Taarifa ya Al-Azhar kuhusiana na hali ya mambo nchini Palastina

Jumamosi 7 Octoba 2023

  • | Saturday, 7 October, 2023
Taarifa ya Al-Azhar kuhusiana na hali ya mambo nchini Palastina

Al-Azhar yapeleka salamu za rambirambi kwa ulimwengu ulio kimya kwa ajili ya wahanga wa #Palastina ikieleza heshima yake ushujaa wa wapalastina na kumwomba Mwenyezi Mungu Awasaidia kuvumulia na kupambana na udhalimu wa wajeuri wa kizayuni na ugaidi wao pindi ulimwengu mzima unakaa kimya.

Al-Azhar Al-Shreif yapeleka salamu za rambirambi kufuatia vifo vya mashuhadaa wa ummah wa kiislamu na wa kiarabu, mashuhadaa wa Palastina; nchi ya ushujaa waliopata sharafu ya shahada wakitetea nchi yao na umma wao, wakijitolea muhanga badala ya suala la uhuru na heshima yetu na ya umma wao, suala la Palastina, ikimwombea Mwenyezi Mungu Awape mashujaa wa Palastina nguvu na uvumulivu wa kupambana na udhalimu na ugaidi wa kizayuni.

Ikisikia fahari kubwa, Al-Azhar Al-Shareif inapongeza na kueleza heshima yake kwa juhudi na ujasiri wa wapalastina ikiwataka ulimwengu ulio na uelewa na ustaarabu na jamii ya kimataifa kuangalia kwa makini na kufikiri kwa hekima kuhusu ukaliaji wa muda mrefu zaidi katika historia ya kisasa, ni ukaliaji wa kizayuni kwa nchi ya Palastina, ikisisitiza kuwa ukaliaji huo ni upungufu mkubwa na aibu iliyo wazi kwa jamii ya kibinadamu ya kimataifa ambayo haina uadilifu hata kidogo wala haitambui usawa, bali siasa zake ni za upendeleo hasa kwa mambo yanayohusiana na suala la Palastina.

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inatangaza kuwaunga mkono wapalastina wale taifa walio na subra na ushujaa, ikifurahia ujasiri wao uliohuisha imani yetu na kufufua roho ya matumaini ya mustakabli yenye ushindi mkubwa, na kuturudishia uhai wa umoja na ushujaa wa kuondoa dhuluma na ujeuri baada ya kukata tamaa kuwa itarudi tena kamwe, tunamwombea Mwenyezi Mungu Awape mashujaa hawa subra, uvumulivu, utulivu na nguvu, ikisisitiza kuwa hatima ya ukaliaji wowote ni kuondolewa ingawa baada ya muda mrefu au mfupi.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.