Imamu Mkuu wa Al-Azhar: Tuko tayari kuongeza idadi ya tuzo za masomo kwa wanafunzi wa Rwanda

  • | Wednesday, 18 October, 2023
Imamu Mkuu wa Al-Azhar: Tuko tayari kuongeza idadi ya tuzo za masomo kwa wanafunzi wa Rwanda

     Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Profesa/ Ahmad Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, amepokea Balozi/ Nermin Al-Zawahri, Balozi wa Misri nchini Rwanda, ili kujadili njia za ushirikiano wa Al-Azhar na Rwanda katika nyanja za kisayansi na Da'awa.

Mheshimiwa Imamu Mkuu alisisitiza kuwa Al-Azhar inawajali sana ndugu waafrika, na inawakaribisha daima wanafunzi wa nchi mbalimbali za kiafrika katika vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Al-Azhar. Akisisitiza utayari wa Al-Azhar kwa kuongeza idadi ya tuzo za masomo kwa wanafunzi wa Rwanda ili kusoma katika Al-Azhar, na kutenga sehemu kubwa zaidi yao ili kusoma katika Vitivo vya sayansi za kiutendaji. Kama vile kitivo cha Tiba, kitivo cha Madawa, na kitivo cha Uhandisi, ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Rwanda katika nyanja hizo.

Pia, Mheshimiwa Imamu Mkuu alitangaza utayari wa Al-Azhar wa kuanzisha kituo cha Al-Azhar cha kufundisha lugha ya Kiarabu nchini Rwanda, kwa ajili ya kuwahudumia jamii ya Kiislamu na watoto wa Waislamu nchini humo, akisisitiza kuwa Al-Azhar inawakaribisha maimamu wa Rwanda, ili kujiunga na Al-Azhar Academy ya kutoa mazoezi kwa maimamu, na kuwapa mazoezi ya kujibu tuhuma za makundi yenye fikra potofu, na kuimarisha maadili ya udugu na kuishi pamoja kwa amani, na kubuni mtalaa wa masomo unaoafikiana na jamii ya Rwanda na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea ambavyo vinahitaji kufanya kwa bidii ili kuimarisha maadili ya uwananchi.

Kwa upande wake, Balozi Nermin Al-Zawahri alielezea furaha yake kukutana na Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar, na akithamini juhudi zake za kuimarisha maadili ya udugu na kuishi pamoja kwa amani na kusaidia waafrika. Akisisitiza kushughulikia faili la wanafunzi wa kigeni hapa Misri na kuleta maimamu kwa ajili ya kupata mazoezi katika Al-Azhar Al-Sharif, akiahidi kufanya juhudi kubwa kuhusu kudhihirisha jukumu na juhudi za Al-Azhar Al-Shareif nchini Rwanda.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.