Vijana ndio Silaha ya Umma wakati wa Amani na Vita

Imeandaliwa na: Dkt. Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 9 October, 2023
Vijana ndio Silaha ya Umma wakati wa Amani na Vita

      Kwa kweli vijana ndio uti wa mgongo wa umma wowote na sababu ya ustawi na maendeleo yake na jiwe la msingi la kujenga ustaarabu wake, pia wao ndio silaha ya nchi na mstari wa mbele wa kuilinda nchi yao katika hali zote za amani na vita kwani wana sifa za kuwasaidia wawe na uwezo wa kiakili na kimwili wa kuwawezesha kubadilisha hali na kuendeleza nchi wakati wa amani na kuitetea wakati wa vita.

Vijana ndio msingi wa maendeleo ya umma na tegemeo la mwamko wake, kwa sababu vijana ni ukwasi ulio ghali wa umma, maana umma wowote huwa na hazina mbalimbali .. hazina za kiuchumi, kijeshi, kijiografia, na za kibinadamu, lakini hazina iliyo muhimu zaidi kwa umma ni hazina ya kibinadamu, ile hazina ambayo inaundwa na kuimarika sana kwa vijana.

Kama ungetaka kujua mustakabali wa taifa lolote, basi usiuliza juu ya dhahabu yake na hazina yake ya kifedha, lakini unaweza kuangalia vijana wake na mambo gani wanayoshyghulikia nayo,basi ukiwakuta vijana hao wanashikilia Dini, basi utambue kuwa ni taifa kubwa lenye hadhi nzuri na ujenzi nguvu, ama ukiwakuta vijana hao ni wamepoteza maadili wakawa na tabia mbaya wakishughulikia mambo duni na maovu, basi ujue kuwa ni taifa dhaifu (nyonge), litakaoanguka kwa haraka mbele ya madui wake, kwa hivyo basi vijana ni msingi wa umma na sababu ya kuimarika au kuanguka kwake.

Kwa hakika vijana walikuwa katika zama za kale na za kisasa kwa taifa lolote ni msingi wa mwamko na ustawi wake, nao katika kila mwamko ni siri ya nguvu zake, nao katika kila wazo ni wenye kubeba bendera yake Mwenyezi Mungu Amesema kueleza hali ya vijana wa Al-Kahf: "Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu" [Al-Kahf: 13]. Kwa hiyo, vijana wana umuhimu mkubwa katika maendeleo na ujenzi wa jamii, na roli yao yao haihusiani na uwanja maalumu, bali inaingiliana na nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi, na sekta mbalimbali za ustawi, kwani wo ndio wanayo tamaa na matarajio zaidi kuliko katika jamii, na kwa kuwa harakati (mchakato) ya mabadiliko, marekebisho na maendeleo haiishii mipaka maalumu kwao, kwani wao ni msingi wa mabadiliko na nguvu unaoweza kuyafanya, kwa hivyo, taasisi, makampuni na bodi za umma zinatakiwa kuvuta nguvu zao na kuzitumia kwa manufaa ya umma.

Kwa kweli, vijana waiislamu walikuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa umma na mataifa, ambapo na juu ya mabega yao staarabu zimezuka, na walikuwa na athari kubwa katika mwamko wa umma wa Kiislamu katika zama zote na nyanja tofauti, wakastahiki kuwa ni mifano mema na ruwaza njema kwa vijana wa umma katika zama zote.

Vijana ndio wa kuitikia haraka wito za kimarekebesho, ambapo wamekabiliana na ubatili, na walikubali na kukiri haki, kwani huwa na nyoyo nyepesi zenye huruma, na kwa kuwa wana roho nyamavu, na hawana matarajio katika maisha kama hali ya wakubwa na mabwana ambao kila anapowajia Mtume walikuwa wanamkadhibisha, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema kuhusu watu wazima waliokuwa wanaongoza kaumu wao kwenye njia ya upotofu na ukafiri: "Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao(23) Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa (24)" [Az-Zukhruf: 23-24]. Ilhali vijana walikuwa ndio wa kwanza kukabiliana na ubatili kwa imani na uthabiti kama ilivyotokea na Bwana wetu Ibrahim (A.S.), alipohojiana na kaumu wake, na kama ilivyotokea na‎ watu wa pango (Al-Kahf) ambao walikuwa vijana kupambana na mfalme dhalimu.

Miongoni mwa mifano bora iliyopigwa ya vijana wema katika enzi ya Maswahaba ni Zaid Ibn Thabit ambaye ni mfano mzuri sana aliyeusiwa na Mtume (S.A.W.) ajifunze lugha ya kisiriani. Zaid Ibn Thabit alisema: Mtume (S.A.W.) aliniambia: "Je, unajua kisiriani? Nikasema: hapana. Mtume (S.A.W.) akasema: uijifunze, kwa kuwa risala na vitabu vyake vinatujia. Zaid alisema: basi nikaijifunza katika siku kumi na saba". Al-‘Amash alisema: Mtume ‎(S.A.W.) ‎alikuwa anatumwa vitabu ambavyo hapendi kuviangalia ila anayemwaminika, hivyo Zaid alipewa lakabu ya mfasiri wa Mtume. Kumbe! mfasiri huyu wa Mtume ‎(S.A.W.)‎ alikuwa na umri gani? Miaka 13!!

Baada ya hayo amepewa kazi ya kukusanya Qur’ani katika enzi ya utawala wa Bwana wetu Abu Bakr (R.A). Ambapo baada ya kifo cha Mtume‎ (S.A.W.),‎ waislamu walishughulikiwa vita vya uasi, na katika vita vya Al-Yamamahm, idadi ya mashahidi wanaohifadhi Qur'ani Tukufu ilikuwa kubwa, kwa hiyo Omar Ibn Al-Khattab (R.A.) baada ya vita kumalizika na moto wa fitna uakazimwa kabisa, alikwenda kwa Khalifa Abu Bakr akimpa shauri la kuikusanya Qur'an kabla ya wengine wa wahifadhi na wasomaji wa Qur’ani hupatwa na kifo. Khalifa Abu Bakr aliomba Istikhaarah kutoka Mola wake na kuomba ushauri wa maswahaba wenzake, kisha alimwagiza Zaid Ibn Thabit aanze kazi hiyo ya kukusanya Qur'ani kwa msaada wa baadhi ya maswahaba wenye uzoefu.

Zaid alisimama na kumaliza kazi hiyo barabara, ambapo alikuwa analingana na kupinga na kuchunguza mpaka alikusanya Qur'ani na kuipanga vizuri . Zaid alisema kuhusu ukubwa na uzito wa jukumu hilo: (Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau wangalinikalifisha kwa kuhamisha mlima kutoka mahala pake hadi pengine, basi ingalikuwa nyepesi kwangu kuliko kazi niliyokalifishwa nayo; ambayo ni ukusanyaji wa Qur'ani). Mwishoni, Zaid japokuwa ujana wake, alimaliza kazi hiyo kwa ukamilifu na kukusanya Qur'ani katika msahafu moja.

Enyi vijana wa umma wetu! Tambueni nafasi yenu na majukumu yenu kuhakikisha ustawi na maendeleo ya umma wenu, msiwe sababu ya shida za umma wenu, msidanganyi kwa madai maovu ya makundi ya kigaidi wala msiathirike kwa fikra zao potofu, tambueni kuwa maslahi na mustakbali wa umma na jamii yenu hufungamana na kutegemea michango yenu na juhudi zenu katika kukuza na kuimarisha amani na utulivu katika jamii zenu.

Wakati wa amani na wakati wa vita nyinyi ndio sababu ya kuhakikisha ushindi na mafanikio ya umma na jamii, hivyo jitahidini kuwa na elimu, ujuzi na uvumilivu wa kutosha kutekeleza majukumu yenu kwa jamii, umma na ulimwengu mzima.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.