Taarifa ya kituo cha Al-Azhar cha kutoa Fatwa kuhusu tukio la kuwashambulia watalii

  • | Monday, 9 October, 2023
Taarifa ya kituo cha Al-Azhar cha kutoa Fatwa kuhusu tukio la kuwashambulia watalii

    Kwa hakika, Sheria ya kiislamu ilipambanua baina ya haki a mdhulumiwa anayetetea nafsi na ardhi yake, na baina ya kumshambulia “aliyepewa amani” aliyeruhusiwa na nchi kuiingia kupitia viza, ambayo ni ahadi ya amani na inayodhamini usalama wake.

Kwa hiyo Uislamu haikuruhusu kumdhuru mwanadamu anayepewa amani na nchi kupitia viza ya kuiingia, kwani kwa mujibu wa viza hiyo mgeni amepewa haki ya amani na usalama, na jamii inadhamni usalama wake na kusaidiana na kumlinda yeye na kuhifadhi damu yake, sawa sawa akiwa mwislamu au si mwislamu, na huyo anaitwa katika sheria “anayepewa  amani au mwenye ahadi” kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake (S.A.W) {Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu},[Al-Tawbah:6], aya tukufu inasisitiza kukataza kumshambulia aliyepewa amani, naye ni mwanadamu anayekwenda kwa nchi kwa mujibu wa kanuni inayopanga mambo yake, bila ya kujali dini, kabila au dini yake.

Watu waliopewa amani ni pamoja na wanafunzi wageni, mabalozi, wafanya biashara, watalii na wengine. Na aya na hadithi zilizohusiana na suala hilo ni nyingi na miongoni mwa hadithi hizo ni ile hadithi iliyopokelewa na Mtume (S.A.W) “Mtu yeyote anayempa mwingine amani ya kulinda damu yake  na kumwua; basi mimi ni hasimu wake, hata akiwa aliyeuwawa ni mkafiri”. Na hadithi iliyopokelewa na Ibn Habban, kwa hiyo kituo cha Al-Azhar cha kutoa Fatwa kinatahadharisha kufuata fikra potofu inayoathiria vibaya utulivu na usalama wa jamii, tukimwomba Mwenyezi Mungu azilinde damu zetu na nchi yetu kutoka kila shari. Na swala na salamu za Mwenyezi Mungu zimfikie Mtume Muhammad (S.A.W), familia yake, masahaba wake, na taabiina.  

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.