Mchango wa Msikiti katika kusahihisha dhana potofu na kueneza amani

Imeandaliwa na Dkt. Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 5 October, 2023
Mchango wa Msikiti katika kusahihisha dhana potofu na kueneza amani

     Kwa hakika maeneo yaliyo matukufu zaidi katika ardhi ni misikiti kwani ndiyo nyumba za Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa aliyoyasimulia na Abdulr-Razzaq kwa usimulizi wake kutoka kwa Amr bin Maymon Al-Awdiy kwamba alisema: "Niliwasikia Maswahaba wa Mtume wakisema: Hakika misikiti ni majumba yake Mwenyezi Mungu na kwamba haki ya mgeni kufanyiwa ukarimu na mwenye wa nyumba".

Na kutoka kwa Abu Hurairh (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: kwa kweli Maeneo mazuri zaidi kuliko kwa Mwenyezi Mungu na misikiti huku maeneo machafu zaidi kuliko kwa Mwenyezi Mungu ni masoko".

Pia, Mtume (S.A.W.) kubainisha kuwa mahali pazuri zaidi kuliko kwa kupokea elimu ni msikiti na akaelezea kuwa misikiti siyo nyumba za Ibada tu bali ni mahali pa kuendesha maisha na masuala yote ya umma kidini na kidunia. Kuhusu kuifanya misikiti vituo vya elimu Mtume (S.A.W.) alisema: "Yeyote anayeshika njia ya kuomba elimu Mwenyezi Mungu Anamrahisishia njia kwa peponi na watu wangekutana msikitini kwa ajili ya kusoma Qurani Takatifu na kujadiliana mafunzo yake ila utulivu ukawafika, rehma huwapata, Malaika wakawapa amani na upole na Mwenyezi Mungu Akawataja katika waja wake wanaostahiki malipo mema, na kwa hakika asiyestahiki malipo mema kulingana na vitendo vyake hatasaidiwa na nasaba yake".

Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Abi Umamah (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) amesema: "Yeyote anayekwenda msikitini wakati wa asubuhi kwa lengo la kujifunza au kufundisha heri alikuwa anastahiki kupewa malipo ya Hijja iliyokamilika kabisa".

Kutokana na hayo tunaweza kusema kuwa misikiti katika Uislamu si mahali pa kufanya ibada tu, bali ni mahali patukufu ambapo jamii inachangiwa kwa fikra sahihi na kuelimisha watu namna ya kuishi pamoja kwa amani na kusahihisha dhana na fikra potofu. Pia, misikiti ni maeneo ambapo waumini wanashindana kutekeleza ibada kwa Mwenyezi Mungu Aliyesifu hali ya waja wake hawa kwa kusema: {Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni * Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka} [24/36-37].

Kwa kweli Mwenyezi Mungu Ameitakasa misikiti na kuifunganisha na jina lake na ibada ya kujikurubia naye, kwa hiyo waislamu wanatakiwa kuitukuza misikiti siyo kwani ni nyumba ya kufanya ibada tu, bali ni nyumba ya kuendesha mambo yote ya dini mpaka masuala ya dunia. Mwenyezi Mungu Ameunganisha misikiti naye Mwenyewe katika kauli yake (S.W.): {Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu} [72/18]. Na Alitoa onyo kali kwa yeyote anayeiharibu misikiti na kuisababisha ichafuke: {Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa} [2/114].

Misikiti katika Uislamu ni taasisi za kuendesha maisha yote, ni taasisi ya kutoa elimu, malezi, mafunzo mbalimbali ya kidini na dunia, baraza la kushauriana masuala ya umma, ukumbi wa kuchagua mtawala, halmashauri ya kujadili masuala ibuka katika jamii na kutafuta ufumbuzi wake kwa jumla msikiti ni kituo cha kusimamisha dola ya kiislamu na kudhibiti umma kimaneno na kivitendo. Kwa hiyo, tunatakiwa kuzingatia misikiti na kutambua mchango wake kuendeleza hali ya umma wa kiislamu na kuwalea vizazi wanaokuja kuwa dini hiyo ina kituo chake cha msingi ambako waislamu wanaweza kupata mahitaji yao yote kimada na kiroho.

Matatizo mengi ya jamii zetu za kisasa yangerudishiwa kujadiliwa kwa mfumo wa waislamu wa kwanza walipokuwa wanajadiliana masuala yao yote msikitini wakilazimika mafunzo ya dini ambayo msikiti ndio makao makuu yake tungefanikiwa kupata ufumbuzi wa matatizo yetu haya na kuepukana na shida na mashaka tulizo nazo siku hizi.

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kinasisitiza umuhimu wa misikiti katika kurekebisha hali ilivyo katika jamii, kwani mengi ya matatizo ya zama za kisasa huhitaji hekima kuyatatua mbali na mapambano ya kutumia nguvu, lakini kutumia akili na busara zaidi kuliko maoni binafsi. Misikitini upo utulivu na amani ya kiroho ambayo huchangia kufikia suluhisho lililo sawa kwa tatizo lolote, hivo, waislamu wanatakiwa kuhuisha na kutukuza nafasi ya msikiti katiak jamii.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.