislamu wanaosherehekea maulidi ya Mtume (S.A.W.) karibu na msikiti kwenye jimbo la Blushistan kusini magharibi mwa Pakistan, shambulizi hilo lilisababisha zaidi ya watu 50 kuuawa. Shambulizi la pili lililenga msikiti  uliopo kusini mwa mji wa Bishawar kaskazini magharibi mwa nchi hiyo wakati wa swala ya Ijumaa, shambulizi hili lilisababisha kwa uchache watu tano kuuawa na wengine wamejeruhiwa, pamoja na wengine walio chini ya maporomoko ya msikiti mpaka sasa.

Al-Azhar Al-Shareif ikilaani mashambulizi haya maovu ya kigaidi, inasisitiza kuwa mashambulizi haya yaliyowalenga waislamu katika siku za kusherehekea maulidi ya Mtume (S.A.W.) hayaambatani na mafundisho ya dini ya kiislamu na maadili yake hata kidogo, ambapo Uislamu yakataa kumwaga damu za waislamu na wasio waislamu na kutangaza uharamu wa kumwua mtu pasipo na haki kwa mujibu wa Qurani Tukufu, pia, Al-Azhar inaona kuwa jinai hizo hazihusiani na maadili ya kidini na ya kibinadamu, ambapo ni uharibifu na ufisadi katika nchi kwa makusudi, ikishadidisha umuhimu wa kushirikiana kwa pande zote  ulimwenguni kupambana na makundi ya kigaidi na fikra potofu, pamoja na kushirikiana kuondoa fikra hizo kabisa.

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inaeleza huruma yake na kuungana na serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Pakistan katika msiba huu mkubwa, ikipeleka salamu za rambarambi kwa nchi hiyo; serikali, wananchi na hasa jamaa za wahanga wa mashambulizi haya ya kigaidi, ikimwombea Mwenyezi Mungu kuwarehemu waliouawa na kutuliza nyoyo za jamaa zao, na kuwapona majeruhi haraka, na kufanikisha juhudi za timu za ukoaji na kutoa matibabu kwa kuwasaidia majeruhi, na kuilinda Pakistan na umma wa kiislamu na wanadamu wote kutoka maangamizi na maovu.

Kwa hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.