Al-Azhar yaamkia upya uvumilivu wa Wapalestina na kushikamana kwao na ardhi yao tukufu

  • | Thursday, 12 October, 2023
Al-Azhar yaamkia upya uvumilivu wa Wapalestina na kushikamana kwao na ardhi yao tukufu

 

     Al-Azhar inaamkia upya uvumilivu wa Wapalestina, na kuthamini sana kushikamana kwao kwa ardhi yao tukufu, na utiriri wao wa kubaki kwenye udongo wake, bila ya kujali hatari na mauaji, kwani ardhi ni kama heshima na utukufu, na Al-Azhar inatoa ujumbe wake kwa wale wanaoshikamana na ardhi yao kwamba ni bora kwenu kufa mkiutetea ardhi yenu kama mashujaa, mabingwa na mashahidi kuliko kuiacha kwa wakoloni, na tambueni kwamba kuacha ardhi zenu ni tangazo la kifo kwa suala yetu sote na sababu ya kulifuta milele.

Al-Azhar inazitaka serikali za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kweli na za pamoja kuhusu kukabiliana na msimamo isiyo ya kibinadamu ya nchi za kimagharibi zinazounga mkono ukiukaji wa Wazayuni kwa haki zote za Wapalestina wasio na hatia, na kufanya uchunguzi wa kimataifa kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na bado zinaendelea na Wazayuni dhidi ya watoto, wanawake na wazee katika Ukanda wa Gaza uliozungukwa na kutengwa.

Aidha, Al-Azhar inatoa wito kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu kutambua wajibu wake wa kidini na kihistoria, na kuharakisha zoezi la kutoa misaada ya kibinadamu, na kuhakikisha kuipitisha kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Na Al-Azhar inabainisha kwamba kuunga mkono Wapalestina wasio na hatia kupitia njia rasmi ni wajibu wa kidini, kisheria, kimaadili na kibinadamu, na historia haitawataja kwa kheri wale wanaopuuza wajibu huo.

Al-Azhar inasema kwamba kuwalenga raia, wakiwemo wanawake, watoto na wazee wasio na silaha, na kushambulia hospitali, masoko, magari ya kubebea wagonjwa, misikiti na shule ambapo raia wanakaa, na mzunguko mkubwa kwa Ukanda wa Gaza kwa njia hii isiyo ya kibinadamu, na kutumia silaha nzito zilizopigwa marufuku kimataifa na kimaadili, kukata umeme na maji, na kuzuia kufikisha chakula na misaada ya kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza, hasa hospitali na vituo vya afya – hayo yote ni mauaji ya halaiki, na jinai kamili za kivita, na fedheha itakayoandikwa na historia dhidi ya Wazayuni na wafuasi wao, na wale wanaowaunga mkono.

Zaidi ya hayo, Al-Azhar imesema kwamba uungaji mkono usio na mipaka na usio wa kibinadamu wa wamagharibi kwa Wazayuni, na kubariki jinai zao, na tunachokiona kutoka upendeleo na ubaguzi wa vyombo vya habari vya Kimagharibi dhidi ya Palestina na wananchi wake, ni uongo unaofichua madai ya uhuru ambao Wamagharibi wanadai kuyatetea na kuyalinda, na udanganyifu kwa maoni ya umma duniani, na kuhusika katika kuunga mkono jinai na nguvu dhidi ya Wapalestina wasio na hatia; na kufungua njia mpana kwa jinai za kikatili na za kigaidi zinazofanywa na mamlaka ya kizayuni nchini Palestina.

Taarifa hiyo ya Al-Azhar imehitimishwa kwa kusema kwamba: ulimwengu wote lazima watambue, bali lazima dunia nzima ijue kwamba bila shaka ukoloni itaondolewa, sasa hivi au baadaye.

 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.