Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampongeza Rais Abdul-Fattah Al-Sisi, na Vikosi vya kijeshi na wamisri kwa maadhimisho ya 50 ya ushindi mtukufu wa Oktoba

  • | Thursday, 5 October, 2023
Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampongeza Rais Abdul-Fattah Al-Sisi, na Vikosi vya kijeshi na wamisri kwa maadhimisho ya 50 ya ushindi mtukufu wa Oktoba

     Mheshimiwa Imamu Mkuu, Profesa. Ahmed Al-Tayeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharief, ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais Abdul-Fattah Al-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kimisri, Amiri jeshi la Misri. Na watu wa Misri, na jeshi mashujaa wa kimisri; Uongozi, maafisa na askari, kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 50 ya ushindi wa Vita tukufu vya kihistoria vya Oktoba.

Imamu Mkuu wa Al-Azhar amesisitiza kwamba Vita vya Oktoba vilikuwa, na bado vitaendelea kuwa mojawapo wa vita vya kijeshi vya kushangaza zaidi katika historia ya Misri na ya ulimwengu wa Kiarabu, kwa kuonyesha ujasiri na kujitolea kwa vikosi vyetu vya jeshi na watu wetu wakuu katika kutetea nchi, kujilinda, na kulinda haki zake na heshima yake. Vita hivyo vitabaki kuwa ushahidi wazi juu ya ujasiri wa Jeshi la Misri, na uthibitisho kwamba askari wa Misri wamekuwa na bado ni ngao inayolinda na mlinzi mwaminifu aliyeilinda Misri kwa karne nyingi kutokana na maadui.

Kwa mnasaba hiyo, Imamu Mkuu wa Al-Azhar ametoa wito kwa Wamisri wote wajifunze maana ya azma, na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga nchi yetu na kuhakikisha uendelevu wake, na kwamba ushindi huu mkubwa lazima uwahimize wafanye juhudi za kuleta maendeleo ya Misri, akimwomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wetu wema wajasiri waliojitolea muhanga kwa ajili ya kuinusuru nchi, na Ailinde Misri na majeshi wake na wananchi wake kutoka kila madhara na mabaya, na kurudisha ushindi huu kwetu kwa kheri, ukuaji, ustawi na utulivu wa kudumu.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.